Napendekeza kufufua Azimio la Arusha na kurasimisha Katiba ya Warioba

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Habari Tanzania!

Poleni kwa mihangaiko ya hapa na pale kwa marika yote.

Napenda kutoa wazo kwa Utawala wa sasa na ule ujao kama itawapendeza na kuona inafaa kwao; na wanapenda kuona kesho yao ikiwa nzuri wanapaswa kwanza kulifufua upya Azimio la Arusha na baadae ndio pafanyike kusimikisha rasmi iliyokuwa Rasimu ya Katiba ya Warioba kuwa Katiba Mpya.

Hii itachochea kila kona ya nchi kwa pande zote Umma kuheshimika, rasilimali kuwa salama, mgawanyo mzuri wa madaraka na kisekta; siasa na biashara kutokukaa kwenye chungu au sufuria moja kama ilivyo sasa; na Taifa Tanzania litapona haswa haswa pasipo shaka lolote.

Mfano; Tazama changamoto za Kiutawala zinavyotokea katika Siasa, Biashara, Serikali na Michezo hii yote ni upungufu na ukosefu wa Azimio la Arusha na Katiba Mpya iliyochakatwa na Jaji Sinde Warioba.

Tanzania ni nchi nzuri sana.
 
Kipindi Cha hilo Azimio hivyo vitu ulivyo taja vilikuwa katika hali gani?

Na Kama lilikuwa bora kwanini lilianguka mikononi mwa aliye lianzisha?
 
Azimio la Arusha ndilo lililoleta umaskini Tanzania na kuifanya nchi hii ipitwe na nchi nyingi za Afrika. Azimio hili halikuwa na mchango wowote mzuri kwa uchumi wa nchi yetu. Azimio lililenga tu kwenye usawa wa watu na kuwabana matajiri kwa kuwafilisi na kuwazuia wasitengeneze hela nyingi bali wagawane na maskini, matokeo yake matajiri walikimbia, viwanda vilikufa na uchumi kuporomoka mno miaka ya 1980s. Kilichofuata ni mwanzilishi wa Azimio hilo JK Nyerere kujiuzulu mwaka 1984 ili kupisha mabadiliko ya kisera. Sasa mwenye azimio yeye mwenyewe aliona amechemsha na akajiuzulu, wewe unataka kurudisha Azimio lililotupeleka kwenye huu umaskini?! Fikiri vizuri.
 
Ukipata nafasi, lisome upya Azimio la Arusha utapata mwanga nzuri.

Tuachane na kukariri kwa mambo ya kusimuliana vijiweni.
 
Kipindi Cha hilo Azimio hivyo vitu ulivyo taja vilikuwa katika hali gani?

Na Kama lilikuwa bora kwanini lilianguka mikononi mwa aliye lianzisha?

Umuhimu wa Azimio la Arusha na Katiba Mpya ni mkubwa mno tofauti na fikra za wengi.

Tanzania bado watu wengi wanawaza kuhodhi kila kitu wao; wanataka watu fulani fulani wawe viongozi wao tu na vizazi vyao, wajihusishe kwenye kila kitu; mwisho ndio wao kuwa chanzo cha umasikini.

Bado tunayo nafasi ya kulileta Azimio la Arusha na Kusimika Katiba Mpya (Warioba) ndio dawa ya kuondoa umasikini na kuleta usawa katika taifa.

Asante.
 
Kijana fungua akili yako na yaone mambo kwa uhalisia na sio kwa nadharia tu! Azimio la Arusha lishapitwa na wakati kijana.

Kuhusu kuwa na katiba mpya nakuunga mkono 100%.

Swali kwako: Najua Azimio la Arusha lilikuwa na baadhi ya vipengele muhimu sana hasa kuhusu maadili ya viongozi wa umma. Zaidi ya maadili ni vipengele vipi ndani ya Azimio la Arusha unavyofikiri ni muhimu kuendelezwa? Jibu tafadhali....
 
Mkuu mbona hauja jibu maswali yangu Azimio hilo matunda yake hayakuwa na manufaa Sana ndo Yale yale mtu anakwiba pesa za umma anakwenda kuhojiwa na kamati ya chama hapana.

Mwalimu mwenyewe lilimshinda hata kulitetea.
 
Kijana fungua akili yako na yaone mambo kwa uhalisia na sio kwa nadharia tu! Azimio la Arusha lishapitwa na wakati kijana.

Kuhusu kuwa na katiba mpya nakuunga mkono 100%.

