Nape refutes Mnyika; TBC takes debate off air


- Nape, amesema alichosema ni kwamba chama cha siasa kinatakiwa kuwa na Social Contract na wapiga kura, yaani wananchi yeye akiita ni ilani mkuu wapi hujaelewa hapo? Soma hapa chini alichosema Nape:-

Na nikaendelea kwa kusema, na huu ndio mtazamo wangu juu ya hili, nafahamu kuna contracts za aina nyingi sana, katika siasa kuna kitu tunaita Social contract. Ilani ya uchaguzi inafaa kuwa social contract kati ya Chama cha siasa na mpiga kura...

Respect.


FMEs!
 
- Nape, amsema alichosema ni kwamba chama cha siasa kinatakiwa kuwa na Social Contract na wapiga kura, yaani wananchi yeye akiita ni ilani mkuu wapi hujaelewa hapo?

Respect.


FMEs!

Hilo si jibu la swali alilouliza Serayamajimbo.

Jibu analo Nape ana anaweza kuanza kwa kusema "Ndiyo ni muongo" au "Si muongo" kwa sababau hii na ile.

Anayezungumziwa hapa kwenye kisehemu hiki ni Mnyika, iweje utake kutosheleza jibu kwa maneno ya Nape?
 
Hilo si jibu la swali alilouliza Serayamajimbo.

Jibu analo Nape ana anaweza kuanza kwa kusema "Ndiyo ni muongo" au "Si muongo" kwa sababau hii na ile.





Nape

Kwa jibu lako unaama kwamba John Mnyika ametudanya hapa? Maana yeye amethibisha hapa kuwa ulisema kwamba kwenye siasa hakuna mkataba(contract).



Kwa hili hatuhitaji mate maana wino upo hapa hapa!


FMEs!
 
Unafahamu tofauti ya social contract na legally binding contract? Mbona humwachi mwenyewe ajibu?
Kwakuwa sijalala bado, Kiranga unataka nijibu nini? Ni kipi sijajibu? Kipindi kinarudiwa kesho mchana sikumbuki saa ngapi......
 

Kwa hili hatuhitaji mate maana wino upo hapa hapa!


FMEs!

Sehemu nyingine zote Nape amejitahidi kurekebisha misrepresentation iloyoletwa hapa kuhusu maneno yake katika debate ile, na alipata endorsement ya Mnyika; jambo hilo limefanya mjadala huu kuwa wa kuvutia na wenye mantiki sana. Hata hivyo kwenye hiyo point ya contract bado Nape na Mnyika wanapishana. Ni vizuri sana wainyooshe, kwa sababu nadhani ndiyo iliyoibua explosion ya mjadala huu na kuvuta hata wale waliokuwa pembeni.
 
naona kuna bromance kati ya Nape na Mnyika.Ubungo haigawiki ile lakini.

Swali lilikuwa huyo Mnyika aliyesema kwamba wewe umesema hakuna contract kadanganya?
 
Unafahamu tofauti ya social contract na legally binding contract? Mbona humwachi mwenyewe ajibu?

- Maelezo ya Nape, nimeyaelewa kama ni Social Contract ya wanasiasa ninaikumbuka sana ile ya kina Gingrichna Republicans, sasa sielewi, legal binding contract inatafuta nini kwenye siasa,

- Labda unieleweshe mkuu unaongelea nini maana sioni kuhusika kwa legal binding contract na siasa, au?

es!
 
naona kuna bromance kati ya Nape na Mnyika.Ubungo haigawiki ile lakini.

Swali lilikuwa huyo Mnyika aliyesema kwamba wewe umesema hakuna contract kadanganya?

Nakushauri kesho mchana kama upo bongo angalia kipindi toka mwanzo mpaka mwisho,kama haupo Bongo watakaoangalia wataeleza hapa.
 
Nakushauri kesho mchana kama upo bongo angalia kipindi toka mwanzo mpaka mwisho,kama haupo Bongo watakaoangalia wataeleza hapa.

Hujaweza kunisaidia.

Sipo bongo na nilitaka kusikia "from the horse's mouth" .
 
Nakushauri kesho mchana kama upo bongo angalia kipindi toka mwanzo mpaka mwisho,kama haupo Bongo watakaoangalia wataeleza hapa.

- Mkuu umesikika tutasubiri kesho, tukishaiona ndio tutakwua na maswali, si upo anyways, hakuna haraka sana, otherwise ahsante sana kwa kujitolea kuja kutoa maelezo hapa wewe na mwenzako Mnyika, saafi sana tunataka vijana wa aina hii yenu katika uongozi!

Respect.


FMEs!
 

Sasa mbona unamfanya kama Mariah CArey aliyekunywa one too many unamkimbiza off stage?

Mwanasiasa anaogopa challenge ya kwenda toe to toe na wananchi anawaambia wasubiri kipindi wakati yeye yupo hapa?
 
- Too low kwangu kujibu hii! Otherwise nitasubiri kesho nione kwanza hiyo shoo kama alivyoshauri mwenyewe, saa hizi bongo ni suiku sana kesho kuna kazi, ndio maana nimemuelewa Nape na Mnyika pia.

es!
 
Mkuu, ni kweli kuwa katika siasa za Tanzania, hakuna mkataba wowote kati ya wapiga kura na wanasiasa. Ni jambo la kusikitisha na ambalo halimpendezi yeyote. Nadhani ndio maana Nape anaonekana bogus, kama ulivyosema hapo juu. Wabunge na Rais wa Jamhuri wanaapa kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa kwenye Katiba ya nchi, na wala sio kama walivyoahidi kwa wananchi. Na huo ndio mkataba walionao. Wakikiuka mkataba huo, mkataba unaweza kuwa terminated. Hakuna mwanasiasa wa Tanzania anaeweza kutekeleza majukumu yake kikatiba akawa amekiuka mkataba alionao kwa Taifa. Nadhani pia, ndio maana Nape alisema alichokisema.

Kwa upande mwingine, nadhani Nape hakutakiwa kuusema ukweli huo kwa kipindi hiki na kwa watu kama sisi ambao hatupendi kuusikia ukweli kama huo. Watanzania wengi wanapenda kusikia yale wanayotaka kuyasikia tu.
 
Ndugu zangu habarindiyohiyo ana haja ya kutiliwa shaka.

Nape amesema haku M-refute Mnyika na wote wamesema hapa kuwa waliweka
maslahi ya taifa mbele zaidi ya chama.

Huyu bwana ye katulia kimyaaaa......kazi ipo.
 

Kugombea uchaguzi ni sawa kabisa na ku-bid kwenye tender. Wapiga kura wanachokifanya ni ku-evaluate na kuchagua bidder anaefaa. Katika kuchagua hakuna contract. Contract inakuwepo baada ya bidder kuwa selected na kuapa kutekeleza majukumu yake kama anavyotakiwa. Na katika hili, mkataba pekee ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nothing more.

Haiwezekani kukawa na contract moja kati ya wananchi na bidders wengi (kabla ya selection/election). Kama hivyo sivyo, je wale wanaokuwa wamepata kura chache (na kushindwa uchaguzi) nao wanakuwa na mkataba na waliowapa kura zao? Maana mshindi wa uchaguzi hatakuwa na la kuwatekelezea wale ambao hawakumchagua. Ama sio?
 
Muda wa Marudio ya Kipindi imekuwa siri, nahisi kuna kitu kinafichwa hapa ngoja niusakanye nikiupata nauweka hapa ili kila mtu aone na tuache kujadili speculations
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…