Nape Nnauye: CCM tunapinga Uwepo wa Serikali Tatu.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepinga muundo wa Muungano wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Chama hicho tawala kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa mbele ya Tume hiyo yanabaki kama yalivyo, hivyo msimamo wao ni kuwapo kwa muungano wenye muundo wa Serikali mbili.

“Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.

Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM wakiwamo, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na John Malecela, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na baadhi ya wabunge ambao mara kadhaa wamekaririwa wakipinga pendekezo la Serikali tatu.

Hata hivyo, Nape alisema matamshi ya viongozi hao yalikuwa ni maoni yao binafsi na kauli yake ndiyo rasmi ya chama hicho... “Mimi ndiye msemaji wa chama hiki. Ndiye ninayeeleza msimamo wa chama chetu, yanayozungumzwa na watu wengine hata kama ni viongozi siyo msimamo wa chama ni maoni yao binafsi.”

Habari ambazo gazeti hili ilizipata zinasema katika kikao hicho cha CC kulijitokeza hofu ya suala la wananchi kuwa na mamlaka ya kuwang’oa wabunge ikiwa hawatatekeleza masilahi yao na kwamba pendekezo hilo lina upungufu kwani halitafsiri masilahi hayo ni yapi.

Waunda kamati

Nape alisema rasimu iliyotolewa na Tume siyo waraka wa mwisho kwani bado unatoa fursa kwa Watanzania kuijadili na kutoa maoni yao na kwamba CCM kitatumia nafasi hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu jambo hilo.

Alisema chama hicho kitawasiliana na wanachama wake zaidi ya 6,000 nchini ili waendelee kutoa maoni yao kuhusu suala hilo.

“Wengi wanadhani rasimu hii ndiyo ya mwisho… hii ni ya mwanzo tu, itajadiliwa italetwa ya pili na ya tatu, kwa hiyo hatuwezi kusema kilichoelezwa kwenye tume ndiyo msimamo. Ndiyo maana tumeamua kurejesha suala hili kwa wanachama wetu liendelee kujadiliwa,” alisema na kuongeza:

“Kama wanachama wetu wakiamua kuwepo kwa Serikali tatu, hatutachakachua, tutayachukua na kuyapeleka kama msimamo wetu, lakini tutakubaliana ikiwa uamuzi utakuwa umewahusisha wanachama wetu katika ngazi zote.

“Hatuangalii kipengele kimoja tu. Tutapitia vipengele vyote hadi kuzimaliza kurasa zote zaidi ya 70 zinazoainisha mapendekezo ya Tume ya Jaji (Joseph) Warioba.”

Alisema wanachama wake wanapaswa kuipitia na kuijadili rasimu hiyo kwa kuzingatia mapendekezo kilichoyatoa awali wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya.

“Tulitoa maoni yetu na sasa tunaijadili Rasimu ya Katiba Mpya kwa kuzingatia maoni yetu yale, CCM tunakwenda kwa mujibu wa sheria,” alisema. Habari kutoka ndani ya CC ya CCM zinasema chama hicho kimeipa kazi kamati ambayo ilitumika kuandaa mapendekezo yake awali, kupitia rasimu hiyo na kufanya ulinganisho wa yale ambayo chama hicho kilipendekeza dhidi ya yale yaliyozingatiwa katika Rasimu ya Katiba hiyo.

“Kamati itafanya ulinganisho na baada ya hapo tutakwenda kwa wanachama kuwaeleza ni yapi tulipendekeza kama chama na ni yapi ambayo Tume imeyazingatia na hapo tutapata mawazo yao ambayo tutayatumia katika ngazi ya mabaraza ya Katiba,” kilisema chanzo chetu.

Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
 
Kabla hata ya kuanza kwa zoezi la kukusanya mawazo ya wananchi kupitia tume ya Warioba, tayari wananchi tulikuwa tumeisha fungwa midomo kwa kuwekewa mipaka katika swala muhimu la muungano ambalo kimsingi ni tatizo SUGU tokea kuanziswa kwake April 1964 mpaka mwaka 2013 ambapo viraka zaidi ya 10 vimeishawekwa bila mafanikio huku mafarakano yakizidi kila kukicha katika hii ndoa tegemezi.

Hiki kipengele katika Hadidu za Rejea hakikupaswa kuwepo pale kiliposema,

Mwarobaini wa matatizo ya msingi siyo muungano wenye serikali moja, mbili au tatu bali ni sauti kwanza ya wananchi kupitia REFERENDUM kuamua wanataka kuendelea na hii ndoa TEGEMEZI au kuachana nayo. Kama ikitokea wananchi wengi wataamua kuendelea kuwepo na muungano basi wapewe tena nafasi ya kuamua ni muungano gani wanataka kuendelea nao.

Kinachotakiwa kwa sasa TUPIGANIE REFERENDUM kujua mwerekeo wetu kwa kizazi chetu kijacho.

One Look Is Worth A Thousand Words kama picha hapa chini zinavyoonyesha.
 

Attachments

  • image.jpg
    70.6 KB · Views: 474
  • image.jpg
    72.2 KB · Views: 528
Well, ni maoni yao hayo ila waelewe kuwa katiba inayoandaliwa ni ya watz wala siyo ya chama hicho.

CCM inatambua kwamba katiba ni ya wananchi ndiyo maana hujawahi kusikia CCM ikitishia kujitoa kwenye huu mchakato wa kuandaa katiba mpya.
 
