Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Wajumbe, naomba niwathibishie kwamba maneno aliyoyasema Waziri Nape Nnauye kuhusu ushindi katika uchaguzi siyo mzahaa. Hatanii, Nape ni jambazi la kura.
Katika uchaguzi wa 2020 aliyekuwa mgombea wa Chadema jimbo la Mtama Ndugu Mathew alive alitekwa na watu, "wanaojulikana" saa chache kabla ya muda wa kurejesha fomu kuisha yaani saa kumi alasiri. Kijana huyu aliachiwa baada ya saa kumi na hivyo kukosa fifa za kugombea na hivyo Nape kupita bila kupingwa. Aibu!
Baada ya kuhenyeshwa na Magufuli kwa uongozi wa ujanja ujanja hatimaye Magufuli akafariki katika kifo tata had leo Wasukuma hawajaambiwa ni nini hasa kilimuua ndugu yao lakini Nape akisema, "Mungu ameamua ugomvi". Akamshirikisha Mungu kwenye suala la uovu wake.
Leo Nape anamfundisha kada mwenzie namna ya kushinda uchaguzi kihalifu lakini pia akimshirikisha Mungu. Ibilisi!
Naomba nikiri mbele yenu wana-Jamii Forum kwamba Nape amewahi kunipigia simu kwa kunishambulia na kudai kwamba, "namshambulia hapa jimboni Mtana". Lakini katika maneno yake yote ya kejeli, shombo, matusi kwangu pia aliniambia maneno yafuatayo;
"Usidhani sikufuatilii unavyonishambulia. Lakini nikuhakikishie kwamba Ubunge wa Mtama nitaacha kwa hiari yangu 2030". Pigia mstari maneno "KWA HIARI YANGU". Nini kinampa kiburi na jeuri Nape kuachia jimbo kwa hiari yake? Je, 2025 nani mwingine atatekwa?
Kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama havichunguzi kauli kama hizi. Kwa nini kama wapiga kura wasioone kwamba kauli hii inatosha kabisa kumfurusha Nape uongozini maana amemchafua hata mteuzi wake. Kama waziri anajua mbinu haramu za kupoka haki za watu (kura) kwa nini tusiamini ndiyo taswira halisi ya Bosi wake. Nape asipuuzwe wala kulifanyia mzaha kauli hii. Anamaanisha!
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!