Nape Nnauye: CCM tunapinga Uwepo wa Serikali Tatu.

Hata mimi nataka serikali mbili
1:Serikali ya Jamhuri ya watu waTanganyika (Government of PEOPLES REPUBLIC OF TANGANYIKA)
2:Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Hizi porojo za muungano sasa basi.
 
CCM inatambua kwamba katiba ni ya wananchi ndiyo maana hujawahi kusikia CCM ikitishia kujitoa kwenye huu mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Haijatishia kujitoa bali inalazimisha serikali mbili
 
Tanganyika + Zanzibar + Ujirani mwema. Hatutaki Tanzania bara + Zanzibar + Majungu...
...kweli muungano wa serikali mbili ndo tunautaka Tanganyika na zanzibar, hizi mbili zitatupa serikali ya muungano yaani tanzania. thus lazima kwanza tuwe na serikali mbili huru ili tupate muungano....
 
CCM ni chama changu. Nipo humu tangu mwanzoni mwa miaka ya1980 mara baada ya kuhitimu masomo yangu ya Chuo Kikuu. Chama hiki kimekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwake hapo 1977. Kilirithi madaraka ya TANU na ASP.Kama chama chochote cha siasa,zipo nyakati za shida na raha. Zipo nyakati za changamoto za kisiasa.

Tangu kuanzishwa kwake,CCM haikuwahi kukumbana na upinzani wa kisiasa kama ulio sasa nchini.Huo ndiyo ukweli. Mfumo wa vyama vingi ulioasisiwa hapo mwaka 1992 sasa unakuwa shubiri kwa CCM kama chama tawala. Zamani kidogo,mtu yeyote aliyegombea uongozi kupitia CCM alikuwa na uhakika wa ushindi.Sasa ni tofauti. Vyama vingi vina nguvu ya ushawishi. Ingawa kuna vyama vingine vingi vya siasa nchini pinzani kwa CCM,CHADEMA ni tishio zaidi.

Kama chama kikuu cha upinzani nchini,CHADEMA kinaimarika kila uchao. Raha ya CCM inapungua kwa kasi. Hivi karibuni,Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyo chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba imetoa Rasimu ya kwanza ya Katiba mpya.Haraka sana CCM ikaitisha kikao cha Kamati Kuu kuijadili na kutoa msimamo wa chama. Ni jambo jema.

Jana,msemaji wetu Nape Nnauye amekaririwa akisema kuwa CCM haikubaliani na mfumo wa Serikali tatu. Akasema kuwa CCM haikupendekeza hivyo. Yenyewe haikutaka hata Serikali moja.Ilitaka Serikali mbili kama sasa.Pia Nape Nnauye akasema kuwa Kamati Kuu imemuomba Jaji Warioba aweke hadharani mtiririko wa Rasimu zote za Katiba mpya.

CCM inasahau mambo mawili muhimu. Kwanza,Tume ya Jaji Warioba ni Tume huru,Haiingiliwi wala kupelekeshwa na yeyote awaye. Hivyobasi,mtiririko wa Rasimu utatolewa na Tume kwa muda wake na kwa jinsi yake. Pili,CCM au chama chochote cha kisiasa nchini si lolote katika uundwaji wa Katiba.Katiba ni ya wananchi na wala si ya wanachama wa chama fulani cha kisiasa.

