Nape: Tumewaagiza TCRA wachunguze wale wanaodhalilisha watu waliowakopesha Mtandaoni

Nape: Tumewaagiza TCRA wachunguze wale wanaodhalilisha watu waliowakopesha Mtandaoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye amesema Serikali imetoa maeleko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwafuatilia na kuchunguza Watu wanaotumia taarifa za waliowakopesha Mtandaoni kwa lengo la kudhalilisha wakopaji.

Amesema maelekezo hayo pia yanahusisha Kitengo cha Cyber Crime Unit ili kujua wahusika wanapata wapi namba wanazotumia kusmabaza ujumbe baada ya kushindwa kulipana kwa kuwa ni kinyume cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Nape amesema hayo Bungeni, leo Juni 27, 2024.

Pia soma:
 
BUNGENI: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye, amesema Serikali imeshatoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kitengo cha Cyber Crime Unit kuwafuatilia na kuchunguza Watu wanaotumia taarifa za waliowakopesha Mtandaoni kwa lengo la kudhalilisha Wakopaji

Ameyasema hayo Bungeni leo Juni 27, 2024 , ili kujua wahusika wanapata wapi namba wanazotumia kusambaza ujumbe baada ya kushindwa kulipana kwa kuwa ni kinyume cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi
 
Nape Toka azaliwe Leo ndio kaongea mambo ya msingi
pole gentleman kwa kadhia,

jamaa sio wangwana kabisa kwenye hili pamoja na kwamba huenda wanawasitiri watu na fedheha mbalimlali za kimaisha ila udhalilishaji wao sio mzuri, hadi mama mkwe wanamjulisha eti mnanadaiana?:pedroP:
 
Kutoa maagizo ni jambo moja na utekelezaji ni jambo jingine. Tusubiri tuone, maana viongozi wetu kwa kutoa "maagizo" hawajambo.
 
Hao jamaa wanajiona wako juu ya sheria.Haiwezekani wanaanza kudai pesa siku ya tano ya deni wakati deni katika APP yao ni siku saba ukianza kuwaelekeza waangalie APP yao wanakukatiza na kuanza kukutisha eti utalipiwa na na baba yako mama yako dada zako we subiri tu.
 
Nchi ina vituko hii majambazi na wahuni wengine mpaka hao TCRA watumwe na Waziri ndio wafanye kazi...tusubiri siku ingine wakitumwa kwa wale wa tuma hela kwenye namba hii..
 
Nikweli kabisa hii mikopo kama vp iondoeni kabisa maana wanatudhalilisha kwanza hawajui mtu kukwama kuchelewesha saa moja au mbili wanaanza kukudhalilisha
 
Ukifanya yafuatayo inapunguza kero.
1. Futa app(Scammer app). Hutumika kufuatilia taarifa zako za mawasiliano na text messages zinazoingia pamoja na Gallery.
2. Line uliyokopea hamishia kwenye kiswaswadu.
3. Lipa deni
Note.
Ukikopa online kwa kuwa wanachukua IMEI na wewe unakuwa na App yao, basi control and privacy ya simu yako unaikosa. Wanakuwa na uwezo wa ku access vitu vingi vya siri kwenye simu yako. Kiufupi unakuwa uchi
 
1719556238530.jpeg
 
Back
Top Bottom