Napataje malighafi ya mchikichi, nataka kuanza kukamua Mafuta

Napataje malighafi ya mchikichi, nataka kuanza kukamua Mafuta

WatesiWETU

Senior Member
Joined
Jan 2, 2022
Posts
106
Reaction score
248
Habarini Guys.

Nimepata idea ya Kukamua Mafuta ya Mawese au ya Mchikichi ila sasa malighafi ya uhakika na bei rafiki ndio najaribu kuwaza.. inapatikana wapi kwa wingi??

Kama una uzoefu wa Ukamuaji wa Mawese na Mchikichi naomba unisaidie kujua yafuatayo:

1. Mkoa wenye uhakika wa Mchikichi na Mawese!
2. Gharama za mashine ya Kukamulia yakuanzia siyo zile kubwa sana
3. Changamoto za kuyafanyia refine na hatuazake..

Asanteni

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Uko mkoa gani? Mikoa ambayo mawese inapatikana kwa wingi ni pamoja na Kigoma na Mbeya.

Kama waweza ungetembelea uone uzalishaji na kujua mawili matatu kuhusu hiyo BIASHARA. Au tembelea Sido iliyo karibu yako uombe kupewa taarifa.

ASANTE.
 
Uko mkoa gani?.
Mikoa ambayo mawese inapatikana kwa wingi ni pamoja na Kigoma na Mbeya.

Kama waweza ungetembelea uone uzalishaji na kujua mawili matatu kuhusu hiyo BIASHARA.
Au tembelea Sido iliyo karibu yako uombe kupewa taarifa.
ASANTE.
Mawese yanatoa mafuta ya aina mbili, hajaweka wazi anataka akamue mafuta yanayotokana na gamba la nje la mbegu (mekundu) au yanayotokana (kama ya nazi) na mbegu ya ndani...
 
Mawese yanatoa mafuta ya aina mbili,haja weka wazi anataka akamue mafuta yanayotokana na gamba la nje la mbegu (mekundu) au yanayotokana (kama ya nazi) na mbegu ya ndani...
Nataka ya kupikia.. tena nimekosea nilitaka kumaaisha Mchikichi siyo mawese..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nataka ya kupikia.. tena nimekosea nilitaka kamaaisha Mchikichi siyo mawese..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu, michikichi ina mafuta ya aina mbili na yote hutumika kwa kupikia na wenyeji. Mafuta yanayokamuliwa kutoka kwenye mbegu ya ndani yapo kama ya nazi na yana bei kubwa sana.

Mafuta mekundu mtaji wa mashine yake ni nafuu sana tofauti na yale yatokanayo na kubanguliwa mbegu zake.
Karibu Kyela, karibu sana Mwaya.
 
Kwa Dar njoo Mvuti. Huko utakutana na na legend wanaofanya hiyo kazi. Wanakamua kwa kiasi kikubwa tu. Pwani nenda Ruvu JKT zamani tulikuwa tukilima na kukamua, sasa sijui kukoje.

Nitakupa namba za wanaofanya hiyo kazi huku Mvuti nikionana nao
 
Njoo Kigoma kuna malighafi ya kutosha japo kwa sasa mawese yapo juu sana. Faida utakayopata ni kubwa sana endapo utaipata hiyo malighafi (magazi ). Kwa hapa nilipo changamoto ni ukosefu wa mashine za kukamulia.

Watu wanakamua locally kwa kutumia mitambo duni ya kuzunguka kwa kutumia mikono yaani ni nguvu mwanzo mwisho but ukiwekeza kisasa zaid utapiga hela sana kwani watu bado wako usingizini kuhusu hii fursa adimu. Mimi pia naitamani sana ila changamoto ni capital. Kwa sasa dumu la Lita 20 ni kati ya elfu 65 hadi elfu 70.

Kwetu pia tunayo hiyo malighafi japo siyo sana lakini kuna watu wanayo ya kutosha. Pia kuna njia nyingine inatumika kuipata, mtu anakukabidhi shamba wewe unampa kiasi kadhaa cha pesa mnakubaliana utakaa kwa muda gani kama ni mwaka au miezi sita unakuwa unavuna kama kwako then muda ukiisha unampisha.

Mise pia ni bonge la dili kwani mafuta yake yanatafutwa sana especially SIDO Kigoma kwa ajili ya kutengezea sabuni. Hivyo ukikamua mawese then unaita MTU mwenye mashine ya kumenya mise then unabeba kupeleka SIDO kuuza kwa bei nzuri tu.
 