Ina maana hiyo katiba ni ya ccm? Kumbe ndo maana ccm ilichakachua mabaraza ya katiba! Kweli tunasafari ndefu mpaka kupata katiba ya wananchi! Huwezi kulinda muungano kwa serikali mbili, vinginevyo utavunja muungano!
 
Ina maana hiyo katiba ni ya ccm? Kumbe ndo maana ccm ilichakachua mabaraza ya katiba! Kweli tunasafari ndefu mpaka kupata katiba ya wananchi! Huwezi kulinda muungano kwa serikali mbili, vinginevyo utavunja muungano!

Hivyo "viroba" huwa mnanyweshwa muda gani? Mbona muda wote vichwa vyenu vijana wa Bar Vichaa vinakuwa na "moto"?

Baada ya kuisoma hii thread, ni wapi imesemwa katiba ni ya CCM?
 
Alisema chama hicho kitawasiliana na wanachama wake zaidi ya 6,000 nchini ili waendelee kutoa maoni yao kuhusu suala hilo.

[/FONT][/SIZE]

jamani hapa si ndo kuwalisha watu maneno? kwani watanzania ni wajinga kiasi cha kuambiwa cha kufanya na Nape Nnauye , binafsi nnaona kama magamba wameteleza, toeni maoni yenu kama chama then na wananchi watatoa ya kwao
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa bandiko hili Ng'wamapalala. Napata tafsiri yenye sura mbili hapa: Kwanza CCM inakubali haina uwezo wa kuishawishi Zanzibar kukubali Serikali Moja ili hali wakijua upepo wa kisiasa ulivyokaa hautaki Serikali Mbili. Katika Serikali mbili Zanzibar wanainyonya bara. Zanzibar ni Kupe, na hili kupe tunalipulizia DDMaki mwaka huu. Dawa hiyo haikufaa, tunaweka dozi kubwa ya DIP mpaka hilo kupe litoke. Muungano hakuna! Hatuwezi kuendelea kuvimbisha matumbo wa wabunge na wachangiaji uongozi wengine kutoka nchi jirani hatuna faida yoyote nayo. Hizo fedha zisaidie maendeleo mengine Tanganyika. Kwa kauli hii ya CCM kutaka Serikali Mbili, muungano hakuna. Tumaini kidoooogo lingekuwepo wangependekeza Serikali moja. Kikwete anaingia katika historia kama Gorbachev wa Afrika! And its done!
 
kwa jinsi rasimu ya katiba ilivyo,chama cha mapinduz kimeonesha nia mbaya ilionayo kwa kupinga maoni yaliotolewa na wananch,nadhan ccm kuna haja ccm kuheshimu rasimu hiyo,ccm inalengo la kuleta machafuko nchini,watanzania tusikubali kurubuniwa na ccm chenye uroho wa madaraka,hakika kuweni macho na hlo,
 
Ina maana hiyo katiba ni ya ccm? Kumbe ndo maana ccm ilichakachua mabaraza ya katiba! Kweli tunasafari ndefu mpaka kupata katiba ya wananchi! Huwezi kulinda muungano kwa serikali mbili, vinginevyo utavunja muungano!

haya ndiyo madhara ya kukurupuka nape kasema ni ya watanzani na wanairudisha kwa wananchi ikajadiliwe na watoe maoni yao.
 
Ina maana waliotoa maoni kwenye mikutano ya tume wote sio "wanachama" wa CCM?

Mi kuniambia muungano wenye serikali mbili siwaelewi... What type of muungano is that.
Yes, binafsi nataka serikali 2, yaani Tanganika+Zanzibar (+ujirani mwema)...
 
Unaongelea nini wewe? CCM ni taasisi na inayo haki ya kutoa maoni yake juu ya rasimu kama ambavyo taasisi nyingine yoyote inavyoweza. Ukitaka kila mtu aipongeze rasimu eti kwakuwa wewe unaipenda, hiyo itakuwa siyo demokrasia.
 
Jana Stella mwampamba alisema CHADEMA hakina msimamo eti kilipinga Tume halafu sasa kinaunga mkono rasimu. sasa mbona CCM nao wanawaiga CHADEMA kutokuwa na msimamo - maana waliunga mkono Tume sasa wanaipinga. inaonekana CCM na CHADEMA zote zinamchanganya Stella.
 

Tanganyika + Zanzibar + Ujirani mwema. Hatutaki Tanzania bara + Zanzibar + Majungu...
 
CCM kuweni na huruma na Wanzazibar jaman,wamemwaga sana damu kudai mamlaka yao huru kwnn mnataka kuendelee kuwakandamiza?au mnataka wajivike mabomu muwapige na propaganda za kidini ndo muamini?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivyo "viroba" huwa mnanyweshwa muda gani? Mbona muda wote vichwa vyenu vijana wa Bar Vichaa vinakuwa na "moto"?

Baada ya kuisoma hii thread, ni wapi imesemwa katiba ni ya CCM?

Watu mbona mnawashwa sana na huu Muungano! Aidha serikali moja au tatu.Masuala yenu ya serikali mbili tulishachoka.Na ss tanganyika tuwe na Serikali yetu sasa.
 
Tanganyika + Zanzibar + Ujirani mwema. Hatutaki Tanzania bara + Zanzibar + Majungu...

Very correct Mkuu! Good neighbors; that should do.
Wakileta za kuleta tunawashukia kama mwewe na panya!
 
Kitawasiliana na "wanachama wake zaidi ya 6000" inchini ili waendelee --
 
Wanakataa serikali tatu lakini hawatoi sababu na hawasemi faida ya serikali mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…