Nape: CCM bado ina imani na tume ya katiba nchini

ACHEBE

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
348
Reaction score
76
CCM BADO INA IMANI KUBWA NA TUME YA KATIBA

Nape Nnauye
NA MWANDISHI WETU
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimesema bado kina imani na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya.

Imesema licha ya CCM kutofautiana kimawazo katika baadhi ya maeneo katika rasimu ya kwanza ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini haina ugomvi na tume hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

"Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii, na kwa kweli tunamatumaini nao sana kuwa watatimiza wajibu wao kwa weledi mkubwa", alisema Nape.

Nape alibainisha kwamba pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza ya katiba , CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe inapendekeza serikali mbili.

"Kama mnavyoona katika hili, wakati tume inapendekeza muundo wa serikali tatu sisi CCM tunapendekeza muundo wa serikali mbili, lakini hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye mawazo tofauti na yetu", alisema Nape na kuongeza;

"Kumekuwepo na ripoti na makala kadhaa zinazojaribu kuonyesha kama vile kuna mvutano kati ya tume na CCM, au CCM na wengine wenye mawazo tofauti na CCM. Ukweli ni kuwa hali hiyo inayojaribu kujengwa kwa nguvu si ya kweli. Tuache hoja zishindane kwa hoja na nguvu ya hoja ndio iwe msingi wa ushindani".

Nape alitaka ushindani uwe kwenye hoja bila kushutumiana ili jatimaye mawazo ya wengi yasikilizwe na kuzingatiwa.

Alisema, CCM inasisitiza kuwa itaheshimu mawazo ya Watanzania, kwani katiba inayotengenezwa ni ya watanzania wote bila ya kujali itikadi zao.

"Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaounga mkono baadhi ya hoja za CCM hasa hoja ya serikali mbili. Tumeshuhudia maoni ya wajumbe wengi wa mabaraza na wananchi kwa ujumla wakiunga mkono mawazo haya ya CCM ya muundo wa muungano wa serikali mbili na hoja kadhaa zingine", alisema Nape na kuongeza;
 
Jaji Warioba kiboko yao(muhogo nchungu) kwa ccm they know

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
CCM BADO INA IMANI KUBWA NA TUME YA KATIBA

Nape Nnauye.

"Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii,
Nape alibainisha kwamba pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza ya katiba , CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe inapendekeza serikali mbili.

"Kama mnavyoona katika hili, wakati tume inapendekeza muundo wa serikali tatu sisi CCM tunapendekeza muundo wa serikali mbili, lakini hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye mawazo tofauti na yetu", alisema Nape na kuongeza;

"Kumekuwepo na ripoti na makala kadhaa zinazojaribu kuonyesha kama vile kuna mvutano kati ya tume na CCM, au CCM na wengine wenye mawazo tofauti na CCM.Tuache hoja zishindane kwa hoja na nguvu ya hoja ndio iwe msingi wa ushindani". Nape alitaka ushindani uwe kwenye hoja bila kushutumiana ili jatimaye mawazo ya wengi yasikilizwe na kuzingatiwa.

Alisema, CCM inasisitiza kuwa itaheshimu mawazo ya Watanzania, kwani katiba inayotengenezwa ni ya watanzania wote bila ya kujali itikadi zao.

"Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaounga mkono baadhi ya hoja za CCM hasa hoja ya serikali mbili. Tumeshuhudia maoni ya wajumbe wengi wa mabaraza na wananchi kwa ujumla wakiunga mkono mawazo haya ya CCM ya muundo wa muungano wa serikali mbili na hoja kadhaa zingine", alisema Nape
Ngongo Jasusi JokaKuu Mchambuzi platozoom
 
Last edited by a moderator:
Nani kamwambia kwamba Wananchi tunaunga mkono mfumo wa serikali mbili? Wanaounga mkono ni wale wanaokwenda kutoa mawazo huku wakiwa wamebebeshwa waraka wa ccm ambapo mara zote wamekuwa wakitolewa nishai na wajumbe wa tume na kuitwa vibaraka.
 
