Nape: Wanahabari, kama Mwanasiasa akitoa lugha ya matusi jukwaani achana naye usiripoti taarifa yake

Nape: Wanahabari, kama Mwanasiasa akitoa lugha ya matusi jukwaani achana naye usiripoti taarifa yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumzia uamuzi wa Rais Samia Suluhu kuruhusu mikutano ya siasa ya vyama, ambapo amewatahadharisha Wanahabari juu ya mikutano hiyo.

Nape amesema “Rais amefungulia mikutano ya hadhara, ni matumaini yangu Wanahabari wa Tanzania watabalansi stori za mikutano hiyo, kwani tukibeba hivihivi tutawapeleka watu kusiko.

“Na siyo tu kubalansi, wakati mwingine una sababu gani ya kuchapisha matusi, mwache atoe matusi wewe ondoka zako.

“Usirekodi kila kitu, siyo kila kitu ni stori, wito wangu kwa Wanahabari uhuru uliotolewa utumike vizuri, kama ni kukosoa tukosoe kwa ukweli ili tujenge Nchi.

“Uhuru lengo lake ni kutusaidia kuwa macho katika kuhakikisha kwamba rasilimali za Nchi yetu zinawanufaisha walio wengi, hili linaweza kufanywa na Wanahabari, tusaidieni.”
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumzia uamuzi wa Rais Samia Suluhu kuruhusu mikutano ya siasa ya vyama, ambapo amewatahadharisha Wanahabari juu ya mikutano hiyo...
Hii inawezekana wapi kwenye dunia hii ambapo kila mtu ni mwandishi; dunia hii ambamo NAPE na wenzake walidukuliwa wakimsema marehemu JPM na dunia ikapata habari kesho yake; dunia hii ambamo mtu anavua ngua anajirekodi na kusambaza utupu wake. NAPE unajidanganya fanya mengine
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumzia uamuzi wa Rais Samia Suluhu kuruhusu mikutano ya siasa ya vyama, ambapo amewatahadharisha Wanahabari juu ya mikutano hiyo...
Huyu huyu si ndiye aliyemuita Mgombea Maiti. Akadai hawataki kupeleka Maiti Magogoni. Au hilo kwake siyo tusi!!

Kwa ubongo wa kuku tayari kesha sahau hilo, leo anajifanya msitrabu. Ngoja tuone 2025 atakuja na matusi gani!!?
 
Akae kwa kutulia aache kuweweseka,kama ni tusi litarekodiwa kama lilivyo,kama sheria itakuwa imevunjwa waende mahakamani.
 
Nape akiwa iringa soko kuu kwenye mkutano wa hadhara enzi akiwa mwenezi 2010 au 2011 alipata kusema “ CCM ni sawa na nywele za kichwani kwani zinaonekana na kila mtu na wapinzani ni sawa na nywele za kwapa na mavuzi ndio maana hawaonekani na hawapendwi na wananchi maana hawaonekani “ sasa nape alitukana au alitoa hoja?
 
Angetoa orodha ya matusi ili wajue kipi cha kuongea na kuacha, asimame katika kushauri na si kuwapangia cha kuongea.

Unataka vita kisha unamchagulia pa kukupiga mpinzani wako uzuri hakuna mtoto Kati Yao asiye weza pima maneno pindi awapo kwenye ulingo wa siasa labda azidiwe na jazba. Tambueni hii nchi yetu wote.
 
Ameshaanza kuweweseka na kuwachagulia watu cha kuongea na kuandika...
 
Back
Top Bottom