Napendekeza kuanzishwa kwa ‘Human UBER Services’ kwa miji ya Dar es Salaam na Dodoma kuongeza ufanisi katika ukuaji uchumi

Napendekeza kuanzishwa kwa ‘Human UBER Services’ kwa miji ya Dar es Salaam na Dodoma kuongeza ufanisi katika ukuaji uchumi

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kwa kutumia mfumo huu wa ‘Human UBER Service’ (HUS) mtu anakuwa Na uwezo wa kwenda hadi Dodoma toka Dar ‘Virtually’ bila kusafiri, ambapo atafanya kazi zake Dodoma na kurudi Dar, muda wote hio akiwa amelala tu kwenye sofa nyumbani kwake.

Katika mfumo huu, vijana wasio na ajira huko Dodoma watajisajili kwenye database ya kampuni ya HUS, ambapo wataleta dhamana na wadhamini endapo lolote litatokea, wakate na bima ya Liability ikibidi.

Itakapotokea mteja aliyepo Dar es Salaam anahitaji kukodi kijana aliyepo Dodoma kumfanyia kazi zake za mizunguko ya kufuatilia vitu mbali mbali mfano vibali na shughuli zingine mbali mbali huko Dodoma, ataingia tu kwenye ‘app’ ya HUS na kuchagua mmoja wa vijana waliopo online na waliopo karibu na eneo analotaka kumfanyisha kazi (ili automatic bill charges ziwe ndogo), kisha watawasiliana kwa simu au whatsapp na atamueleza kwa kina ni task ipi anaitaka aifanye, mfano :

“Nenda wizara ya madini, ukifika wasialiana na mtu fulani, atakupatia document flani, ukitoka hapo nenda stendi ya basi, kisha itume kwenda mkoa flani kwa mtu flani nk.

Mfanyakazi akishatuma receipt ya bus kwa whatsapp maana yake ameshakamilisha Task, na mteja atapaswa kucheck kibox cha ‘Task complete’, na automaticall ‘Wallet’ yake ya (HUS) itakatwa pesa, ambapo mfanyakazi ataingiziwa pesa kwenye wallet (Tigo pesa) yake na wamiliki wa mfumo watakata comission yao, na serikali kuchukua kodi yake automatically.

Mfumo huu wa HUS unaweza kupunguza mauzo ya Ticket za SGR kati ya Dodoma na Dar es salaam, lakini hii ndio maana halisi ya ‘Uchumi wenye ufanisi’.

Nakaribisha maoni.
 
Uaminifu, Uaminifu, Uaminifu

Kwenye hizi kazi wataingia ma TISS na hata matapeli wafanye yao. Japo ni nzuri sana hii
Ndio maana mwanzoni kabisa, nikasema kijana apeleke dhamana na wadhamini (mfano serikali ya mtaa imtambue nyumba anayoishi,mjumbe wake, na wazazi wake wanapoishi watambulike, nk.), pia akate bima ya kazi yake hiyo (Professional indemnity), ili akivunja uaminifu na kusababisha hasara yeyote, bima wanalipa hasara yote na usumbufu wote atakaosababisha.
 
Labda vimzigo vidogo vidogo, vyeti na vitu ambavyo 'havina maana kuiba" ndiyo unaweza kumuamini mbongo.

Hapa Tanzania mtu anakuibia live, unamjua na anahonga his way out.
 
Labda vimzigo vidogo vidogo, vyeti na vitu ambavyo 'havina maana kuiba" ndiyo unaweza kumuamini mbongo.

Hapa Tanzania mtu anakuibia live, unamjua na anahonga his way out.
Ndio maana nikasema wataweka ‘Dhamana na wadhamini’ ; pia mfumo utaweka tiers ( madaraja) , mtu aliedumu kwa uaminifu, kwa Muda mrefu kwenye mfumo na kupewa rating nzuri zaidi na wateja, atakuwa anachajishiwa malipo makubwa zaidi na mfumo automatically, hivyo kama unakitu cha thamani zaidi, ni vyema ukakodi mfanyakazi mwenye rating kubwa kwenye mfumo maana ameonesha uaminifu na ubora katika kazi, ila utamlipa zaidi kuliko yule mwenye rating ndogo (muda mchache kazini). Pia wafanya kazi waliokatiwa bima kubwa tu ndio utashauriwa kuwapa mizigo yenye thamani kubwa.., ila pia utalipia premium kumtumia huyu mfanyakazi mwenye bima kubwa.
 
Mradi ukionyesha mafanikio, unaweza kuwa rolled out kwa mikoa mingine kama Arusha, Mwanza, Mbeya, na Tanga
 
Inaweza ikawa ni njia nzuri kwa serikali kuongeza wigo wa mapato (kureplace) watakayoyapoteza kwa nyumba za kulala wageni (guest house, lodges, hotels nk.) kukosa wateja.
 
wenzetu japan wameendelea ukiwa na stress unaweza kuajili bibi ana act kama bibi yako kweli vivyo hivyo unaweza kuajiri girlfriend, baba na mama
 
wenzetu japan wameendelea ukiwa na stress unaweza kuajili bibi ana act kama bibi yako kweli vivyo hivyo unaweza kuajiri girlfriend, baba na mama
Kabisa, maendeleo hayana mipaka
 
Back
Top Bottom