Nape aongoza mazishi ya Sharomillionea

Mbona sijamuona huyo Nepi wala kijani anayoisema muanzisha uzi au katumwa na magamba halafu CDM wakienda huwa hawajioneshi kama hao magamba.

HATARI!
Weka mbali na tembo
 

Wednesday, November 28, 2012




Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nauye, akitupa mchanga kaburini, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga

Waombolezaji wakimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu msibani, wakati wa mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu Tanzania, yaliyofanyika leo, kijijini kwa marehemu, Lusanga, Muheza mkoani Tanga

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu Tanzania, Hussein Ramadhani, maarufu Saharo Milionea, likiwasili nyumbani kwao, Lusanga, Muheza mkoani Tanga, wakati wa mazishi leo.

Mzee Kingi Majuto akitupa mchanga kaburini kumzika Sharo Milionea
Kwa picha zaidi bofya read more

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Rais wa Bongo Movies Simon Mwakifyamba na Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga

Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo

Baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva na filam Tanzania, wakiwa kwenye mazishi ya Sharo milionea

Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama Anna Mkapa, kwenye msiba huo. Pamoja naye ni Nape

Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando akiwa na baadhi ya wasanii kwenye mazishi hayo

Vijana wakiwa wamepanda mnazi kuona mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga

(Picha na Bashirb Nkoromo).​



Wednesday, November 28, 2012






Mama yake mzazi Sharo Millionea akiwa ameshikwa baada ya kuishiwa nguvu baada ya kutoka mochwari kuchukua mwili wa mwanae.
(kwa picha zaidi bofya read more)


Twende huku mzee...! Msanii wa vichekesho ambaye ni mshirika wa karibu wa marehemu Sharomilionea, King Majuto (kushoto) akiongozwa na muigizaji JB wakati wa shughuli za mazishi ya Sharomilionea leo mchana kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

Jeneza la marehemu Sharomilionea kabla ya kupelekwa makaburini na mwili wa marehemu kuzikwa kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.

Waombolezaji wakiwa katika ibada ya sala ya jeneza la marehemu Sharomilionea katika kijiji chao cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.

Mwili wa marehemu Sharomilionea ukiswaliwa kabla ya kuzikwa leo mchana (Novemba 28, 2012) kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

Baadhi ya waombol;ezaji waliojitokeza kumzika Sharo Milionea kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya Sharomilionea leo Novemba 28, 2012

Mama mzazi wa marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Shari Milionea' (wa tatu kushoto) akilia kwa uchungu nyumbani kwake Lusanga, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga. Pembeni ni ndugu na jamaa wa marehemu.







Picha: Kwa Hisani ya Jiachie.blogspot.com na GPL


















 
It is possible that this incidence has halted alot NAPE and it looks like he is confused upto thinking where was ccm before his death. Poleni ccm lakini MMEPITILIZA KUOMBOLEZA !!
 
Thanks to all who have made it possible kumlaza kwenye nyumba yake ya milele hadi ataporudi Mungu
 
R.I.P... Barabara zetu hizi ZITATUMALIZA... Tunahitaji Inter-REGION POLICE PATROL... Sio wawe ka MIGUU wawe kwenye MAGARI ya POLISI
 
rip sharo "oooh maaama" milionea

nape na ccm yao wanakurupukia mambo bila hata kujiuliza...mbona marehemu alikuwa "m4c"...

ushauri rahisi kwa nape na wenzake type zake huko ccm ..wasikilize wimbo wa mrisho mpoto ...chocheeni kuni mbichi ugali usongwe"...mmekuja msibani na kuwapa wafiwa zawadi ya sabuni za unga aliyewaambia nguo zetu chafu nani?
 
picha ya pili na nne mwisho ni utovu wanidhamu

kwako ni utovu wa nidhamu ila kwao "wanauza nyago"...na makamera ya video msibaniiii...ni majaliwa yake molaaa ohhh kuuona mwaka....full mbwembwe na mapozi msibani.
 

Na ALIKUWA ametoka kwenye MAZISHI ya MSANII JOHN MAGANGA...
Naona anavutia VIJANA
 
CCM kwa kupenda kudandia kila kitu. Mtu amekufa kutokana na usimamizi mbaya wa barabara wanajitiatia kuwahi mazishi. Machozi ya mamba. Anyways, wasanii wanawazika wasanii wenzao. CCM wanachafua maadili kwa kufanya madili wakati wasanii nao wakichafua maadili yetu kimila. Tangulia Sharobaro.
 
kama huwezi kuzisoma hizo picha na kuona matatizo yaliyomo basii sina la zaida la kukusaidia

NDIO MAANA TUNA JAMII FORUMS... Kama MTU HAELEWI HOJA anauliza SWALI sio KUACHWA kwenye DIM LIGHTS as USUAL kwahiyo tusinge WEKA HIZO PICHA????

BE REAL MAN... SHARING is WHAT we NEED not HOLDING DOWN your EMOTIONS!!!
 
k
k
Stive nyerere kwa kujipendekeza.Njaa mbaya.
 
NDIO MAANA TUNA JAMII FORUMS... Kama MTU HAELEWI HOJA anauliza SWALI sio KUACHWA kwenye DIM LIGHTS as USUAL kwahiyo tusinge WEKA HIZO PICHA????

BE REAL MAN... SHARING is WHAT we NEED not HOLDING DOWN your EMOTIONS!!!



okey siku zote mwalimu hodari humuuliza mwanafunzi kaelewa nini kabla ya kumfundisha kwa usahihi, karibu uniambie umeelewa nini kwa mtizamo wako ?
 
okey siku zote mwalimu hodari humuuliza mwanafunzi kaelewa nini kabla ya kumfundisha kwa usahihi, karibu uniambie umeelewa nini kwa mtizamo wako ?

Maombolezo ya Msanii Mashuhuri
 
Hiyo rangi ya kijani kulikoni ! wako wanafanya mazishi au wanafanya campaign kupitia kifo cha mtu maarufu ! NI KUMKOSEA MUNGU ADABU KUCHANGANYA MAZISHI NA MATAKWA YA KIDUNIA!! GOD ONLY VALUE YOUR SOUL AND NOT YOU ARE WORLDLY ACHIEVEMENTS!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…