Kwa Dar njoo Mvuti.
Huko utakutana na na legend wanaofanya hiyo kazi.
Wanakamua kwa kiasi kikubwa tu.
Pwani nenda Ruvu JKT zamani tulikuwa tukilima na kukamua, sasa sijui kukoje.
Nitakupa namba za wanaofanya hiyo kazi huku Mvuti nikionana nao
Wanatoa wapi hàyo matunda
 
Mawese yanatoa mafuta ya aina mbili,haja weka wazi anataka akamue mafuta yanayotokana na gamba la nje la mbegu (mekundu) au yanayotokana (kama ya nazi) na mbegu ya ndani...
Alitembelea maeneo ya uzalishaji atapata elimu kubwa Sana na halisi na ya vitendo, lakini pia anaweza rahisisha kwa kutembelea ofisi za SIDO mahali alipo atapata details nyingi Sana mpaka upatikanaji wa machines.
 
Mkuu,michikichi ina mafuta ya aina mbili na yote hutumika kwa kupikia na wenyeji. Mafuta yanayo kamuliwa kutoka kwenye mbegu ya ndani yapo kama ya nazi na yana bei kubwa sana.
Mafuta mekundu mtaji wa mashine yake ni nafuu sana tofauti na yale yatokanayo na kubanguliwa mbegu zake.
Karibu Kyela,karibu sana Mwaya.
Mekundu ndio yanayoitwa mafuta ya mise?
Hutumika kutengeneza sabuni?
 
Wanatoa wapi hàyo matunda
Wewe nenda Mvuti kisha uliza wanakotengeneza Mawese, wao watakupa full info. Unaweza kuwatumia wao kama nguvu kazi. Mimi sinufaiki na chochote katika hilo, so msaada wangu utaishia hapo.

Kuna jamaa ana mashine yake ya kukamulia Mawese. Wengine wanakamua locally.
 
Wewe nenda Mvuti kisha uliza wanakotengeneza Mawese, wao watakupa full info.
Unaweza kuwatumia wao kama nguvu kazi.
Mimi sinufaiki na chochote katika hilo, so msaada wangu utaishia hapo.
Kuna jamaa ana mashine yake ya kukamulia Mawese. Wengine wanakamua locally.
Ila Mvuti kubwa mkuu
 
Alitembelea maeneo ya uzalishaji atapata elimu kubwa Sana na halisi na ya vitendo, lakini pia anaweza rahisisha kwa kutembelea ofisi za SIDO mahali alipo atapata details nyingi Sana mpaka upatikanaji wa machines.
Be blessed bro.. kwa ushauri

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe nenda Mvuti kisha uliza wanakotengeneza Mawese, wao watakupa full info.
Unaweza kuwatumia wao kama nguvu kazi.
Mimi sinufaiki na chochote katika hilo, so msaada wangu utaishia hapo.
Kuna jamaa ana mashine yake ya kukamulia Mawese. Wengine wanakamua locally.
Asante ndugu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Njoo kigoma kuna malighafi ya kutosha japo kwa sasa mawese yapo juu sana.Faida utakayopata ni kubwa sana endapo utaipata hiyo malighafi (magazi ) .kwa hapa nilipo changamoto ni ukosefu wa mashine za kukamulia.watu wanakamua locally kwa kutumia mitambo duni ya kuzunguka kwa kutumia mikono yaani ni nguvu mwanzo mwisho but ukiwekeza kisasa zaid utapiga hela sana kwani watu bado wako usingizini kuhusu hii fursa adimu.mi pia naitamani sana ila changamoto ni capital. Kwa sasa dumu la Lita 20 ni kati ya elfu 65 hadi elfu 70.kwetu pia tunayo hiyo malighafi japo siyo sana lakini kuna watu wanayo ya kutosha. Pia kuna njia nyingine inatumika kuipata, mtu anakukabidhi shamba we we unampa kiasi kadhaa cha pesa mnakubaliana utakaa kwa muda gani kama no mwaka au miezi sita unakuwa unavuna kama kwako then muda ukiisha unampisha. Mise pia ni bonge la dili kwani mafuta yake yanatafutwa sana especially SIDO kigoma kwa ajili ya kutengezea sabuni. Hivo ukikamua mawese then unaita MTU mwenye mashine ya kumenya mise then unabeba kupeleka SIDO kuuza kwa bei nzuri tu.
Asante sana kaka.. mchango wako umenipa mwanga.. ngoja nijiaandae kutembelea Kigoma..

