Nape Nnauye: CCM tunapinga Uwepo wa Serikali Tatu.

This just make sense; hivi watu walitaka CCM ichukue msimamo gani? Lakini pia kwani msimamo wa serikali tatu ni LAZIMA uwe wa kila Mtanzania?
 
Mkuu mi naona bora ya ccm wamewaomba watanzania waendelee kutoa maoni yao lakini chadema hata hawajulikani wapo upande gani mara wajitoe mara warudi na mara wasuse sijui viongozi viongozi wao wapoje.
 
Ina maana hiyo katiba ni ya ccm? Kumbe ndo maana ccm ilichakachua mabaraza ya katiba! Kweli tunasafari ndefu mpaka kupata katiba ya wananchi! Huwezi kulinda muungano kwa serikali mbili, vinginevyo utavunja muungano!

uroporopo!
 
haya ndiyo madhara ya kukurupuka nape kasema ni ya watanzani na wanairudisha kwa wananchi ikajadiliwe na watoe maoni yao.

Kasema anairudisha kwa wanachama wa CCM. Wanachama wa CCM sio wananchi wote. CCM watoe ya kwao, taasisi nyingine zitoe ya kwao, wananchi watoe ya kwao, Tume itupe matokeo ya wengi wape. Nakubaliana na mjumbe hapo juu aliyesema JK anaandika historia ya kuwa Gorbachev wa Afrika. Zanzibar ni kama Lesotho au Swaziland kuwe na muungano au usiwepo bado watakuwa wanatutegemea kwa asili mia kubwa.
 
Mimi shukrani zangu nazipeleka kwa rais jk kwa kuipa uhuru wa kutosha tume ya katiba ili ifanye kazi yake kwa uhuru mwisho wa siku tutapata katiba bora.
 
haya ndiyo madhara ya kukurupuka nape kasema ni ya watanzani na wanairudisha kwa wananchi ikajadiliwe na watoe maoni yao.
Umefumukia wapi wewe? We hujaona kataja hadi idada? Au siku hizi watanzania tumefikia millioni 6?(Japo pia imekosewa na kuandikwa 6000)huko kwenye vikao vyenu huwa mnalogwa muwe mazezeta,Eti ameipa kamati kazi ya kupitia vifungu vyote na kuazama ni vingapi kati ya walivyopendekeza WAO(ccm)vimefanyiwa kazi,
Hapo hapo wewe na mazuzu wenzako munadai eti ccm inadai katiba ya wananchi
 
  • Tukitegemea vyama vya siasa ndio vitupe mwongozo kwenye hili suala la muungano; tutegemee mengi.Hawa wakati fulani wanakuwa na agenda za siri.
  • Tukumbuke wakati tunajadili haya yote; Maalim seif huko Zanzbar anachochea kuvunja muungano "Zanzbar tunataka mamlaka kamili; Tunataka kiti chetu UN" Ni maneno ambayo amekuwa akiyakariri maalim.


  • Juzi Katika kipindi cha Dakika 45, Jaji warioba kasema wameona wapendekeze serikali tatu kwa sababu pendekezo tofauti na hilo linaweza kuvunja muungano.(ni nani anataka kuvunja muungano na kwa nini ?)


  • Hoja ya kina Nape ya kuendelea na serikali mbili haina maelezo ya kina na kuridhisha.


  • Hoja yenye maelezo ya kina na ya kuridhisha ni Muungano wa serikali moja ila hoja hii haiungwi mkono na wanasiasa bila sababu za msingi.


  • Kuna hoja kwamba Wazanzbar Hawataki Serikali moja,mara hawataki mbili, mara hawataki tatu? Je! kama hawataki tunawalazimisha wa nini?


  • Tunataka referandam baaaas!
 
