Nape na "Hoja yako ya Serikali Tatu" Unazisoma alama za nyakati?

Nape na "Hoja yako ya Serikali Tatu" Unazisoma alama za nyakati?

Profesa

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
905
Reaction score
624
Nimekuwa nikifuatilia kauli mbalimbali za viongozi wangu wa CCM na wale wa serikali kupitia mikutano ya hadhara, midahalo na hata kupitia vyombo vya habari kuhusiana na Katiba mpya.

Ziko nukuu nyingi tunazoweza kufanya kwa kauli zinazopishana ndani ya CCM na kila mmoja akiwa na mamlaka ya kile anachosema, lakini hizi chache za hivi haribuni naweza kuanza nazo.

Reference nzuri ni ya Waziri wa Sheria na mambo ya Katiba (kwa tafsiri sahihi) Mh Mathias Chikawe, katika kipindi cha hivi karibuni cha Dk 45, ITV alitahadharisha kuhusu mchakato wa Katiba na alionekana kutoa muelekeo wa mambo hasa pale alipofafanua kuhusu utaratibu uliopelekea kuwepo kwa Rasimu na kuhusu swala la Serikali Mbili au Tatu. Kimsingi alikuwa makini kutokuonyesha upande anaouegamia lakini tayari ujumbe wa wazi ni kuwa Rasimu hii ya Katiba na utaratibu wake umeletwa na serikali (ya Chama cha mapinduzi) kwa nia njema tu na mpaka kupata rasimu, hekima na utaalamu wa hali ya juu umehusika na Rais wa nchi alibariki mipango yote hii (Tume ikiwa inateuliwa na kuratibiwa na Rais mwenyewe??).

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana: ingawa kwenye radio na Runinga walionyesha na kutangaza sauti na picha zilizorekodiwa za Katibu Mkuu wetu wa CCM (pamoja na yanayosemwa) kauli yake ilijaa umakini sana, alionyesha kuwatahadharisha wananchi kuamua kile wanachoona kinafaa na kuwa serikali ya CCM itayaheshimu maoni yao, iwapo wataamua serikali mbili au tatu basi vyovyote vile itaheshimiwa. kasoma alama za nyakati.

Kwa upande wako bwana Nape, unaonekana majukwaani ukitumia nguvu nyingi sana kuonyesha kile unachodai ni "Msimamo wa CCM" kuwa serikali mbili ndio sahihi na kutumia upinzani kujenga hoja yako (huku ukisheheni siasa za vijembe, ambazo kimsingi zimepitwa na wakati). Sikufurahishwa sana na staili yako ya kushawishi wanachama wa CCM kuhusu hoja ya serikali mbili (na Wenzangu wengi hawakusemi vema) na ulionekana kukosa umakini kabisa katika hoja zako. Ungekuwa unaleta vigezo makini vyenye ushawishi. Pia ingefaa ukatenganisha wakati wa kuushambulia upinzani hasa kwenye hoja za msingi kama hii ya Katiba ambayo ni ya kitaifa, na kutupotezea muelekeo tukashindwa kuunganisha kile unachokitetea kama ni kutokana na kilivyo au ni kwasababu upinzani wamesimama upande mwingine? Mfano, Serikali ya CCM imejinadi kuwa ifikapo 2015 umasikini babibai (kauli ya Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini wakati akifafanua Mpango wa Gesi kuja Dar na ameendelea kunukuliwa na TBC kila mara katika vionjo vya matangazo ya kiserikali), wewe unatuambia serikali tatu ni gharama, tupe vigezo, na vyanzo vya mapato vinavyopendekezwa na jinsi gharama zinavyoongezeka.

Kimsingi siku zote hizi unapoongea, ninaona kama unaweweseka na CHADEMA, na hapo kiukweli unawapandisha sana chati, husemi la CCM bila kutaja au kunukuu ya CHADEMA, kwanini? Kwani sisi CCM hatuwezi tukaongea yetu yenye mvuto na hoja tukamaliza tukawaacha wananchi waamue? na pia nimegundua unatumia nguvu nyingi kueleza hisia zako bila kusoma kauli za viognozi wako, sasa sijui nani kakutuma, maana kuna kutumwa na Vikao rasmi vya chama na kuna kujaribu kujipigia debe au kuwapigia debe akina fulani (maana najua ndani ya CCM makundi hayajaisha).

Wananchi wa leo sio wa jana usipoongea wewe vyombo vya habari vinaongea nao na vinawapa elimu ya kutosha, so watakupima wewe na kile wanachoendelea kuelimishwa na ulimwengu wa leo wa utandawazi. Kifupi, hawadanganyiki bila hata kuwa na chama chochote, wanakusikiliza ili wajue wanabaki CCM au waende pengine. Busara yako ya leo inapima ya kesho, usidanganyike na hali uliyonayo sasa, dhamana uliyopewa ni kubwa sana.

Soma alama za nyakati usije ukahaha pale mambo yatakapogeuka. Kumbuka mchakato wa Kuelekea vyama vingi, ni nini kilitokea? Sawa shawishi serikali mbili, lakini unasoma vema alama za nyakati na mbinu zako za ushawishi zinalenga umakini na uzito unaostahili kushawishi bila kuonyesha dalili ya kupagawishwa na upinzani? ​

Kinachonishangaza ni pale ambapo unatushawishi kuwa "CCM yenyewe inapinga kile ilicholeta kupitia serikali yake".
 
Unapoteza muda kuongea maneno ya Busara kwa mtu Kilaza. Angekuwa na uelewa mdogo tu umemshauri vizuri sana huyu mchumia tumbo, halijui alitendalo.
 
Back
Top Bottom