Ni wazo zuri sana, ila mimi najiuliza hivi tuna timu za vijana ngapi zilizo hai?
Serengeti Boyz iliishia wapi?
Kakakuona pia iliishia wapi?
Under 20 ile iliyoundwa baada ya Coca Cola Cup final iliyojumuisha mikoa yote ipo wapi? na timu nyingi nyingi tu za vijana ambazo baada ya mashindano kuisha basi vijana wanapoteana.
Sishangai hata hii timu ikapotea baada tu ya mashindano hayo. Mikakati mingi utekelezaji hafifu hivi kweli tutasogea tunapotaka tufike? Bila kuwekeza kwenye Kandanda tusahau kufikia level ya nchi kama Cameroon, Misri, Tunisia, Ghana, Nigeria.
Kuwafunga Cameroon si kigezo kwamba tunaweza, cha msingi ni kuifanya timu hii itake over in next two years by then watakuwa na miaka 25 average.
Natoa Pongezi zangu za dhati kwa Julio, ni kocha mzalendo na anakipaji cha kupandisha mori na ari ya ushindi kwa timu anayofundisha, ni kweli style yake ni sawa na Jose wa Madrid, anacheza na saikologia na wachezaji na hii ipo katika makocha wachache duniani.
Bravo naunga mkono akabidhiwe timu - na hii timu iwe ya kundumu.