Nape Nnauye: Dkt. Slaa, Mdude na Wakili Mwabukusi wamekamatwa kwa kauli za Kutaka Serikali Ipinduliwe

Serikali ipi iliyochaguliwa kidemokrasia?
 
Nape kasahau kuwa nae na Mzoga gang walitakiwa wawekwe lupango kwa makosa haya haya ya uhaini dhidi ya awamu ya 5 hadi yeye akaenda kuomba msamaha akitembea na magoti pamoja na na wazee wake, ule ulikuwa ni uhaini uliopitiliza lakini jembe akawaacha tu na kumwachia Mungu, narudia tena Nape hana uhalali wa kutoa hizi porojo.
 
From kukosoa mkataba to "tuipindue hii serikali" watajilaumu wenyewe tu kwenye hili wamejichanganya wenyewe na kupelekea kumpa hasimu wa chance kuu
 
ili kuzuia machafuko ya kijamii yanayoweza kutokea kutokana na wito wa uasi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kamwe haiwezekani kuwaachia watu kama mzee silaha na huyo mwabukuzi wakipanga njama za kihaini na uchochezi wa kuvuruga amani ya nchi.

Sisi kama watanzania wapenda amani tunalaani vikali vitendo vyao wazee wenye lengo la kuchochea machafuko.

wachukuliwe hatua za kisheria kama wahalifu wengine.

Wametokana kutokana na kauli zao za kichochezi na kutaka kufanya uhaini, sio suala la kukosoa mkatataba wa Bandari.
 
Kwanini huyu waziri anamjibia waziri wa mambo ya ndani ambaye ndiye mwenye dhamana na polisi?

Leo huyu waziri amekuwa msemaji wa serikali badala ya yule aliyeko Ikulu?

Huyu ndiye aliyewatuma polisi kuwakamata akina Slaa, Mdude na Mwabhukusi kwa chuki binafsi na mgongano wa maslahi
 
Huyu waziri anatakiwa avuliwe cheo hicho kisha ashitakiwe maana ni mmojawapo ya watu walioshauri Slaa, Mwabhukusi na Mdude wakamatwe akibeba wito kutoka kwa spika. Waziri wa mambo ya ndani na wasaidizi wote kwenye wizara hiyo hawafai maana wananchi wanawalipa mishahara kuwanyanyasa haikubaliki.
 
Aisee NAPE Muogope MUNGU wako
 
Hata mimi kanishangaza sana huyu bwana mdogo ni kijana wa hovyo sana, unajua bado anataka kujifanya nae ni mtoto wa wenye nchi, anasahau kuwa haya yana mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…