Napata changamoto kwenye mfumo mpya wa kuomba leseni ya biashara

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Habari wakuu. Hapa nimepambana since asubuhi hadi sasa kijasho kinanitoka, kuna mfumo mpya umetambulishwa na Tamisemi kwa wale wanaohitaji lesseni za biashara unaingia hapa.

Tausi.tamisemi.go.tz.

Ila kila nikiingia wakinitaka niingize NIN namba (Namba nida) then next ni create password wanakataa na huu ndio ujumbe napokea.

Msaada kwa wanaojua hapo nafeli wapi.

mfumo wao umefeli tangu ijumaa usiku, nilijaribu kuwasilisha tatizo kwao wanalitambua hilo. hakuna unapokosea boss
 
kaka umewasiliana nao kupitia namba Gani....kama unazo nipasie Nina shida nao
mm sijapata tabu nimeprint Bill nikapata Control namba nikalipa Mpesa nika print license fasta tu ndo iyo
 
Maana hawa jamaa hawaeleweki kabisa
kaka kazi ya mfumo maana yake nikuwa mtanzania uutumie hakuna atakaye kuzingua kutumia mfumo ulioandaliwa kwaajili ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia, mambo yanachange sikuhizi unaweza pita usajili leseni nk bila kufika ofisini
 
Yani hata TRA kufanyiwa tax clearance haiitajiki tena, ukishaingia tu kwenye hiyo tovuti unajaza details, unalipia unapewa leseni?
 
Yani hata TRA kufanyiwa tax clearance haiitajiki tena, ukishaingia tu kwenye hiyo tovuti unajaza details, unalipia unapewa leseni?
kwa business names unapooanza tax clearance hahitajiki kupata leseni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…