Napendekeza: Harusi ya mzee Mengi ifanyike uwanja wa Taifa

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Kama tujuavyo Mzee Machache yupo katika pilika pilika za kufunga ndoa na mchumba wake mrembo (K-Laini) sasa kwa jinsi mzee huyu alivyo na watu na umaarufu wake napendekeza harusi ifungwe pale Uwanja Mpya wa taifa.

Ili matabaka yote tuhudhurie,hongera sana mzee & K-Laini. Kazi imebaki kwa Madam Wema na mpenzi wake wa zamani Diamond a.k.a Dangote.
 
Daah uzee sasa mwisho Segera daah! Mzee kajitwalia mtoto lainiiiiiii anatafuna taratiibu. Hiyo harusi sidhani hata kama itafungiwa Tanzania. Kwa nyie Subirini Harusi ya Babu wa CHADEMA.
 


Ni kweli kwa maana ya watu wa tabaka zote kuhudhuria, lakini kumbuka uwanja wa taifa ni kwa ajili ya michezo, na ulipaswa Kua uwanja weNye heshima na hadhi kuubwa kabisa tofauti na sasa ambapo umekua ni uwanja wa mechi za mabonanza kama mtani jeMbe, wasanii wa filamu vs bongofleva, masheikh vs maaskofu, na siku nyingine hata matamasha ya muziki kufanyika hapo.

hili linauondolea hadhi uwanja huu ambao umejengwa kwa gharama kuubwa mno na matokeo yake kusaabisha uchakavu wa mapema kwa miundombinu yake.
Sishangai kwa nini siku hizi hata mechi za ushindani za timu ya taifa hazina hamasa tena, ni kwa sababu tayari uwanja umeshakuwa wa kawaida sana kwa watu kwani karibu kila wiki kuna mechi za mabonanza zisizo na tija au tamasha la wanamuziki.
Kwa wenzetu watu wanavimis viwanja vyao vya taifa hadi kupelekea kuchajiwa pesa kwenda kufanya tour tu na siku za mechi pale taifa lao liwapo uwanjani watu huwa na hamasa za kutisha.

Nadhani ombi lako likipitishwa si muda mrefu uwanja huu utageuka kumbi la sherehe kwa watu maarufu na wengine watataka kuutumia kwenye sherehe zao za birthday, kipaimara na hata sendoffs.
JAMANI TUUPE HADHI UWANJA HUU UMEJENGWA KWA MABILIONI YASIYOPUNGUA SITINI NA USHEHE HIVI,,,,,,
 
Daah uzee sasa mwisho Segera daah! mzee kajitwalia mtoto lainiiiiiii anatafuna taratiibu. Hiyo harusi sidhani hata kama itafungiwa Tanzania. Kwa nyie Subirini Harusi ya Babu wa CHADEMA.

Siasa hadi huku... umetishaje...!!
 
Hongera Mwnyekiti Machache. Au ndo unajiandaa kugombea Uraisi. Anyway! Na hili la Wema ameingiaje humu jamani? Mwacheni na maisha yake.
 
aisee, yaonyesha unapenda kuhudhuria harusi eh...!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…