Napata wasiwasi, Arsenal anaweza akatwaa EPL kiutani utani

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Wakuu wa jukwaa heri ya mwaka mpya.

Mnauonaje mwendo wa Arsenal kwenye mbio za ubingwa pale EPL.

Arsenal kama utani, anakimbiza mwizi kimya kimya, ligi ilivyoanza tukasema hafiki krisimasi atakuwa kashatoka kileleni.

Krisimasi pamoja na mwaka mpya umefika, naona kasi yao inazidi. Tunaemtegemea Man City nae anaanza kudondosha alama. Sasa gap ni alama 7.

Naanza kupatwa na wasiwasi, Arsenal chini ya Arteta inaweza ikatwaa ubingwa msimu huu kwa udhaifi wa timu kubwa nyingine.

Wasiwasi wangu ni kelele zao. wanasumbua sana, tutaweka wapi sura zetu?
 
Tangu najitambua Mimi ni Arsenal damu, na nilisikitika msimu fulani Arsene Wenger alipolaumiwa na waingereza kwamba kwanini kachezesha first eleven bila uwepo wa muingereza hata mmoja. mbaya zaidi hata wale sub hakukuwa na muingereza, kitendo kilichowaudhi wenye nchi yao na kudai wamempa laana ya kutochukua kombe la ligi kuu.

Kweli tangu msimu ule My favorite team imekuwa ya kugombea big four tu. But kwa Sasa tuna kijana machachari kabisa, si mwingine
Ni Mikel Arteta huenda akatutoa kimasomaso kwenye huu msimu.

Japo mechi ya Leo na Wagumu
New Castle inanitia hofu kiasi.
 
Wakuu wa jukwaa heri ya mwaka mpya.

Mnauonaje mwendo wa Arsenal kwenye mbio za ubingwa pale EPL.

Arsenal kama utani, anakimbiza mwizi kimya kimya, ligi ilivyoanza tukasema hafiki krisimasi atakuwa kashatoka kileleni.

Krisimasi pamoja na mwaka mpya umefika, naona kasi yao inazidi. Tunaemtegemea Man City nae anaanza kudondosha alama. Sasa gap ni alama 7.

Naanza kupatwa na wasiwasi, Arsenal chini ya Arteta inaweza ikatwaa ubingwa msimu huu kwa udhaifi wa timu kubwa nyingine.

Wasiwasi wangu ni kelele zao. wanasumbua sana, tutaweka wapi sura zetu?
Wajitahidi wasije wakamruhusu Man city akakaa pale juu kwasababu itakuwa bye bye ukizingatia msimu huu wana halaand na nadhani Klopp na Liverpool yake ni mashahidi.
 
Leo ni leo kwa Arsenal,akishinda basi tusubirieni sie Man u tuwapigie tena kwa mara ya pili
 
Naanza kupatwa na wasiwasi, Arsenal chini ya Arteta inaweza ikatwaa ubingwa msimu huu kwa udhaifi wa timu kubwa nyingine.
Hata usipokuwa na wasiwasi arsenal wana timu nzuri na wanaweza wakatwaa ubingwa, wasiwasi wako wewe sio kigezo cha arsenal kutokuchukua ubingwa, na unaposema arsenal inaweza kuchukua ubingwa kwa udhaifu wa timu nyingine kumbuka hata hao wengine waliokuwa wanachukua ubingwa sababu ni hiyo hiyo udhaifu wa timu nyingine, usiishi kwa kukariri zama zimebadilika sasa.
 
Naanza kupatwa na wasiwasi, Arsenal chini ya Arteta inaweza ikatwaa ubingwa msimu huu kwa udhaifi wa timu kubwa nyingine.

Wasiwasi wangu ni kelele zao. wanasumbua sana, tutaweka wapi sura zetu?
Mkuu arsenal abebe ubingwa kwasababu ya udhaifu wa timu nyingine? Huo ni utani. Arsenal atabeba ubingwa kwasababu ndio timu bora zaidi msimu huu.

Sura zenu pelekeni saluni mkafanyiwe scrub.😂😂
 
Daah ndo mshaanza kutusema🤣🤣
 
Hata usipokuwa na wasiwasi arsenal wana timu nzuri na wanaweza wakatwaa ubingwa, wasiwasi wako wewe sio kigezo cha arsenal kutokuchukua ubingwa, na unaposema arsenal inaweza kuchukua ubingwa kwa udhaifu wa timu nyingine kumbuka hata hao wengine waliokuwa wanachukua ubingwa sababu ni hiyo hiyo udhaifu wa timu nyingine, usiishi kwa kukariri zama zimebadilika sasa.
Kunywa maji usiwe sana siriaz...sisi mashabiki wa Man U tutaeka wapi sura zetu
 
Naogopa
FB_IMG_1674146562540.jpg
 
Back
Top Bottom