Napenda iwe hivi

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
Ba ndugu siku hizi vijana wengi tumekuwa tukikwepa kufunga harusi na si ndoa hii inatokana eidha na swala zima la kiuchumi au kijitia kitanzi mtu anaamua kubeba kifaa kimya kimya bila kushirikisha ndugu, jamaa na marafiki.
Wengi wetu kikubwa kinacho tusuta ni ile hali ya kufunga harusi ya kifahari magari msululu mrefu kama wa Mh. Pinda anaenda kufungua mradi.
Mi napenda harusi inakuwa simple tu vikao vichache na michango kiduchu tusije baadae tukashikana masharti ooh nimetoa laki 3 nimekunywa bia 2 tu.
Harusi kama hii hapa naipenda sana kwa kweli.


Yaani simple hakuna cha ukumbi sijui MC sijui nani gharama za nini wakuu? Hizi garama kwa nini msipeleke misaada mashuleni watoto wetu wasome ili wawe na maisha bora. Au kwa nini msipeleke kusaidia magereza au kusaidia watoto yatima yanini ufanye harusi ya kufuru kwani kuna kitu cha ajabu? Wewe uliyefanyia sherehe za harusi Kempsiky na mimi niliye fanyia sherehe kwenye open space kuna tofauti gani na usikute ya kwangu itadumu na kudumu kuliko yako.
Napenda sana maisha simple.
Baada ya harusi ukichukua usafiri wako wa border to border mnaenda zenu coco beach kula upepo kuna ubaya wowote? check hapa simple tu na mywife katikati mshikaki maisha mapya yanakuja.


Yaani simple na mpambe wangu nyuma nyie wa kisasa mnaita Bestman.
Napenda sana iwe hivi nikipata mwali jamani 2012 nawaalikeni nyote member wa JF mje msheherekee mimi sihitaji michango mikubwa ni kiduchu tu watu mnaenjoy.
 
Jamani kumbe mnapenda harusi za kujionyesha kuwa una uwezo.
Tujadili kwa nini harusi zinazo fungwa kwa mbwembwe nyingi iwa hazidumu?
 
harusi za mbwembwe mara nyingi huchangiwa na influences za watu wako wanaokuzunguka. mfano wewe mwenyewe utapenda ufanye simple, lakini wazazi wako wakakuambia walikua wanachangia miaka mingi kwa wengine sasa ni zamu yao kuchangiwa, so unajikuta huna jinsi.
la pili wakati mwengine wewe mwenyewe au mkeo anataka kuuza sura(kuosha), kwa wenzake!, sasa unategemea nini hapo?
 
pili wakati mwengine wewe mwenyewe au mkeo anataka kuuza sura(kuosha), kwa wenzake!, sasa unategemea nini hapo?

Yeah hiki ndicho wengi iwa wanakifanya wanataka kujionyesha mambo flani au maswala ya kulipiza.
 
Mi napenda iwe simpo,lakini wenye kupenda kuifanya babkubwa wasubiri kwanza nimalize yangu kisha kama watataka makuu basi waandae ili mimi na mke wangu tuende kama wageni waalikwa wale mahsusi kabisa,kama mjomba anavyoalikwa kwenda kufungua miradi. Hapo nadhani patakuwa sawa kwa upande wangu.
 
Wakuu shusheni nondo juu ya harusi hizi zinazofungwa kwa mbwembwe zinadumu kweli ndoa zao?
 
Hii ndo yenyewe mkuu!Ndoa ndoa tu!ukafungie kwenye ndege,au wapi!kikubwa ni maelewano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…