CCM kutotaka au kutaka haitoshi. Watueleze kwa nini wanataka serikali mbili na siyo tatu au moja.
 
aidha serikali ya majimbo au serikali tatu, serikali moja au mbili ni uliberali
 
CCM kutotaka au kutaka haitoshi. Watueleze kwa nini wanataka serikali mbili na siyo tatu au moja.
Mkuu; wanaotaka serikali mbili hawana hoja critical kwa sasa zaidi ya kusema nyerere alipendekeza hivyo.


Wanaotaka serikali tatu nao hudai lengo ni kuunusuru muungano japo wanashindwa kueleza ni kivipi tutanufaika na uwepo wa serikali zote hizo dhidi ya gharama za kuziendesha.

Wanaotaka serikali moja; wana sababu clear na za kueleweka kwamba kama tunataka mshikamano, seikali moja ndio mshikamano wa ukweli na usiotatanisha.
 
JK bingwa wa fitna! kamtanguliza Nape kwenye hili, kwenye uzinduzi wa rasimu alimtanguliza Ghalib Bilal!!
 
jamani hapa si ndo kuwalisha watu maneno? kwani watanzania ni wajinga kiasi cha kuambiwa cha kufanya na Nape Nnauye , binafsi nnaona kama magamba wameteleza, toeni maoni yenu kama chama then na wananchi watatoa ya kwao

na kwa kusema kuwa "kama wanachama wataamnua, sisi hatutachakachua...."
hapo kuna katabia na kamchezo amekiri kuwa huwa wanakafanya, ila anaahidi not this time katika suala hili.
 
Last edited by a moderator:
Viongozi wetu inabidi waelewe kuwa watanganyika wamechoshwa na huu muungano. Hauna faida kwetu,na hatuna chuki na Wazanzibari. Ila tuna kazi kubwa inayotusubiri ya kujenga institutions za Tanganyika yetu, from scratch.

Sasa haya mambo ya serikali tatu au mbili yameshatukinaisha na tunaomba mtusikilize. Kuvunjika kwa muungano siyo jambo la aibu na wala siyo jambo la uadui. Misri na Syria ziliwahi kuungana na wakavunja muungano. Mbona hawakorofishani?

Serikali moja, ama haiwezekani basi tuishi kwa amani kama nchi mbili jirani.
 
Kwa tofauti kubwa wanayokuja nayo CCM na CUF, hawa hawaeleweki -wana uhuru wa kutoa maoni lakini wasifikiri wao ndiyo Tanzania. Rasimu ya Katiba Mpya ni matokeo ya maoni kutoka jamii yote ya Tanzania na mtanzania mmoja mmoja, ni sauti ya watanzania wengi walivyosema. Kutokana na matamshi ya Katibu wa CUF, Zanzibar inataka autonomy inayoipa Zanzibar kuwa na madaraka kamili na CCM inataka kuturudisha nyuma. Serikali tatu ni karibu zaidi na matakwa ya Zanzibar kuliko serikali mbili. Ni dhahiri Tanzania bara na Tanzania visiwani wanataka mabadiriko kutoka serikali 2. Kwa maana ya nia safi ya muungano leo tungekuwa tunazungumzia serikali moja, nje ya hapa tunalazimisha tu. Tuheshimu maoni ya watanzania.
 
Hatuhitaji pungufu ya mamlaka kamili zanzibar,mpaka kieleweke,zanzbr kwanza porojo mwisho chumbe.
 
Haki ya kutoa maoni ni ya wote....... kila mtu anapaswa kusikilizwa mwishowe maoni ya walio wengi ndio yatapewa haki ya kuunda katiba.
 
Ccm Hata Hivyo Inapaswa ielewa katiba tunayoitaka ni mali ya wananchi na sio chama. wananchi wameamua kuwa na serikali tatu na sio warioba aliyeamua. pia ccm kupinga kuajibishwa kwa wabunge ni udhaifu mkubwa kwa chama kikongwe kama hicho wanataka kuendelea kutuletea wabunge feki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…