PreGE2025 Nape Nnauye awaonya CHADEMA 'Kuweni na adabu kwa Rais Samia'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, ameweka wazi msimamo wake kuhusu hoja zinazoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuhusu unyonyaji katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye zao la korosho, akisema wengi wao walikosa ujasiri wa kuwatetea wakulima wakati suala hilo lilipokuwa likipigiwa kelele bungeni mwaka 2018.

Akizungumza mbele ya wakazi wa Kilwa mkoani Lindi siku ya Alhamisi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wakati wa ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, Nape amesema ni unafiki kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani kujifanya kuwa na uchungu na zao la korosho wakati historia inaonesha walikaa kimya wakati wakulima walihitaji sauti yao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akimtaja aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema, Nape alisema licha ya kuwa na fursa ya kuwatetea wakulima wa korosho wakati wa mjadala mzito bungeni, alichagua kunyamaza.

“Tulikuwa tunapigana kwa ajili ya wakulima wa korosho, tukasimama kuwatetea, lakini hawa walikaa kimya. Leo wanajifanya wana uchungu, ni wanafiki,” amesema Nape.

Katika kueleza mchango wa serikali ya sasa, Nape amesema hakuna Rais aliyewahi kusimama na mkulima wa korosho kama Rais Samia Suluhu Hassan. “Wanakulwa, wanakusini, wakulima wa korosho, nataka niseme hivi, katika historia ya zao la korosho, hakuna Rais aliyesimama na mkulima kama Mama Samia. Hayupo!” amesisitiza.
 
Raisi Samia ataipata adabu kwa watoto wake, wakwe zake, n.. Wajibu wa Chadema na wengine ni kuheshimu nafasi yake, na wala sio yeye binafsi
 
Hahahaaaa
Yaani huyu sa100 washamuona bibi yao rahisi kumuingia hapo Nape anatafuta nitoke vp tuu hana lolote!
 
Chama legelege huzaa serikali legelege. Ccm ni chama cha hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…