Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Mimi siyo mdau sana wa kuanzisha nyuzi kuhusu member humu ndani lakini leo nimejikuta tu ninyooshe mkono wangu kumtakia heri member financial services. Leo nilikuwa napita humu nikakutana na uzi wake february akiuliza na kuomba ushauri kuhusu namna ya kukabiliana na hali ya kufikisha miaka 30 bila kuwa na familia. Nilijisikia kuguswa maana mara kadhaa nimekutana na nyuzi zake akieleza changamoto mbalimbali anazopitia kwenye mahusiano. Hata akichangia kwenye nyuzi nyingine zinazohusu mahusiano, comments zake zinaonekana kama ni mtu aliyekata tamaa but bado anamiini pengine kutakuwa na chance nyingine ya yeye kuufurahia ulimwengu huo.
Siyo rafiki yangu, but mara chache chache huwa najaribu kufanya naye mazungumzo kwenye nyuzi za watu just kujaribu kufanya ajisikie poa. Sijui kama nitaonekana kama najipa umuhimu kwenye maisha ya mtu mwingine but hivyo ndivyo akili yangu imekuwa ikinisukuma. Kama jamii, tunaishi na watu wenye changamoto mbalimbali hivyo ni vyema kuonyeshana ukarimu ili kufanya kila mtu ayafurahie maisha haya mafupi tuliyonayo.
So, mimi napenda kumwambia ndugu yangu huduma za kifedha kuwa kila mmoja ameonja uchungu wa kikombe cha mahusiano. Tunachotofautiana ni kiasi cha maumivu tuliyoyapata na uwezo wa kuhimili na kufanya maamuzi ya kusimama tena na kusonga mbele. Kuna wanaopona haraka, wanaochelewa na kuna ambao huathiriwa sana kiasi cha maisha yao kuchukua njia mpya kabisa ambayo hawakuwahi kabisa kuifikiria.
Hivyo basi, japokuwa sijui sana kwa undani ni kipi hasa kilimtokea lakini napenda kumtakia kila lenye heri katika ulimwengu huo. Najua kuwa kadri muda unavyokwenda na unaona vitu havitokei inaweza kuamsha hisia za ku-panic hali inayoongeza uwezekano wa kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Hivyo namuomba awe tu mtulivu ili aweze kuchakata kila aina ya taarifa inayokuja mbele yake kwa usahihi.
Kuna watu wanaweza kuhoji kwa nini nisingemtumia tu ujumbe binafsi. Ndiyo, ni jambo jema lakini naamini kuwa hayuko peke yake, kuna watu wengine ambao wanapitia hali anayopitia, hivyo ninachokisema kwake nakisema na kwao pia. Lakini pia mkuu financial services, samahani kama hautafurahishwa mimi kuanzia uzi huu kukuhusu, lakini nikuhakikishie kuwa lengo langu halikuwa baya.
Lakini kama pia labda nilichokisema siyo kile unachokipitia kwa maana ya pengine labda sikuelewa vyema nyuzi zako na comments zako ama ni stunts tu za jf kupiga soga kufanya muda usonge, pia kumradhi.
Uzi tayari...