GTA
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 878
- 651
Habari za saa hizi wanajamvi we zangu.
Nilikuwa na wazo la kufungua biashara ya kuundumi wateja wanaoitaji pesa (Kutoa) na kuweka kwa upande wa mabenki yani NMB Wakala, CRDB Fahari Huduma na nk.
Ningependa kufahamishwa taratibu za kuanzisha au kujiunga n kuwa WAKALA. Pili mtaji wa shilling ngapi unaitajika.
Nawasilisha.

Kukusaidia.
Uwe na TIN na leseni ya biashara fulani. Uwe umeoperate kwa miaka 2 au zaidi. Accts statement za angalau miezi 6 iliyopita. Ualeta hata za MPESA, TIGOPESA n.k
Uwe sehemu nzuri kibiashara na kiusalama. Mfanyakazi angalau awe form 4 (japo sio lazima sana)
Nenda bank ukasaini mkataba wa Agency Business.
GTA
Habar!
Kwa NMB Mambo yapo hivii;
1.Biashara iwe ina zaidi ya mwaka mmoja.
2.Tin namba TRA
3.Kopi ya kitambulisho
4.Leseni mbili(mpya na yazamani) za biashara
5.Bank statement
6.Picha mbili (Passport size)
7.Picha ya jengo(Kwangu walipiga wao wenyewe)
8.Wadhamini wawili (wawe na vitambulisho)
9.Barua ya mtendaji wa kijiji au kata
10.Mtaji(Kianzio) 2,000,000/=
gharama ya mashine 200,000/=
Muhuri 50,000/=.
kwa CRDB Mahitaji yanafanana lkn nitakuthibitishia kuhusu kianzio kukipambazuka.
Nakutakia mafanikio