Nape aongoza mazishi ya Sharomillionea

jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.....wahenga hawakukosea
 

Mkuu kwa haraka haraka unaweza ukadhani hivyo, lakini katika Uislam rangi ya kijani hutumika sana. angalia bendera ya Saudia Arabia, libya , uae, oman na nchi zengine za kiislam utakuta rangi ya kijani ndio imetumika kwa njia moja au nyengine. Hata nembo ya OIC rangi ya kijani pia ilitumika

sasa whether ile iliwekwa na CCM au ni bahati tu hapo siwezi kujua. lakini vitambaa vingi vya misikitini huwa ni rangi kijani.
 
Basi sawa kama ni hivo,sikuelewa nilidhani ndo rangi ya CCM
 
Jamani wapi watu wanakwenda kucheka tuuuuuuuu! I knw sm countries in europe huko, kuna sehemu watu huwa wanakwenda kucheka tu, kama kuna hiyo sehemu hapa kwetu naomba muongozo tafadhali! Nataka nichekeeeeeeeee, hii nchi ni zaidi ya mr.bean! Lol
 
Sina uhakika sana kama hiyo ni bendera ya ccm maana misiba mingi niliyohudhuria mara nyingi naona jeneza limefunikwa kitambaa cha kijani.
 

Usilete mambo yasiyokuwa na msingi, Jeneza halikuwa na viashiria vyovyote vya CCM hivyo vitambaa vilivyokuwa vimefunikwa ni vitambaa tu ambavyo vina rangi ya kijani lakini havina maana na CCM

jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.....wahenga hawakukosea


Hata mimi binafsi ndivyo ninavyoelewa kuwa Uislamu katika kufunika majeneza wanatumia Kitambaa cha Rangi ya Kijani, yaani ni sawa mfano kwa Wakatoliki kutumia kitambaa cha rangi ya njano na nyeupe haina maana kuwa wanashabikia Timu ya yanga, bali ni rangi za Bendera ya VATICAN CITY.

Lakini pia na mimi katika hili labda nitamshangaa huyu muheshimiwa mmoja anyeonekana amevaa Jezi full za CCM, sijui anatafuta umaarufu wa kujulikana kwa NAPE ili ampe ulaji.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwa kifupi hapa.JF huwa.tunasema mtoa.mada amekurupuka...
 

kwa hisani ya AnnaPeter
 
Ukiwa msanii ni kiyoo cha jamii, Ukiwa mwanasiasa unatafuta uongozi kwa jamii. Hivyo Mwanasiasa akiwatumia wasanii vizuri ana uwezekano mkubwa wa kufanikisha alitakalo. alimradi asiwe na mafyongofyongo na mafindofindo. Lakini katika mazishi ile si bendera ya CCM ni kitambaa chenye rangi ya kijani na juu yake maandishi ya njano yaliyonukuliwa kutoka katika QOURAN tukufu, hutumika kufunikia jeneza
 
Kama wasanii wanatumika katika Kampeni za siasa,kwa nini wasiheshimiwe wanapokufa.? Sanaa ni sehemu ya social life. Kuna Wizara inayohusika na sanaa.
Halafu,hata kama unataka kuandika makala weekend,nani ataisoma kama watu wote wamekwenda kubugi man?
 
Don't take anything by chance; CCM hawachelewi kuchemsha na wala mtoa mada hajakurupuka hata kidogo

Narudia tena amekurupuka... Hudhuria mazishi ya kiislam.alafu angalia jeneza.linafunikwa na kitambaa cha rangi.gani...
 
Ila nasisi wabongo tumezidi uchama...kwenye mazishi si tumezoea kuvaa black and white jamani! tuseme hao waliovaa manguo yao ya vyama vyao hawakuwa na mashati meusi kweli!??
Tanzania na watanzania hapa ndipo tunapokosea...yaaani ni uchama kila mahali! inaudhi sana....
 
tuonyeshe uhalisia wetu kwenye huzuni tuwe na huzuni tuvae nguo za huzuni ,kwenye chama tuvae kichama sio kila mahali ni chama kwanza hata misibani ,kwenye ibada ,harusi n.k tuwe makini kwa hili tuache mzaha .
 
sasa hapo ukweli ni nini basi? mbona yanayokanushwa ndio yanayoonekana?
 
1) ina maana sharobaro alikuwa ni mmoja wa viongozi wa ccm?
2) kama sio uvccm na sare zao wakati wa kushusha mwili wa marehemu walitumwa na nani?
3)kulikuwa na ulazima gani kuzikwa kwa itifaki ya ccm?

4)kwa nn asingezikwa kwa heshima za kawaida ambazo wanapewa wananchi wengine hata kama ni watu mashuhuri?

5)hivi wasanii wote wa Tanzania ni wafuasi wa CCM au?

Nasitisha kutoa rambirambi zangu mpaka pale nitakapojibiwa hoja zangu kwa umakini mkubwa,

NAOMBA MOD UNILINDE nawasilisha,U
 
Ukiona hivyo ujue kuwa ccm ni taifa kubwa,au maana yake ni ipi nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…