Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema video inayosambaa ikimuonyesha akisema kuna mbinu nyingi za CCM kushinda uchaguzi ikiwamo zisizo halali imepotoshwa na hakuwa na maana iliyotafsiriwa na watu wengi.
Kauli ya Nape kuhusu bao la mkono soma: Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono
“Nimeona mjadala wa video hii. inapotoshwa kwa kukata vipande watakavyo wapotoshaji. Msingi wa mjadala huu ulikuwa utani wa hoja ya zamani ya “goli la mkono”.. uliorushwa wakati naongea ndio maana kuna kicheko kabla. Haikuwa serious version. Mimi muumini wa uchaguzi huru na haki. Vizuri tuendelee kushindana kwa hoja,”ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X leo Jumanne Julai 16, 2024.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Nape: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Nape ameibuka kuelezea hoja hiyo ikiwa ni saa chache tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla leo, aseme kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho.
“Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” amesema.
Pia soma: CCM wapinga kauli ya Nape Nnauye kuhusu imani yake kwenye ushindi wa chaguzi nchini, wasema CCM haihitaji mbeleko
Nape alitoa kauli hiyo jana Julai 15, 2024 usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi na kauli hiyo ililenga kumhakikishia ushindi wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.