BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Huko CWT hali siyo shwari. Ni juzi tu mdau mmoja kaleta Uzi juu ya manyanyaso ya vyama vya wafanyakazi Tanzania hasa CWT (Chama Cha Walimu Tanzania). Wadau wengi tulichangia sn hapa. Sasa kumbe ni km tulitia petrol kwenye moto. Leo naamka nakutana na gazeti la NIPASHE likiwa na habari ya Walimu wetu wanaodhulumiwa na CWT. Nikajisemea kimoyomoyo "kumbe mapendekezo ya mtaala wa Elimu umekuja na kuwabadilisha Walimu".
Miaka mingi chama Cha Walimu (CWT) kimekuwa kikinyooshewa vidole na Walimu lakini kwa vile Kuna watu Wana maslahi nacho wamekuwa wanakikingia kifua.
Sasa naona kifo chake kimefika. Sasa Walimu wanakimbilia chama kingine kipya naskia kinaitwa CHAKUHAWATA ( sijui hata kirefu chake). Huko wanasema makato ni 5,000 kwa wote bila kujali una daraja gani la mshahara.
Hongera sn wasomi na wataalamu wa watoto wetu sasa kuzitambua haki zenu na kuondokana na kasumba ya uoga, kwa heri CWT. Na mliohama wasaidieni na wengine waliobaki waondoke hasa zile sehemu ambazo Halmashauri zao zimekuwa zinahongwa na CWT ili waajili wenu wasisaini barua zenu za kuondoka CWT.