Waache kutapatapa. Mbona wanajishuku. Wamwache mzee afanye kazi maana serikali ya CCM ndio ilitaka fasta fasta katika suala hii lakini mzee kajitahidi kuja na vitu hadimu kidogo. Hapo ni fasta fasta je angepewa mda wa kutosha. TUngepata katiba ya kwenda nayo miaka 100
 
Semeni tu kuwa mmegundua kuwa hamna jeuri ya kumkataa
 
Hii haifuti Kauli yake kuwa wazee wasubiri kufa tu
 
- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?

- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!

Le Mutuz
 
hatimaye mtasema mnaunga mkono kila hoja, hilo la serikali mbili ni la viongozi wa ccm pekee na wala sio la wananchi
 
- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?

- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!

Le Mutuz
Senility is a deadly disease
 
CCM wana matatizo gani...?Mbona wanafanya tuwachukulia kama vichaa...watu wasio kuwa na akili timamu....kwa sababu wana fanya hili swala la katiba kama la chama......hili ni swala la nchi....hii sio km siasa zao za kipumbavu za ugaidi na ukabila....hili ni swala linaloangalia mustakabali wa nchi.....waache ushamba wa kijinga
 
- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?

- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!

Le Mutuz

Baba yako Mzee Malecela si ndiye muasisi wa serikali tatu mpaka Mwl Nyerere akamfukuza uwaziri mkuu?
 
- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?

- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!

Le Mutuz
Kumbe na wewe ovyo, sikujua!!!!!!
 
Nakishangaa hiki chama cha MAGAMBA! Kila anaye pewa uongozi hajui hata anatakiwa azungumze nini kwenye hadhira yake. Sasa huyu nae sijui ni nani kamwambia kuna KAMATI YA KATIBA!!???? Hivi kama kiongozi wa JUmuiya hajui kutofautisha kati ya KAMATI na TUME unatarajia ataleta tija ya aina gani kwa anao waongoza kama si maruwe ruwe matupu!!!??

Hivi ni kwa nini kila anaye oewa uongozi anageuka kuwa msemaji wa MAGAMBA? Nape anasema wana imani na TUME, huyu KJ naye anatoka na lake. Na tatizo kubwa hata haui kwamba RASIMU ni ya Tanzania, yeye anazungumzia maslahi ya MAGAMBA.

Utumbo mwingine haufai hata kuliwa, ati?
 
- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?
- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!Le Mutuz
Nawashauri tena Le Mutuz na Nape kwani CCM mkanyamaza kuna ubaya gani maana hii si Rasimu ya Vyama vya Siasa
  • (Wanachama wa CCM hawazidi 2,500 na sio hai wote lakini waliojiandikisha na kuchukua Kadi hata waliopitia Makazini na JKT watafika 6,000 muulizeni Chiligati)
  • Siku itakapofika Kura za maoni za Watanzania wote ndipo watu watakapoadhirika kwani haya Mabaraza yanadanganya na hayatapiga Kura, kwa hiyo Sinde Warioba mpaka sasa maoni anayoyakusanya ni ya Serikali 3, Bunge, Mahakama, Usalama wa Taifa nk.
  • Zanzibar wameshashtaki Mahakamani kuwa hawataki hizi habari za Muungano, iwe ya Serikali 1 au 2 au 3 wanataka Zanzibar yao sasa kura zikipigwa hata Tanganyika yote watoe 46,000,000 na Zanzibar wakatae hata kwa 700,000 Warioba ataangalia Majority ya Kura za visiwani kuwa HAWATAKI SERIKALI HIZO ((iwe 2 km CCM inavyotaka) Mnajua kura za Maruhani.
Soma vizuri hiyo rasimu ni ya Serikali 3 kwani ina wabunge wasiozidi 40 watakaotoka kila Mkoa 2 (mwanamke na mwanamume) jua bado kuna rasimu ya hizo Serikali ya Tanganyika na Zanzibar hazijaandaliwa.
Hebu wakuu mnyamaze aibu ya kunzisha Vyama vingi 1992 wakati wa Prestroroika ya Gobachev Baba wa Taifa alisema Watanzania 90% wamekataa vyama vingi lakini twendeni tu kwenye mfumo huo.
Likaja la EAC zikapita Tume kutushauri msiwaingize Rwanda na Burundi bado mkang'ang'ania tuungane SASA TUNAKIONA HAITACHUKUA MWAKA TUTASAMBARATIKA.
Hivyo basi ni heri ipotee CCM kuliko TANGANYIKA (maana kwa Zanzibar ndio basi tena mmemuona Abeid Karume kapasua jipu KIZOTA)
Mke akiikataa Ndoa usimlazimishe atajakuabisha mbele ya watu wa Mataifa na Sura mtaificha wapi?
 