Matamshi ya Nape Nnauye (akiweka hadharani msimamo wa CC yaCCM) yaweza kutafsirika kama kuilazimisha Tume ya Jaji Warioba kupendekeza Serikali mbili. Kwa Katiba,CCM hawana ubavu huo na si lolote,si chochote.Isione donge kwakuwa mapendekezo mengi ya upinzani yamekubaliwa na Tume ya Jaji Warioba. Hiyo si demokrasia. CCM iache kuweweseka mapema hivi. Ina mambo mengi ya kufanya kutekeleza Ilani yake ya 2010-2015. Katiba mpya isiwe kisingizio chakuacha wajibu wetu kama chama tawala.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Tuesday, June 11, 2013
CCM wamkaanga Warioba
WAUNDA MABARAZA YAO YA KATIBA KUJADILI RASIMU
Na Hellen Ngoromera
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetofautiana na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, katika pendekezo la kutaka muundo wa serikali tatu katika rasimu ya Katiba iliyotolewa hivi karibuni.
Katika kupingana na maoni ya tume ya Jaji Warioba, Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM, imeamua kupeka rasimu hiyo kwa wananchi wake kuanzia ngazi ya matawi na kutaka yaundwe mabaraza ya Katiba ya chama hicho ili kujadili rasimu hiyo hususani muundo wa Serikali ya Muungano.
Wakati CC ikipitisha azimio hilo, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba, amesisitiza kuwa suala la serikali tatu kwa sasa haliepukiki kwani zisipokuwapo kuna hatari ya muungano kuvunjika.
Kauli ya Warioba imekuja huku kukiwa na mbinyo wa ndani na nje ya CCM, wakiwamo viongozi waandamizi wa chama hicho tawala na makundi ya urais 2015, kupinga pendekezo la kutaka kuwe na muundo wa serikali tatu.
Habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa CC kutoka visiwani Zanzibar, waliliambia gazeti hili kuwa wajumbe wa Zanzibar walicharuka na kuhoji kwanini Jaji Warioba aliamua kuingiza pendekezo hilo kwenye rasimu ya Katiba wakati msimamo wa chama anaujua.
Wajumbe hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walimshambulia Warioba kuwa si kweli kwamba Wazanzibari wengi walioulizwa kuhusu muundo wa serikali walipendekeza serikali tatu.
Katika kikao hicho mahususi kwa ajili ya kujadili rasimu ya Katiba kilichofanyika jana chini ya Rais Jakaya Kikwete, Kamati Kuu (CC) ya CCM imeazimia kuipeleka rasimu hiyo kwa wanachama wao kuanzia ngazi ya matawi ili ijadiliwe kwenye mabaraza ya Katiba ya chama kwa kuzingatia maoni yaliyopelekwa awali kwenye tume ya Jaji Warioba.
Hatua ya CC kushindwa kutoa msimamo na kuamua kuipeleka rasimu hiyo kwenye matawi yake imeongeza hofu ya CCM kuhusu muundo wa serikali tatu zilizopendekezwa na tume wakati chama hicho tangu awali msimamo wake ni muundo wa serikali mbili kama ilivyo sasa.
Tayari baadhi ya vigogo waandamizi wa chama hicho akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wamepinga kipengele hicho cha rasimu kinachopendekeza serikali tatu.
Hofu ya Sitta na wenzake wanaopinga ni kwamba mchakato wake umelenga kuvuruga muungano na kuibebesha mzigo serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kauli na misimamo ya kina Sitta ni maoni yao binafsi na kwamba wana haki ya kufanya hivyo kama Watanzania wengine.
Alisema msimamo wa chama utatolewa baada ya rasimu hiyo kujadiliwa na wanachama wao kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa ambapo katika ngazi ya taifa itajadiliwa na vyombo vikuu vya uamuzi vya Sekretarieti, Kamati Kuu na NEC.
Nape alifafanua kuwa wanachama watakachoamua ndicho kitakachochukuliwa na kupelekwa kwenye tume ya Jaji Warioba kama msimamo wa CCM.
“Kamati Kuu imekiagiza chama kijipange kujadili rasimu hiyo ndani ya chama kama baraza la kitaasisi la Katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza,” alisema.
Aliongeza kuwa jumuiya za chama za Umoja wa Vijana (UVCCM), Umoja wa Wanawake (UWT) na Wazazi zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba, hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huo.
“CCM kama baraza la Katiba la kitaasisi litapitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya chama yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wenu watashiriki kutoa maoni yao,” alisema.
Nape aliongeza kuwa pamoja na kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, CC inaiomba tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.
Alipoulizwa ni kwanini CCM inapata kigugumizi kutoa msimamo kuhusu rasimu hiyo kama walivyokwisha kufanya vyama vingine, Nape alisema wao hawakurupuki pasipo kuwashirikisha wanachama wao.
“Hiki ni chama kikongwe, haiwezekani kila kiongozi kutoa msimamo wake bila utaratibu. Sisi lazima tuoneshe mfano, si umesikia CUF Mwenyekiti wao, Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif, wanapingana kuhusu muungano,” alisema.
