Mimi nasoma chuo kikuu hapa Tanzania. Mwaka jana mwezi wa tisa nilinunua plot lakini niliporudi chuo ndugu zake na muuzaji ambao ni wa kike walienda mahakamani wakidai mimi na mwenyekiti wa mtaa aliyeandikisha hayo makubaliano yetu eti tumekula njama ya kuuza ardhi ya familia wakidai eti muuzaji ni kichaa lakini huyo huyo muuzaji alishawahi kuuza plot nyingine shahidi akiwa huyo huyo mama anayenishitaki. Kumbuka hizi plot zinatolewa kwenye shamba moja kubwa. Mimi niliitwa mahakamani na ndugu zangu walipodai kuwa nipo chuo wanaonishataki pamoja na hakimu wa primary court walidai mimi siko chuo yaani hawakuamini. Na kesi iliamuliwa kuwa ile plot niliyoinunua kurudi kwa wale walalamikaji na mahakama iliamuru mimi nisilipwe, kesi iliisha mahakamani bila mm kujua kama natafutwa na ndugu zangu walilazimishwa kulipa hela za kufuta kesi na kulipa usumbufu wa walioenda kunishtaki na wameshalipa takribani million moja na laki nane. Je nitawezaje kuanzisha upya shauri langu lisikilizwe upya? Au sheria hairusu jamani? Nategemea kwenda nyumbani mwezi wa saba nikiwa nimemaliza chuo sasa sielewi nianzie wap. Kesi iliisha tar 5 mwez wa kumi na moja 2013. Ahsanteni naombeni msaada.