Nape Nnauye kuhusu Bunge Live: Wabunge wakipigana haileti picha nzuri

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhusu bunge live, anafafanua:

"Spika wa Bunge, Tulia Ackson alisema hili jambo linazungumzika na tutajadiliana na Serikali tuone namna ya kulifanya liende.

“Studio ya bunge ndiyo inaamua warushe vipi matangazo najua kwa mfano nchi ya Afrika ya Kusini wana'delay' fulani yaani kwamba wanarusha live bunge lakini kuna 'delay' ya dakika 15 au nusu saa hako ka 'delay' kanawapa room wabunge waone kama katafaa kwenda hewani.

“Kwa mfano ikatokea wabunge wanarushiana maneno machafu bungeni na tumeona baadhi ya wabunge ya wenzetu wanapigana sasa vitu kama vile havipeleki sura nzuri.

“Kupeleka dakika 15 au nusu saa siyo mbaya lakini isipitilize na kuwe na utaratibu kwamba kama kuna jambo fulani la kujadili na wabunge wakaona linafaa tu kujadiliwa ndani.

“Suhuhisho ni kanuni ya kuendesha studio ya bunge ambayo ni kazi ya bunge."
 
KWANI HAYO MABUNGE AMBAYO WABUNGE WAKE WANAPIGANA TUNAWAZIDI AKILI, UCHUMI AMA SIASA?
 
Kwamba hatuna haki ya kuona wawakilishi wetu wakipigana kwa sababu wao ni waheshimiwa na malaika?...

Kwa hiyo ni haki kwao kufanya mambo yasiyofaa kizani na yanayofaa mwangani?

Sijui watu wakipata madaraka wanakuwaje!
 
Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhusu bunge live, anafafanua:

"Spika wa Bunge, Tulia Ackson alisema hili jambo linazungumzika na tutajadiliana na Serikali tuone namna ya kulifanya liende.

“Studio ya bunge ndiyo inaamua warushe vipi matangazo najua kwa mfano nchi ya Afrika ya Kusini wana'delay' fulani yaani kwamba wanarusha live bunge lakini kuna 'delay' ya dakika 15 au nusu saa hako ka 'delay' kanawapa room wabunge waone kama katafaa kwenda hewani.

“Kwa mfano ikatokea wabunge wanarushiana maneno machafu bungeni na tumeona baadhi ya wabunge ya wenzetu wanapigana sasa vitu kama vile havipeleki sura nzuri.

“Kupeleka dakika 15 au nusu saa siyo mbaya lakini isipitilize na kuwe na utaratibu kwamba kama kuna jambo fulani la kujadili na wabunge wakaona linafaa tu kujadiliwa ndani.

“Suhuhisho ni kanuni ya kuendesha studio ya bunge ambayo ni kazi ya bunge."
Na nchi ambazo walipigana zimepata gani? Hii nchi ni yetu wote, wabunge mna Siri gani? Kama mijadala kama ya Richmond ilipita bungeni ikiwa live,kitu gani kiliharibika? Wewe Nape umekuwa mbunge 2015 ndo ukazima na bunge,kwa ungeanza 2005 mijadala kama ya Richmond na mingine km escrow tusingeona? Athari ni zipi kwa wananchi tulioyaona hayo!!!
 
Hivi kuna watu wenye hamu ya kuangalia bunge la sasa kweli?
Move za kituruki na kihindi hakuna?
 
kinacho jadiliwa hakina umuhimu kwa wananchi zaidi ya kutetea matumbo yao tu,hivyo watajua wenyewe warushe au wasirushe
 
Back
Top Bottom