Nape ataka "faili" la Rose Muhando

Nape ataka "faili" la Rose Muhando

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Nape.jpg


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametaka kupewa maelezo maalum ya kimaandishi juu ya mwenendo wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando ili aweze kuchunguza madai ya utapeli yanayosemwa juu yake.

Nape alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa endapo atafanyia kazi tuhuma zilizotolewa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka la kila mwaka, Msama Promotions, waliodai mwimbaji huyo hakutokea jukwaani, licha ya kupewa malipo yake na stahiki zingine zilizostahili.

rose_muhando.jpg


“Kwanza ieleweke kuwa mimi sikuambiwa, ila nilisikia wakiwatangazia watu waliokuwepo uwanjani juu ya kutokuwepo kwa Rose kwenye tamasha hilo. Sasa mimi siwezi kufanya kazi kwa maneno ya mtaani, kama kuna wasanii wanatapeli, niletewe maelezo kimaandishi yakiwa na ushahidi wa tuhuma zao, hapo ndipo nitaweza kujua hatua za kuchukua,” alisema.

Awali, ofisa mmoja wa Msama Promotions aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji, alisema Rose alikuwa amepewa malipo yote, ikiwa ni pamoja na usafiri wa gari la kumtoa Dodoma hadi Mwanza, lakini hakuweza kutokea katika onesho hilo.

“Tulishamalizana na Rose na kila mmoja alijua atakuwepo, lakini tunashangaa mara ya mwisho hapatikani kwenye simu na hatujui kapatwa na masaibu gani,” alisema ofisa huyo.

Source: Naniliu
 
Maskini huyu mama sijui anayo yapitia, alikuwa anaeleweka ila sijui dhoruba gani imemkumba. Mungu amsaidie aione njia tena
 
Nadhani kabla kusaidiwa hao Maprotmoter naomba waziri aanze kuwasaidia hawa wasanii juu ya haki na kazi zao.
 
Huyo Msami nae kama boya tu kila mwaka hua analalamika kuhusu Rose Muhando lakni likija tamasha jipya anampa tena tenda si upuuzi huo sasa
 
Msama kesi zako na Rose zinachosha sasa mara ngapi unalalamika baada ya muda unamualika tena akatumbuize weiiii
 
Mpaka waziri tena!!! Ina mana wamemshindwa au!?!? Kama hataki wao wana mlazimisha yanini!?
 
kwa hiyo waziri ndio polisi/mahakama?? Msama vipi tena?
Hapa nina mashaka mbona hii ni police case ya kawaida kabisa isiyomhusu waziri? Wale wawili ni wafabiashara kupitia mgongo wa dini wamedhulumiana....Nape aangalie mipaka ya kazi yake na ukomo pia ili kuepuka mgongano wa kiutendaji
 
Back
Top Bottom