Hana presure wala kisukari,ana umbile la kawaida kama kilo 80. Ni mwnwsheria haimchoshi sana,ana madeni anayolipa kwa shida,na mkate wake wa siku ana mudu ingawa haulingani na hadhi yake..Mkewe hushutumu sana kuwa ana mahawala,ingawa yeye anasema hana.cha ziada amewahi kufanya musterbation sana kabla hajaoa na pia akiwa chuoni miaka 15 ilopita.
Pole sana mkuu, Niliuliza ili wadau wenye solution waweze kushauri specifically.
Cha kwanza ambacho ningem(ku)shauri ni mazoezi, tendo zima kwa mwanaume linachagizwa sana na flow nzuri ya damu mwilini, So mazoezi husaidia sana katika hili. na mazoezi kujenga (endurance ya misuli/mwili) so kama tendo lilikua linamchukua dakika 2 inaweza kwenda nusu saa au zaidi bila yeye pia kuchoka kulingana na mazoezi anayofanya . (maana wasio na mazoezi hata ya kutembea hufika haraka sana, huchoka haraka na wengine huishia kupepesuka maana hawana stamina ya kutosha) mazoezi pia huondoa misongo ya mawazo mkuu.
Pili anapaswa kuushinda woga alio nao ndani yake juu ya tendo zima, kwa kuwa na fikra chanya kuwa anaweza sana na alenge kuchelewa kufika kileleni katika mawazo yake, pia imagination inahusika sana- kujenga picha ya tukio zima kichwani. (hii ni kama mbegu, ukipanda hata kwenye jiwe itaota, kwa hiyo akijitahidi itakuwa kama anavyodhamiria moyoni)
Tatu, ajitahidi kuconcentrate na tendo. na ikiwezekana awe anabadilisha mazingira ya tukio kadri itakavyowezekana.
Nne, masterbation huchangia sana uume kukosa nguvu na kwa kuwa mfanyaji mara nyingi hutumia nguvu kuliko inavyotakikana, so mazoezi hapa ni njia sahihi zaidi na kujenga hisia chanya juu ya uwezo wake.
Pia ajitahidi sana kula vyakula vyenye proteins kama nyama (michemsho ni mizuri zaidi kuliko rosti), samaki, karanga, maharage na jamii ya kunde, mayai n.k kulingana na wataalamu watavyoendelea kushauri.
unfortunately mimi ni mtaalamu wa biashara, so wataalamu wa sayansi ya mwili watashauri vizuri zaidi.