W.J.Malecela should take a chill pill and relax,This Constitutional Proposal is for the National interest and not for the Chama cha Mapinduzi's interest.Malecela Junior should take that into his big head.
 
CCM BADO INA IMANI KUBWA NA TUME YA KATIBA

Nape Nnauye
NA MWANDISHI WETU
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimesema bado kina imani na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya.

Imesema licha ya CCM kutofautiana kimawazo katika baadhi ya maeneo katika rasimu ya kwanza ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini haina ugomvi na tume hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

"Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii, na kwa kweli tunamatumaini nao sana kuwa watatimiza wajibu wao kwa weledi mkubwa", alisema Nape.

Nape alibainisha kwamba pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza ya katiba , CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe inapendekeza serikali mbili.

"Kama mnavyoona katika hili, wakati tume inapendekeza muundo wa serikali tatu sisi CCM tunapendekeza muundo wa serikali mbili, lakini hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye mawazo tofauti na yetu", alisema Nape na kuongeza;

"Kumekuwepo na ripoti na makala kadhaa zinazojaribu kuonyesha kama vile kuna mvutano kati ya tume na CCM, au CCM na wengine wenye mawazo tofauti na CCM. Ukweli ni kuwa hali hiyo inayojaribu kujengwa kwa nguvu si ya kweli. Tuache hoja zishindane kwa hoja na nguvu ya hoja ndio iwe msingi wa ushindani".

Nape alitaka ushindani uwe kwenye hoja bila kushutumiana ili jatimaye mawazo ya wengi yasikilizwe na kuzingatiwa.

Alisema, CCM inasisitiza kuwa itaheshimu mawazo ya Watanzania, kwani katiba inayotengenezwa ni ya watanzania wote bila ya kujali itikadi zao.

"Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaounga mkono baadhi ya hoja za CCM hasa hoja ya serikali mbili. Tumeshuhudia maoni ya wajumbe wengi wa mabaraza na wananchi kwa ujumla wakiunga mkono mawazo haya ya CCM ya muundo wa muungano wa serikali mbili na hoja kadhaa zingine", alisema Nape na kuongeza;
Nape Nnauye,

Hiyo mijadala unaifanyia wapi ili nasi watanganyika tujumuike nawe kujadiliana kwa hoja? Hatukuoni kwenye mijadala yoyote; Vinginevyo, kwa manufaa ya CCM, ni muhimu kamati kuu ya CCM (wewe ukiwa ni mmoja wa wajumbe wake) muelewe kwamba imefikia mahali ambapo wananchi wengi wataweza kustahimili kwa urahisi sana kifo cha ccm kuliko watakavyoweza kustahimili kifo cha Tanganyika;
 
- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?

- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!Le Mutuz
Je, pale wananchi wanaposoma maagizo ya CCM ni sawa?
 
Back
Top Bottom