Jaji Warioba apigilia msumari
Wakati pendekezo la kutaka kuwe na serikali tatu limewagawa Watanzania, Jaji Warioba amesisitiza kuwa bila serikali tatu muungano utavunjika.
Jaji Warioba aliyasema hayo juzi usiku wakati alipokuwa akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa hewani na kituo cha televisheni cha ITV, huku akionesha dhahiri kujibu maoni ya vigogo kama Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta na wadau mbalimbali, waliolalamikia muundo wa serikali tatu wakidai kwamba ni gharama kuuendesha.
“Huwezi kung’ang’ania gharama, ulazimishe kwa sababu watu wanaogopa gharama, kuna hatari ya muungano kuvunjika, ni lazima uangalie watu wanataka nini na ndicho ambacho tumefanya kwamba kama tukilazimisha serikali mbili, kuna hatari ya muungano kuvunjika.
“Zanzibar wanataka madaraka yao, uchumi wao waumiliki wao wenyewe na ndiyo mabadiliko waliyokuwa wanataka. Bara wanasema kama Zanzibar wanataka hayo itakuwa imekuwa huru, utawafanya nini, huwezi kufanya mabadiliko? Kwahiyo mimi naona ukifanya hivyo hatari ya kuvunjika ni kubwa zaidi, sasa uone kama unataka muungano gharama zitakuwapo kwani hata tulipoanza gharama zilikuwapo.
“Sasa tumefika hapa tunasema ni afadhali tuwe na serikali tatu lakini tujitahidi kupunguza matumizi. Tunavyoona ni afadhali tuwe na serikali tatu…mi nitakuwa mnyonge sana muungano ukiwa dhaifu,” alisema Jaji Warioba.
Alieleza kwamba ikiwa wananchi wanataka kukwepa gharama muungano uvunjwe, lakini ikiwa wanautaka ni bora gharama ziwepo na kusisitiza kwamba aonavyo yeye ni muhimu zaidi nchi hizo kuwa pamoja kuliko vinginevyo, kwani hali hiyo inasaidia kupunguza gharama kuliko nchi hizo zikiachana, kwani gharama zitakuwa kubwa.
Alisema katika kukusanya maoni yao wamepata mambo mengi muhimu ambayo pengine hata wananchi hawayazungumzi, akatolea mfano suala la maadili ya viongozi.
“Tulipopita tulisikia watu wakisema kuhusu maadili, matatizo mengi yapo hata ya wananchi kutokuwa na imani. Walizungumza wakitaka hatua zichukuliwe.
“Na matatizo mengine yanayotokea ni kwa sababu ya maadili ya viongozi kuporomoka,” alisema Jaji Warioba.
Muundo wa serikali tatu kukopa
Kuhusu suala hilo Jaji Warioba alisema atakayekuwa na jukumu la kukopa kwenye muundo huo ni Serikali ya Muungano.
Alisema hata serikali hizo mbili zikija zitaweza kukopa kwani hata hivi sasa utaratibu huo upo.
“Lakini hata sasa hivi kuna utaratibu kuwa serikali zote wanakopa lakini serikali zote zitakuwa na nafasi yake kwenye kukopa,” alisema Jaji Warioba.
Kuhusu mpaka wa mkopo kwa nchi, mwenyekiti wa tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba alisema inategemea na serikali yenyewe kwani hata hivi sasa utaratibu huo upo na ikiwa serikali ya Zanzibar inataka kukopa hudhaminiwa na Serikali ya Muungano.
Kukwepa kutaja Serikali ya Tanganyika
Kuhusu kukwepa kusema Serikali ya Tanganyika, Jaji Warioba alisema walikuwa wanatengeneza Katiba ya Muungano ambayo inafahamika kuwa ni Tanzania Bara na Zanzibar.
Alieleza kuwa kwa Katiba ijayo ikiwa suala hilo litawekwa, Zanzibar wanaweza kuchagua majina yao bila kuingiliwa, kwani halikuwa jukumu lao kuwachagulia.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, ikiwa Tanzania Bara watakapotunga katiba yao watataka jina libaki Tanganyika, itakuwa juu yao, lakini kwa Katiba ya sasa inahusu Tanzania Bara na Zanzibar.
Bunge la Katiba Novemba
Kuhusu Bunge la Katiba, Warioba alisema litakaa baada ya tume yake kukamilisha rasimu ya pili ya Katiba ambayo itatokana na mapendekezo ya wananchi.
Alisema wanatarajia kuikamilisha kazi hiyo mwishoni mwa Septemba mwaka huu.
“Mawazo yao yatarudi kwetu na tutaangalia kama kuna umuhimu wa kubadili popote au kuacha kama ilivyokuwa ili kutengeneza rasimu ya mwisho.
“Utaratibu wa kisheria ambao umewekwa tunatakiwa tumalize kazi yetu mwisho wa Oktoba ili Novemba Bunge la Katiba likutane,” alisema Jaji Warioba.
Alieleza matarajio ni kwamba mwishoni mwa Septemba watakuwa wamekamilisha rasimu ya pili ambayo pia wataitangaza na baada ya mwezi mmoja, Bunge la Katiba litakutana.
Pamoja na mambo mengine alisema iwapo katika mapendekezo ya wadau wataona kuna jambo zito wanaweza kuliingiza watafanya hivyo lakini mpaka waliridhie kwamba suala hilo ni bora zaidi.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, sheria inaelekeza kwamba baada ya kuiandaa rasimu waitangaze kwenye gazeti la serikali na umma kisha iende kuzungumzwa na wananchi kwenye mabaraza yao pamoja na makundi mbalimbali.
Bonyeza Zaidi
swahilivilla: CCM wapinga serikali tatu
Chanzo: Tanzanian Daima
 
