Naona namba 11:11 kila mara

iamriq_arthur

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2021
Posts
440
Reaction score
1,086
Natumai mu wazima wa afya,

Twende moja kwa moja kwenye maada kuu, kama watu wa kiroho wanavyotafsiri alama hii 11:11, kuhusu alama hiyo kwa upande wangu kila siku naiona kwenye mizunguko ya maisha yangu, na tafsiri yake ni kuwa baada ya kuiona hyo namba mara kwa mara hivi karibuni utarajie upokea mambo mazuri.

Lakini kwa upande wangu tangu nianze kuiona namba hiyo ni muda sasa natarajia kupata nafuu ya maisha lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya tu na maisha yanazidi kuwa magumu, mfano siku ya leo hii namba

11:11 nimeiona mara 3 ikijirudia sehem mbali mbali lakini mambo yangu yanazidi kuwa magumu,

Je naweza nikawa nakosea mahala ndo ikawa sababu ya hii namba kutofanya kazi???
(11:11 angel numbers)
 
Kwa mfano hapo ulivyoweka bandiko lako na sisi tukaiona kwa mara ya kwanza. We unakuwa unaiona mara ya ngapi mtu anapotoa mchango wake notification ikikujia?. Na sisi tutegemee mafanikio?

Fanya kazi kijana hakuna hela za UNICEF wala WHO.
 
Katika moangilio wa numerology, nambari 11 inachukuliwa kuwa "nambari kuu" na inasemekana kuwa na mzunguko wa juu wa vibrational na maana ya kina. Wengine wanaamini kuwa kuona nambari 11 ni ishara kutoka kwa ulimwengu au malaika wako wa walinzi kwamba unapaswa kuzingatia uvumbuzi wako na safari ya kiroho. Inaweza pia kumaanisha kuwa unakaribia kupata mwamko wa kiroho au kuingia katika awamu mpya ya maisha yako.
 
Kwa akili hizi ccm bd wana miaka mingi ya kutawala
bora mleta mada kwa comment yako ccm inaonyesha ccm itatawala miaka nenda rudi.

Majibu ya matatizo ya dunia yapo kwenye ulimwengu wa roho. Wazungu wanatupiga gape kwasababu ya mambo kama haya.

Yote unayoyaona duniani yashafanyika katika ulimwengu wa roho kinachofanyika sasa ni utekelezaji tuu.

Unaonekana hupendi kusoma unachojua ni vijembe. Nakuwaza ushirikina ndo maana mleta kaleta jambo la msingi ukakurupuka bila kutuliza akili.
narudia kwa akili yako ccm itaendelea kutawala.
 
Reactions: K11
Km taifa tuna hitaji kuimarisha sekta ya afya hasa kitengo cha afya ya akili
 
Number 11, ilishachakachuliwa
Mitume walikuwa 11, kila walipoenda walijaza.
Timu ya mpira wachezaji 11,
Sina namna rahisi ya kukufanyia spoon feeding,
ujaelewa na siwezi kuelezea zaidi, pambana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…