Vip lakini, Bei ya mashine zake za kisasa ni bei gani??

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sorry nimeshindwa Ku quote. Bei za machine za kisasa sijui kwakweli labda SIDO wanaweza kuwa na details zaidi. Huku niliko ni kijijini na hakuna mwenye hiyo mashine ya kisasa hivyo ni fursa nyingine hiyo kwani watu watakuwa wanakuja kukamua kwako na kukupa pesa au mawese.

Pia kama utakuwa na mtaji na soko lako zuri la mawese watakuwa wanakuuzia hapohapo baada ya kukamua kwani wengi hawasafirishi bali kuna wanunuzi wanapita kila asubuhi kwenye eneo ambapo processing inafanyika kwa ajili ya kutoa order ya kukusanya product.

Pia wanakuuzia mise ambayo utaimenya(machine zipo au utanunua yako) then utapeleka SIDO kusaga,utapata mafuta ambayo wanatengeneza sabuni pia na mashudu ambavyo utauza kwa pesa nzuri tu hapo hapo SIDO. Pia itakuwea rahisi kupata connection zaid juu ya upatikanaji wa hizo raw materials na Wateja zaidi kwani watakuwa wanakufuata popote ulipo wakihitaji either kukamua,kuuza au kununua ngazi,mise au mawese.

Ngazi (amagazi kwa kiha)
Ni Yale matunda ambayo yakiiva yanakuwa na rangi ya njano au nyekundu.Haya yakikamuliwa hutoa mafuta ya mawese ambayo ni mazuri na Matamu sana kwa kula

Mise
Ni lile ganda linalobaki baada ya lile ganda la ngazi kukamuliwa. Hili linakuwa kama mfano wa Nazi tofauti ni size tu kwani mise ni midogo kwa size.Hii pia humenywa kwa mashine ambayo hutumia muda mfupi zaidi na kwa debe moja bei yake ni tshs 300/ au kwa kutumia mawe locally na hutumia muda mwingi sana ambapo baada ya kumenya kwa ndani kunakuwa na mse kama Nazi vile ila ni kadogo kwa size .Baada ya kukusanya kiasi cha kutosha cha mise utachagua either uuze mise au upeleke SIDO kusaga na kupata mafuta ambayo ndiyo hayo wanatengeneza sabuni maarufu kama sabuni za Kigoma (gwanji) ambayo ina povu nyingi sana na hutakatisha nguo vizuri sana but si nzuri kwa kuogea japo watu wanatumia. Pia baada ya kukamua tunapata Mashudu ambayo ni chakula kizuri sana cha mifugo kama kuku na nguruwe.

Kwa kifupi hii ni bonge moja la fursa kama utaamua kuifanya seriously na ukiwa na capital nzuri kwani soko lake ni zaidi ya uhakika.

Asante na kila la kheri kama utaamua kuwekeza mwenye eneo hili.
 
Njoo kigoma kuna malighafi ya kutosha japo kwa sasa mawese yapo juu sana.Faida utakayopata ni kubwa sana endapo utaipata hiyo malighafi (magazi ) .kwa hapa nilipo changamoto ni ukosefu wa mashine za kukamulia.watu wanakamua locally kwa kutumia mitambo duni ya kuzunguka kwa kutumia mikono yaani ni nguvu mwanzo mwisho but ukiwekeza kisasa zaid utapiga hela sana kwani watu bado wako usingizini kuhusu hii fursa adimu.mi pia naitamani sana ila changamoto ni capital. Kwa sasa dumu la Lita 20 ni kati ya elfu 65 hadi elfu 70.kwetu pia tunayo hiyo malighafi japo siyo sana lakini kuna watu wanayo ya kutosha. Pia kuna njia nyingine inatumika kuipata, mtu anakukabidhi shamba we we unampa kiasi kadhaa cha pesa mnakubaliana utakaa kwa muda gani kama no mwaka au miezi sita unakuwa unavuna kama kwako then muda ukiisha unampisha. Mise pia ni bonge la dili kwani mafuta yake yanatafutwa sana especially SIDO kigoma kwa ajili ya kutengezea sabuni. Hivo ukikamua mawese then unaita MTU mwenye mashine ya kumenya mise then unabeba kupeleka SIDO kuuza kwa bei nzuri tu.
Kaka naomba tuongee Kwa mapana ,namba yangu ni 0652260743
 
Back
Top Bottom