Serikali tatu ni mzigo kwe2 wananchi mm binafsi napendekeza serikali mbili kwanza 2vunje muungano then 2ingie muungano wa mkataba kila nchi iwe na mamlaka yake binafsi.
 
CCM hawana hoja yenye mashiko, kuwafata wanachama wake watoe maon upya ni ujinga yaliyotolewa na watanzania hawayakubali? Au anafikir vyama kama SAU,TADEA,CUF,N.K Vinaweza kuzunguka TZ nzima kuchukua maon ya wanachama wao? vp kuhusu wasio na vyama? wanadai hawatachakachua majib taasis nying zinajulikana final decision huwa juu,vp tuwaamin,nawashaur washawish wanachama wao kutoa maon yao kwa tume si taasis ya ccm, kikwete & nape jiulizen tena matamko yenu yana walakin.
 
Siasa bwana, watu siku hizi wamefumbuka macho thanks to CHADEMA. Huyu dogo angesema sababu za wao kupendelea Muungano wa serikali mbili and NOT tatu au moja, ili watu waweze kutoa maoni yao pia.Waache kulazimisha watu kukubaliana na mawazo ya watu wachache wanaofaidka na serikali mbili, maana katika CCM pia kuna watu wanataka muungano wa serikali moja au tatu. Muungano wa serikali mbili ni senseless.
 
CCM inatambua kwamba katiba ni ya wananchi ndiyo maana hujawahi kusikia CCM ikitishia kujitoa kwenye huu mchakato wa kuandaa katiba mpya.
Masisiem ni chama mfu hata kama ukichakachua hiyo comment ya kamanda hapo!!!jeikei pia analijua gamba ni janga la kitaifa!!!
 
kwani ni lazima maoni yote yaliyotolewa na CCM yawemo kwenye rasimu hii itakuwa katiba ya watanzania wote sio wana-CCM au chama kingine chochote
 
CCM kuweni na huruma na Wanzazibar jaman,wamemwaga sana damu kudai mamlaka yao huru kwnn mnataka kuendelee kuwakandamiza?au mnataka wajivike mabomu muwapige na propaganda za kidini ndo muamini?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Nijuavyo Wazanzibari wote ukijumlisha Shein, Bilali, Maalim, Karume, Mwinyi, mchana wanaimba kinafiki kutaka serikali mbili, usiku wanaungana na Maalim Seifu kumsakizia aendelee kudai Zanzibar "kujitawala". Lwa hali hii Zanzibar haikubali hata chembe Muungano wa serikali mbili. piga ua. Si mtaona.
 
Hakuna sehemu inayoonesha katiba ni ya CCM..kwa jins nilivyoelewa mimi hayo ni mawazo ya chama tu lakin kuna mchango pia wa wananchi na watakubaliana na maamuzi yatakayotolewa na wananchi..
 
CCM kuweni na huruma na Wanzazibar jaman,wamemwaga sana damu kudai mamlaka yao huru kwnn mnataka kuendelee kuwakandamiza?au mnataka wajivike mabomu muwapige na propaganda za kidini ndo muamini?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

sure! mi ki ukweli sioni sababu ya kuupigania huu muungano
 
haya ndiyo madhara ya kukurupuka nape kasema ni ya watanzani na wanairudisha kwa wananchi ikajadiliwe na watoe maoni yao.
NAPE hajasema wanairudisha kwa Wananchi KENG wewe na pia hana mamlaka hayo kwani sio kiongozi wa wananchi ni kiongozi wa wanaCCM, kasema anairudisha kwa wana CCM. Isitoshe kama hawataki serikali TATU ni wao kama CCM ambao idadi yao ni ndogo tu kulinganisha na Watanzania wengi. Kwa mujibu wa Warioba alisema kwamba zaidi ya asilimia 75 ya waliotoa maoni wamependekeza serikali TATU sasa kwa maelezo ya NAPE kurudi tena kwa wananchi kwa kipengele hicho hicho na kutoa mawazo yale yale tena wakati umeshaonesha kwa dhati kuwa serikali TATU hutaki unataka mfumo wako ambao tayari umeshautolea uamuzi tayari ni kama kuwaambia hao wana CCM kwenda kujipanga kupinga mapendekezo ya RASIMU ya serikali TATU na si kuboresha RASIMU.
 
Cha Kwanza Je Wananchi wanataka Muungano au hawataki?
 
Well, ni maoni yao hayo ila waelewe kuwa katiba inayoandaliwa ni ya watz wala siyo ya chama mfu hicho.
wananchama wote hai na wafu wa CCM hawafikii hata 15% ya wananchi wa Tanzania. Hayo ni mawazo yao lakini si msimamo wa wananchi.
 
Mkuu Highlander, this is well articulated! Rasimu hii ya katiba ni catch 22 kwa CCM, either it recants the theory of 2 govts or embrace the Draft proposals, either way it has disastrous consequences to CCM!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…