Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Serikali kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye imesema, inakusudia kuvifanya vyombo vya habari nchini kufanya kazi kwa uhuru na kwamba, haitaviingilia kwenye uhuru wao.
Waziri Nape amesema, Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari yaliowasilishwa bungeni tarehe 10 Februari 2023, yanalenga kuimarisha uhuru wa kujieleza nchini.
“Serikali itasimamia na kulinda uhuru wa kujieleza Itahakikisha inafanya kila linalowezekana kulinda haki hiyo"
Chanzo: EATV