Napata maumivu kwenye viungo vya mwili nimeenda hospitali lakini sijapata nafuu

konklion

Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
6
Reaction score
1
Poleni na majukumu ndugu zangu kama mjuavyo maradhi tumeumbiwa binadamu mwenzenu nimekuja hapa leo nahitaji msaada wenu,yaan ni hivi kama wiki mbili nyuma nilianza kuskia maumivu kwenye mkono wangu wa kushoto eneo la bega kwa ndani,nikaenda hospitali ya wilaya jirani wakanipa vidonge.

Lakini havijasaidia chochote maumivi yanazidi tu.na kadri siku zinavoenda kuna uvimbe unatokea (usio na maumivi) maeneo ya nyonga kwa juu yan eneo la mkono unaouma kwa chini yani mwanzo wa mbavu upande wa mgongoni nimerudu hospitali wamenipima tena dawa ila sioni nafuu yoyote naombeni ushauri kwa anaejua hili litakua tatizo gani msaada jamini.
 
Huo uvimbe ndio kesi ...nenda hospitali ya rufaa ... ...siku hizi maradhi mengi ...
 
Mkuu tumia dawa inaitwa DICLOKANT (Chagua iliyotengenezwa India) , ni dawa ya kupakaa ipo kma dawa ya meno!
Iweke kidogo mwilini kisha jisugue maeneo ambayo kuna maumivu ya Mwili. Kwa maelezo zaidi nicheki inbox tuongee kwa simu
 
Gout kwani we mlaji wa mbuzi choma na nyama choma kwa sana NI VZR Ukafanya vipimo vikubwa
 
Hizo ni dalili za vidonda vya tumbo ndg, nenda hosp kubwa kapimwe vizur.
 
Mkuu tumia dawa inaitwa DICLOKANT (Chagua iliyotengenezwa India) , ni dawa ya kupakaa ipo kma dawa ya meno!
Iweke kidogo mwilini kisha jisugue maeneo ambayo kuna maumivu ya Mwili. Kwa maelezo zaidi nicheki inbox tuongee kwa simu
Asante ndgu nakuchek
 
Gout kwani we mlaji wa mbuzi choma na nyama choma kwa sana NI VZR Ukafanya vipimo vikubwa
Shukran mkuu.ila mi sio mpenz Wa nyama kbsa.na mbuz skumbuk mara ya mwisho nlikul mwak gan
 
Mkuu pima Na saratani mara nyingi hivo Huwa Ni viashiria japo simaanishi Ni saratani ila Fanya vipimo vya uhakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…