Nape huwa hasemi uongo, huyu ndio mtu mkweli pekee ndani ya CCM

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Ukweli wa kwanza wa nape ni pale aliposema CCM itashinda hata kwa goli la mkono. Sio TU alitoa kauli hii Bali alishiriki kifanikisha goli la mkono,ingawa baadae yeye na wenzake walibatizwa kwa moto.

Kauli ya pili ya ukweli aliyoitoa ni hii ya Sasa kua CCM haitegemei kura zilizopigwa,Bali inategemea muhesabu kura na mtangaza matokeo.

Hizi kauli mbili ni kauli za kweli kabisa na ndio maisha ya CCM wao kwa wao au wao dhidi ya wengine.
Alichokisema ni kweli kabisa na wanaomkosoa huko kwao wao ndio wanasema uongo
Lakini pia nape aliwahi kutoa kauli kulingana na vie alivyokua anajisikia moyoni mwake baada ya Jiwe kuanguka,
Alisema kua,"Mungu amemaliza kesi",ni kesi Gani?,anajua yeye.

Katika amri kumi za Mungu Kuna amri moja inasema usiseme uongo, hapa Nape kasema ukweli.

Nape apewe maua yake Kwa tabia yake ya ukweli. Kwa sababu kwenye chama Chao Kuna kauli mbiu inasema "nitasema kweli daima,fitina kwangu ni mwiko"

Pia soma:Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
 
Wizi wa kura ndiyo mtindo wao hao maccm Kwa miaka yote.

Tofauti ni kuwa Nape amekuwa mkweli Kwa kutamka hadharani, wakati kina Makala, wao wanakanusha kauli ya Nape, wakati gizani wanatekeleza vivyo hivyo anavyotamka Nape!
 
Kwa kauli ya Nape ambaye Ni waziri katika serikali ya CCM, amedhihirisha kwamba EDWARD LOWASA alishinda uchaguzi 2015. Sio maneno yangu. Ni ya Nape.
 
Wizi wa kura ndiyo mtindo wao hao maccm Kwa miaka yote.

Tofauti ni kuwa Nape amekuwa mkweli Kwa kutamka hadharani, wakati kina Makala, wao wanakanusha kauli ya Nape, wakati gizani wanatekeleza vivyo hivyo anavyotamka Nape!
Hivi hizo kura huwa mnaibiwa nyie mkiwa mmezubaa wapi?maana tatizo linaweza likawa sio ccm hapa
 
Siku zake za uwaziri zinahesabika...yy na mwenzie marope
 
Nadhani Tanzania imetosha sasa kulalama na kujadili matatizo.

Huu ni muda mwafaka wa kuzungumzia mikakati madhubuti na fanisi ya kuleta ufumbuzi chanya.
 
Ule uchaguzi mkuu 1995 sijui kwa Mrema lakini kwa Lowasa 2015 aliibiwa kura za kutosha.
Huyu Nape ndio msema kweli kule Chama Chakavu maana kuna siku alishasema tena kuwa Chama Chakavu kinashinda uchaguzi hata kwa "bao la mkono"
 
Ukweli wa kwanza wa nape ni pale aliposema CCM itashinda hata kwa goli la mkono. Sio TU alitoa kauli hii Bali alishiriki kifanikisha goli la mkono,ingawa baadae yeye na wenzake walibatizwa kwa moto.

Kauli ya pili ya ukweli aliyoitoa ni hii ya Sasa kua CCM haitegemei kura zilizopigwa,Bali inategemea muhesabu kura na mtangaza matokeo.

Hizi kauli mbili ni kauli za kweli kabisa na ndio maisha ya CCM wao kwa wao au wao dhidi ya wengine.
Alichokisema ni kweli kabisa na wanaomkosoa huko kwao wao ndio wanasema uongo
Lakini pia nape aliwahi kutoa kauli kulingana na vie alivyokua anajisikia moyoni mwake baada ya Jiwe kuanguka,
Alisema kua,"Mungu amemaliza kesi",ni kesi Gani?,anajua yeye.

Katika amri kumi za Mungu Kuna amri moja inasema usiseme uongo, hapa Nape kasema ukweli.

Nape apewe maua yake Kwa tabia yake ya ukweli. Kwa sababu kwenye chama Chao Kuna kauli mbiu inasema "nitasema kweli daima,fitina kwangu ni mwiko"

Pia soma:Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
Kama ndiyo hivyo basi ukweli huo ufanyiwe kazi usizae machafuko,tuko kwenye kizazi kingine hiki,tusichukulie poa
 
Back
Top Bottom