Nape: Rasilimali za nchi kutumika vibaya ni kwasababu wanahabari wamefumba macho

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Waziri wa habari, Nape Nnauye akizungumza kwenye kongamano la habari leo, tar. 17, 12, 2022 lenye kauli mbiu isemayo, habari kwa maendeleo endelevu.

Nape amesema, rasilimali za Taifa kutumika vibaya ni kwasababu wanahabari wamefumba macho, hawatumii kalamu zao kuibua ubadhilifu.

Amesema wanahabari wakitumia kalamu zao vyema nchi itapata maendeleo kwa kuwa kila rasilimali itatumika vyema kwa maendeleo ya nchi.

Amewaasa wanahabari kutumia kalamu zao kusaidia nchi kupata maendeleo kwa kuandika habari zenye tija, na kufichua maovu yaliyofichika katika matimizi ya rasilimali za nchi.
 
Watu wamendika Sana kuhusu hujuma za mitandao ya Simu lakn mkuu hajatoa maamuzi ambayo wananchi wakaona kweli Waziri usiku amechukua hatua.

Angetakiwa Kwanza atuonyeshe mfano yeye binafsi kwanza
 
Maendeleo yanaanza na wizara yake, Bando zimekuwa ni anasa wakati ni sehemu ya kupashana habari!

Unapomwibia mwananchi Kwa kuweka bei za juu kwenye bando, nchi na wananchi watapata maendeleo karine ipi, upuuzi tu
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye akizungumza kwenye kongamano la habari leo, tar. 17, 12, 2022 lenye kauli mbiu isemayo, habari kwa maendeleo endelevu.

Nape amesema, rasilimali za Taifa kutumika vibaya ni kwasababu wanahabari wamefumba macho, hawatumii kalamu zao kuibua ubadhilifu.

Amesema wanahabari wakitumia kalamu zao vyema nchi itapata maendeleo kwa kuwa kila rasilimali itatumika vyema kwa maendeleo ya nchi.

Amewaasa wanahabari kutumia kalamu zao kusaidia nchi kupata maendeleo kwa kuandika habari zenye tija, na kufichua maovu yaliyofichika katika matimizi ya rasilimali za nchi.
Sio Takukuru, polisi na usalama wa taifa tena bali ni Wanahabari?🤣🤣🤣
 
Kama Taifa tunahitaji revolution na reshuffling!! Chumba cha pili nao wamenivuruga huku, bora niamke zang!!!
 
Attachments

  • 1644504011928.jpg
    1644504011928.jpg
    28.3 KB · Views: 4
Wafichue mnayojadili sirini na kuyalinda kwa nguvu na vitisho
 
Sio Takukuru, polisi na usalama wa taifa tena bali ni Wanahabari?🤣🤣🤣
Wanahabari wana sehemu yao katika kufichua maovu. Wakiandika uovu unaotendeka hao uliowataja watauona na kuchukua hatua.
 
Ameanza kubadili ulimi Baada ya MATOKEO yale!

Ameona wenye nguvu ndani ya Chama ni nasaba ya mzee aliesingizia kuwa Mungu aliamua ugomvi nae!

Muda sio mrefu ataitwa sukumagang!

Asante wajumbe!
 
hili jamaa uwa ni jinga sana, waliokwapua mamilioni BOT wakati wa kifo cha Magufuli na kuundiwa tume na samia,mbona hamjawataja? samia anawafahamu yeye anawafahamu mbona hajawataja. pure idiot
 
Huwezi pata waandishi wenye weledi na wakati huo huo tasnia ya habari ina changamoto lukuki ambazo zimekuwa Kama puzzle kwa muda mrefu na serikali ikiwa miongoni mwa matatizo katika media industry nitaeleza machache tu

*Sheria sio rafiki kwenye media industry mfano ni Media Service Act 2016 licha kwamba sheria hii imefanya ubainifu wa Journalism as professional bado Kuna matatizo ndani ya sheria hii makubwa na isha lalamikiwa sana lakini serikali haija fanya lolote kubadilisha vifungu tata.

*Maadili ya waandishi hili limekuwa suala mtambuka kwenye tasnia ya habari maana waandishi wengi wamekuwa na harakati za kutaka teuzi na wengine kuonesha mahaba yao kwa vyama vya siasa mfano ulio wazi ni mkutano wa CCM ulio pita umefungua uozo ndani ya tasnia ya habari

*Haki ya matangazo serikali ndo mtangazaji mkuu na chanzo Cha mapato kwenye media ni matangazo hivyo vyombo vya habari vinaimba mapambio tu kwa serikali na sio kufanya kazi ya kuhabarisha umma lengo ni kupata matangazo.

*Mauaji,kesi na kupotea kwa waandishi wa habari bado ni kitendawili kizito kwenye tasnia ya habari bado tasnia ya habari haija sahau kilicho tokea kwa Mwandishi wa channel ten David Mwangosi na Azory gwanda wa mwananchi communication limited (investigative Journalist),yaliyo mkuta Saimon Kabendera sote tu mashaidi bila kusahau kifo Cha utata Cha Stan katabalamo.

*Ndani ya tasnia ya habari kuna viwavijeshi wasio jua lolote kuhusu uandishi(Journalism) na maadil yake (Ethics of Journalism) Wana amini kuwa uandishi ni talent kumbe uandishi ni taalumu (professionalism) Kama ilivyo ualimu,sheria nk hivi mtu Kama Baba levo ,Mwijaku nk wanajua nini kuhusu uandishi wa habari zaidi ya kuleta uchawa kwenye media na habari za udaku (Yellow News)

Niishie hapa GT wataongeza madini zaidi

"Deni la taifa ni odious debt"
 
Nakazia hapo mkuu
 
Anachokisema Nape kinatoka kwenye moyo wake? Leo akijitokeza mwanahabari akaleta habari ya uchunguzi inayogusa rafiki zake ataliacha hilo gazeti?

Wanasiasa husema hiki na kumaanisha kile.
 
Back
Top Bottom