Naona nimpe sunspension kama ya mwezi hivi

Paul dybala

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2023
Posts
524
Reaction score
2,097
Wakuu, poleni kwa kuwasumbua sana. Ni vile naipenda familia yangu na pia naipambania sana licha ya mwenzi wangu kutokuwa na shukrani.

Huenda yote haya yanatokana na kuzoeana sana ndani ya nyumba, yaani ile hali ambapo ugomvi huanza, halafu anajua kuwa hata nikinuna, mwisho wake huwa ni mwepesi tu. Kwa hiyo, anajua siwezi kufanya chochote.

Iko hivi wakuu, hapa tulipopanga tunaishi kwenye vyumba ambavyo ni vya shilingi 50,000 na 60,000. Sasa, mwenye nyumba hupokea kodi za mwaka mzima, hana habari ya miezi sita, miezi mitatu, au miezi sita—ni mwaka mzima.

Sasa kwa mimi, kazi yangu ya boda ni ngumu sana kupata hiyo hela kwa muda mfupi. Hunichukua mpaka miezi miwili kuikamilisha. Ni mpambano wa kuvuja jasho haswa, asubuhi hadi kulala saa sita usiku, na hivyo ninamshukuru Mungu sifanyi marejesho sehemu yoyote, ni ya kwangu. Wakati huohuo, mimi napambana na nimefanikiwa kupata kodi ya miezi kumi nikamkabidhi mwenye nyumba na kumsihi anivumilie japo wiki mbili nimalizie laki moja ili iwe laki sita kusudi niwe nimelipia mwaka mzima.

Kumbe huku mwenzangu hakitaki chumba cha shilingi 50,000, yeye anataka cha 60,000.

Ilitokea mvutano kwelikweli, mpaka baadhi ya huduma zilikuwa zimesitishwa. Mwanamke kavimbisha sura, amenuna hadi hivi navyoandika hapa, eti kisa sijalipia chumba cha shilingi 60,000.

Mimi nimejaribu kukaa naye chini kumueleza kuwa mbona kabla sijafukuzwa mishe kule kwa mchina kila kitu kilienda sawa? Iweje hii ndio iwe sababu ya kugombana humu ndani? Hiki chumba kina shida gani, kwani?

Okay basi, kama unaona ni shida na hukipendi chumba, jaza hela yako. Yaani, atoe 120,000, mimi nimalizie ile laki moja niliyoahidi kwa mwenye nyumba. Kama ni rahisi hivyo.

Kuna siku jirani, mama mmoja kamfumbia eti anaosha vyombo vya plastiki tu. Yaani, alivoniambia, hadi nikacheka tu. Nikampa hela akanunue vya udongo. Maisha ya kuigana iguana, ili mradi tutumie hela ovyo, tukose hata akiba.

Nimemueleza kuwa hakuna kitu kizuri kama kuishi kwako sababu una uhuru—unajua upike nini, ule nini. Hii ni tofauti kabisa na ukiwa kwa mama yako; uhuru huna. Ila kama anahisi hapamfai kwangu, mimi ninamrejesha kwao ili nifanye mambo yangu. Nataka nifocus kwenye kazi, ninunue hata kiwanja.
 
Kusema kweli ni wanawake wachache wanaoweza kuvumilia anguko la kiuchumi na kukuchukulia kwa upendo wa kama mwanzo

Yatapiiita, yanamwishooo....
 
Tafuta hela mwamba! Utakaaje room 1 na manzi?
 
Pole sana ila RULE NO.1
Mwanamme huwa hamnunii mkewe

RULE NO.2 Mwanamme ndio kichwa cha familia unatakiwa ukisema chumba ni cha sh 50 elf hakuna kuhoji tena

RULE NO.3 Tafuta hela soon unaenda kut***ewa

N.b una material wife Na sio wife material.
 
Mkuu samahani kama natumia maneno magumu ila lazima nikuambie ukweli kwamba huyo mwanamke wako hakupendi thus anafanya hivo ili apate tu sababu mgombane then amwage moto
 
Mkuu samahani kama natumia maneno magumu ila lazima nikuambie ukweli kwamba huyo mwanamke wako hakupendi thus anafanya hivo ili apate tu sababu mgombane then amwage moto
Huo ndio ukweli, bila kumuhurumia mtoa mada.
Vinginevyo ni ataishia kuonekana kuwa analalamika tuu. Yaani mwanamke amemfanya jamaa awe mtu wa kulalamika tuu.

Cha msingi hapo ni mwisho wa siku kufanya maamuzi magumu tu. Kwa izo tabia za mkewe jamaa ni atakuwa mlalamikaji na kuonekana mlalamishi kila wakati.
 
Hivi huyu manzi ndio yule aliyekuwa anakunyima utamu mpaka ukapanga umtimue?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…