Napendekeza Bagamoyo iwe sehemu ya Zanzibar ili na sisi tuzamie tupate uraia wa Zanzibar tupate nafuu ya ajira, vyeo, teuzi, n.k

Napendekeza Bagamoyo iwe sehemu ya Zanzibar ili na sisi tuzamie tupate uraia wa Zanzibar tupate nafuu ya ajira, vyeo, teuzi, n.k

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Niendelee kung'ang'ania ubara kwanini wakati uraia wa Zanzibar unarahisisha maisha?

Wazanzibar wamebahatika zaidi kupata uwanja mpana tena wa kipendeleo kabisa katika nafasi za uongozi, ajira, vyeo, teuzi, n.k.

JKT wengi kama sio wote huwa wanabakizwa kujiunga na Jwtz, Polisi, Usalama, n.k na huko wakifika kukiwa na nafasi za vyeo wanapewa kipaumbele maalum ili kubalance mzani wa muungano, Kwa watu wengi wa bara wakimaliza JKT hurudi vijijini kuendelea kulima ama kwenda suma jkt.

Nafasi za ajira wana fungu lao, kigezo kikuu ni uzanzibari, huku wabara wanapigana vikumbo kupata ajira, wazanzibari wapo wamekaa pale wana fungu lao ile asilimia 21.

Teuzi za wakuu wa wilaya, wakurugenzi, mabalozi, n.k. wazanzibar wanaulamba.

kazi za huko Zanzibar ni zao tu, na wana kila taasisi ambayo ipo huku kwetu kuanzia tra, tff, nssf, n.k. wanapiga kote kote kwao na kwetu.
 
Maslahi kwanza utaifa baadae, Vijana wazawa wa kitanganyika wana mavyeti ya degree wapo kitaa, wengine wamejitolea jkt miaka wamerudishwa kitaa, wazanzibar waliokuwa nao huko vyuoni na kambini wana ajira maofisini na majeshini hapa hapa Bara..

kwanini mtu asiutamani uraia wa Zenji?
 
Kwa kweli muungano wetu unatia uchungu sana, imagine raha wanazokula wazanzibar halafu bado wanalalamika. Naamini ipo siku Tanganyika itasimama kivingine
 
Kwa kweli muungano wetu unatia uchungu sana, imagine raha wanazokula wazanzibar halafu bado wanalalamika. Naamini ipo siku Tanganyika itasimama kivingine
Mzanzibari akiweza kufika hadi degree ana uwezekano mkubwa sana wa kupata ajira hapa kwetu kuzidi mtanganyika mzawa.

Mzanzibari akija kujiunga JKT hapa kwetu ana uhakika wa kuajiriwa jeshi lolote lakini wazawa watanganyika wa hapa wakimaliza mafunzo wanarudishwa majumbani.
 
Back
Top Bottom