Naona noma kwenda gym na kamwili kangu kembamba

Naona noma kwenda gym na kamwili kangu kembamba

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Habari

Muda mrefu nimekuwa nikitamani kuanza mazoezi ya mwili gym, lakini mara zote huwa napatwa na hofu kuwa pale gym mimi pekee yangu ndio nitakuwa kimbaumbau

Wale watu wa gym mliwezaje kuanza mkiwa na mili yenu membamba mimi naona noma wakuu.
 
Mwili mwembamba ndio mzuri wa mazoez ,ukiwa linene ukipiga tizi unafutuka kama kiroba wala hautapendeza ila ukiwa mwembamba ni rahisi mno kukata misuli unakula tu chakula cha protein kwa wingi mboga za majani ,matunda na maji ya kutosha ili ngozi isikauke mkuu.
 
Mimi nilikuwa mwembamba hivi sasa nishajipata baada ya gym wala hakuna wakukucheka jiamini....unaanza na kilo kumi bench au 15.
Mwembamba kukata packs ni chap ikiwa huna kitambi.
 
Sasa ndugu unaweza kuendesha familia kweli km mambo madogo tu yanakupa mtihani
 
Back
Top Bottom