Nape na January Makamba mpaka sasa sijaona shukrani zenu kwa rais Samia kwa kuwapa dhamana mlizokuwa nazo, je ni nongwa ya kutumbuliwa?

Nape na January Makamba mpaka sasa sijaona shukrani zenu kwa rais Samia kwa kuwapa dhamana mlizokuwa nazo, je ni nongwa ya kutumbuliwa?

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Posts
8,271
Reaction score
9,113
Kawaida ninavyofahamu mimi mamlaka ya uteuzi ina weza teua na kutengua bila kuhojiwa, nilitegemea vijana hawa kwa maana ya January Makamba, Nape Nnauye na Byabato wamshukuru Rais Samia kwa dhamana walizotumikia, lakini naona kimya.

Je, hawaamini kama cheo ni dhamana?
 
Kwani katiba inasemaje kuhusu ilo? Tuanzie hapo Kwanza kiongozi.
Asante

KAZI ni kipimo cha UTU
 
1721796932317.png
 
Kawaida ninavyofahamu mimi mamlaka ya uteuzi ina weza teua na kutengua bila kuhojiwa,nilitegemea vijana hawa kwa maana ya January Makamba,Nape Nnauye na Byabato wamshukuru rais Samia kwa dhamana walizotumikia,lakini naona kimya,je?,hawaamini kama cheo ni dhamana?
Uchungu bado haujaisha.....
 
Kawaida ninavyofahamu mimi mamlaka ya uteuzi ina weza teua na kutengua bila kuhojiwa, nilitegemea vijana hawa kwa maana ya January Makamba, Nape Nnauye na Byabato wamshukuru Rais Samia kwa dhamana walizotumikia, lakini naona kimya.

Je, hawaamini kama cheo ni dhamana?
Uliposema tu vijana nikajua ni ushauri wa kinaa. Hao jamaa sio vijana rekebisha hilo. Halafu sio hao akina Nape tu, ccm yote kama chama na wanachama wake hawaamini kwenye kupoteza madaraka, unataka wapongeze kinafiki ili iweje?
 
Badala yake wanaziambia taasisi zisambaze meseji za kuwashukuru wao kwa utendaji bora😆😆😆 wamewaponza wenzao mpaka wametenguliwa
Nape alimuingiza Maharagwe Cha kike. Na kwa kitendo cha ule utenguzi Nape ajue hakuna atakayemgusa, hakuna hata atakaye mtangaza mshindi wa kura za wajumbe. Anaweza kuwahonga wajumbe na wakampigia kura kweli, tatizo linakuja Nani hajipendi atatangaza kwamba nape ndio kashinda?
Infact Nape is as good as a dead dodo politically.
 
Kuna watu wana bahati sana nchi hii.
Unawasikia wao tu, wanateuliwa na kutenguliwa, wanateuliwa tena na kutenguliwa wao tu. Yaani mtu anateuliwa zaidi ya mara kumi utafikiria hakuna watu wengine wenye uwezo na staha hapa nchini.
Na kuna watu wanategemea kazi za kuteuliwa tu.
Hawawezi kujiajiri au kuajiriwa pangine.
Nchi ni yetu sote
 
Hii ni ya enzi za Magufuli tena nakumbuka Mzee Mwinyi alimaind sana picha yake kutumika wakati huo (Makamba alivyofutwa kazi na Jiwe) ikizingatiwa picha yenyewe ilichukuliwa miaka mingi nyuma ktk tukio jengine kabisa.
Kiukweli hawa akina Makamba, Nape na Byabato wamemdharau mama, wanaona ilikuwa ni haki yao wao kuendelea kuwa mawaziri kana kwamba nchi hii ni ya baba zao.
 
mama sindiiii alimind kuona anatumika kisiasaaaa
 
Back
Top Bottom