Nape Nnauye: Warioba haitendei CCM haki.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi (Nec-CCM), Nape Nnauye, ametuhumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haitendi haki kwa kuwazuia wajumbe wa Baraza la Katiba kusoma waraka wa chama hicho unaopinga baadhi ya mambo yaliyopo kwenye rasimu.

Nape alitoa shutuma hizo jana alipozungumza kwa njia ya simu, alibainisha kuwa viongozi wa Jukwaa la Katiba akiwamo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, wanataka mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu yapite yalivyo.

"Kwani kufanya hivyo wanazuia maoni ya wananchi, ingawa hatujawatuma kuusoma kwenye mapendekezo, lakini wana haki ya kuutumia wanavyojisikia," alisema Nape.

Alisema wanajua wapo watu wachache wanaoupinga waraka huo wa CCM, lakini hawaelewi kwa sababu unahusu wanachama wao.

"Tume itende haki isikilize mawazo ya kila mtu, inachofanya sasa ni ubaguzi, wao wanatakiwa kusikiliza maoni siyo kutetea rasimu," alisema.

Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti jinsi Jaji Warioba alivyokosoa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wanaokwenda na matamko au nyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua.

MWANANCHI GAZETI
 
Duuuuu ndo xaxa Nnape ameibuka toka mafichoni, kwanini wanawakririsha wadau makapi yao ili wakayateme kwa jaji warioba badala ya kuwaacha wayaseme ya kwao ya moyoni kama walivyopanga , jaji warioba yuko sawa kuwapiga biti watu wanokuja kutusomea nyaraka za kigamba gamba kwani ni sawa na kuivalisha gamba katiba mpya ijayo.
 
Warioba na tume yake kiukweli inabidi itege sikio lake kwa umakini.
Kuna maoni mengi hayakuingizwa kwenye rasimu hii iliyoandaliwa.
Mchakato bado sana
 
mtu akikidharau kila unalo ongea jua kaisha kuchoka kabisa, lakini kwa kukuheshimu hakwambii, wakati wa CCM umeisha miaka 20, ilitosha kabisa kutuonesha dira ya uhakika ya kimaendeleo lakini siku zinazidi kwenda ni watu kung'olewa meno na uchafu mwingi tu, sasa wapumzike wapishe na webgine, kwa nza hata hiii swala la kuandika katiba mpya ili pita kwa mbinde...
 
Hivi, si kuna muda wa tume kuonana na vyama..??? Kama upo, kwa nini CCM wahangaike hivyo..??? Yaani zamu ya wananchi, wazungumzie chama, halafu ukifika muda wa chama, wazungumzie chama, kwani wanaunda katiba ya chama? CCM mnatia aibu, nyie ni chama kikongwe.... Yaani kila kundi fulani linapokutana na tume basi waraka wenu usomwe......
 
Mimi nilifikiri katiba mpya ni kwa ajili ya maslahi ya nchi??

Kumbe kuna watu wanapigania maslahi ya chama. Kwa mtaji huu Watanzania bado sana!!
 
Kila taasisi Kila mwananchi Kila mdau katika nchi hii anahaki ya kutoa maoni yake na yasikulizwe, siyoo taasisi fulani ilazimishe mawazo yake yawe ndo ya Kila mmoja. Nape acheni hizo.
 

mwanachikurasa wa ngapi mkuupo na wananchi apa usitufanye watoto
 
kutoa maoni haki ya kila mtu na kila chombo na kila tasisi hakuna mtu kuziwa mdomo,
 
Sasa hoja zimeshaandikwa na tume, unataka zirudiwe kusomwa-somwa na kila mchangiaji na kuacha kusikiliza hoja za wengine tena ambazo ni huru sio za kukaririshwa na Wasira the old donkey.
Nape Nnauye kichwa chako kimekariri utawala wa ki-imla unadhani kila mtu ni 'mjumbe ndiyo' kama wale wa miaka ya 47.

Meli ya CCM imezama nusu, maji yamemfika Nape Nnauye usawa wa shingoni, hachomoki anakufa na meli yao iliyochoka mno.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Nape we utakuwa mtoto wa nje ya ndoa maana huishi kulalama!
 
Last edited by a moderator:
Nape ni mjinga wa karne! Mzee Warioba anajua hila zenu kama za nyoka
 
Wananchi nchi kwanza maslahi ya vyama yatafuata baada ya kupatikana katiba mpya
 
ili hali anatenda haki kwa watanzania basi huyu Warioba ni shujaa , jemedari na mzalendo halisi....



ccm inaangamia, ccm inakufa, ccm tayari ipo icu
 
Namuunga mkono Warioba na tume yake. Taasisi mbali mbali zina nafasi ya kutoa maoni yao katika Tume. CCM kutaka maoni yao yasome katika mabaraza ya raia ni mbinu ya kutaka kuonyesha kwamba watu wengi wana maoni kama ya CCM! CCM is using wananchi as surrogates and that can't be acceptable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…