RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖MHADHARA WA 14:
Sisi tunaokuja kuomba kazi kwenye maofisi yenu huwa mnatuomba UZOEFU. Swali kubwa mnalotuuliza; "Una uzoefu wa miaka mingapi kazini?"
Hakuna shida; ubaya ubwela. Ngoja basi na sisi tuwaambie jambo hili kwa herufi kubwa; BIASHARA NA YENYEWE INAHITAJI UZOEFU. Kama unasubiri kustaafu au ufukuzwe kazi ndio uanze kufanya biashara, ni lazima biashara itakuuliza; "Una uzoefu wa miaka mingapi kwenye biashara?"
Kama huna UZOEFU WA KUFANYA BIASHARA, maisha ya biashara yatakutimua mtaani bila huruma kama ambavyo nyinyi mnatutimua sisi (tusiokuwa na uzoefu) tunaokuja kuomba kazi maofisini kwenu.
Sisi hatuna roho mbaya ndo maana leo tunawakumbusha jambo zuri sana kwasababu huwa tunashuhudia jinsi pensheni zenu zinavyoteketea mtaani. Ndugu mwajiriwa huzuiliwi kufanya biashara pindi ukiwa umeajiriwa, anza kufanya biashara mapema ili uzoee changamoto za biashara. Kama ajira inakubana (huna muda) hebu mfungulie biashara mkeo/mumeo ili awe anakusimulia changamoto za biashara pindi mkiwa kitandani usiku. Kama unasubiri Kiinua Mgongo (pensheni) yako ndo uanze kufanya biashara, au ununue Fuso au Canter ya kubeba mizigo; ndugu mwajiriwa utaizika pensheni yako mchana kweupeeee.
Baadhi ya waajiriwa (wafanyakazi) mlioanza kufanya biashara kuna hiki kitu mnakosea 👉 Biashara zenu/maduka yenu huwa yanajaa kwenye tarehe za mishahara, wahuni tunasema; mna-bosst mitaji kwenye tarehe za mishahara. Hii ni mbaya sana biashara yako kutegemea mshahara wako ili ujaze duka lako. Biashara inatakiwa kujiendesha yenyewe. Kama unaendesha biashara yako kwa nguvu ya mshahara jiulize ukistaafu au ukifukuzwa kazi utapata wapi hela ya kuboost?
~ TABIA YA KUDOKOA BIDHAA BILA KULIPA
Wafanyakazi wengi mna tabia ya kuchukua (kudokoa) bidhaa kwenye maduka yenu bila kulipa huku ukitegemea mshahara ukitoka utaboost mtaji. Usichukue bidhaa kwenye duka lako kwa matumizi yako bila kulipa au kujikopesha - "Huwezi kuweka chumvi nyingi kwenye mboga hata kama una hela nyingi za kununua magunia ya chumvi".
RIGHT MARKER,
Mbezi Louis, DSM,
Septemba 24.