Swali kwako: Najua Azimio la Arusha lilikuwa na baadhi ya vipengele muhimu sana hasa kuhusu maadili ya viongozi wa umma. Zaidi ya maadili ni vipengele vipi ndani ya Azimio la Arusha unavyofikiri ni muhimu kuendelezwa? Jibu tafadhali....
Mkuu hivi tunahitaji Sheria bora au maadili ya viongozi?
 
Azimio la Arusha ni azimio la kua maskini.kuhusu katiba mpya ni swala la msingi sana
 
Nina uhakika huyu jamaa hajui Azimio la Arusha na hajawahi kulisoma.
 
Tukifufua azimio la arusha tunakua tunaenda kule kwa nyerere

Azimio la Arusha ni moja kat ya sababu kubwa sana kwann Tanzania n masikini , kuhusu katiba mpya nipo na wewe kwa 100%
 
... mrengo wa CCM ni wa kijamaa; ni chama cha kijamaa! Nikionaga yale mamisururu yasiyo na idadi ya V8-VXR kwenye ziara za viongozi hususan aliyepita ni zaidi ya kufuru! Tuache unafiki, tuziambie ukweli japo nafsi zetu!
 
Katiba sawa ,ila sio azimio la arusha ,
Azimio ndo limetuletea umazikini na uvivu uliotopea kwa jina la ujamaa
 
Kijana fungua akili yako na yaone mambo kwa uhalisia na sio kwa nadharia tu! Azimio la Arusha lishapitwa na wakati kijana.

Kuhusu kuwa na katiba mpya nakuunga mkono 100%.

Swali kwako: Najua Azimio la Arusha lilikuwa na baadhi ya vipengele muhimu sana hasa kuhusu maadili ya viongozi wa umma. Zaidi ya maadili ni vipengele vipi ndani ya Azimio la Arusha unavyofikiri ni muhimu kuendelezwa? Jibu tafadhali....
Bro!

Azimio la Arusha nakala zake za vivuli zipo mtandaoni, ukipata wasaa peruzi upate kujisomea.

Azimio lililenga hasa kutokomeza umasikini, kuleta usawa kwa jamii hasa mtu na mtu (kuamini kila mtu ni sawa), haki, maadili kwa viongozi sambamba kuleta tumaini la kujitambua.

Azimio la Arusha + Katiba Mpya ndio mwiba na dawa ya maradhi yote tuliyonayo hasa umasikini, ujinga na siasa safi.

NB
Nafahamu jinsi watu wanavyojishtukia endapo Azimio la Arusha likirejea sababu kuu kwa walio wengi wameshazoea maisha ya kidhalimu na kizandiki ndio hofu ya anguko lao.
 
Katiba sawa ,ila sio azimio la arusha ,
Azimio ndo limetuletea umazikini na uvivu uliotopea kwa jina la ujamaa
Haahaa!

Unajiona mjanja pasipo maana. Ulishawahi jiuliza kwanini mmakonde na mzaramo wanakaa pamoja pasipo kutakana kujuana au kubaguana? Chanzo cha hill ni Azimio la Arusha.

Wewe kuwa huru na kupata hata nafasi uliyonayo chanzo chake ni hilo Azimio la Arusha.

Hakuna jambo zuri na maana kwetu kama taifa kuleta Azimio la Arusha upya na Katiba Mpya (Warioba) hii nchi itakuwa raha kila kona.
 
Nina uhakika huyu jamaa hajui Azimio la Arusha na hajawahi kulisoma.
Hakuna andiko zuri hasa kama taifa tumepata kuyaandika mfanano na Azimio la Arusha na Katiba Mpya ya Jaji Warioba.

Haya maandiko yanapita mambo yote katika taifa.

Leo hii watu wanalalamika hatuna mfumo imara na mzuri kiutawala. Sasa Azimio la Arusha lipo na Katiba Mpya ya Warioba ipo; kazi iwe kwetu kama taifa.
 
Bro!

Azimio la Arusha nakala zake za vivuli zipo mtandaoni, ukipata wasaa peruzi upate kujisomea.

Azimio lililenga hasa kutokomeza umasikini, kuleta usawa kwa jamii hasa mtu na mtu (kuamini kila mtu ni sawa), haki, maadili kwa viongozi sambamba kuleta tumaini la kujitambua.

Azimio la Arusha + Katiba Mpya ndio mwiba na dawa ya maradhi yote tuliyonayo hasa umasikini, ujinga na siasa safi.

NB
Nafahamu jinsi watu wanavyojishtukia endapo Azimio la Arusha likirejea sababu kuu kwa walio wengi wameshazoea maisha ya kidhalimu na kizandiki ndio hofu ya anguko lao.
Unaweza share copy humu ili sote tufaidike kusoma
 
🤭Mkuu Masalu ubunge bado unautaka??
Wakikusoma sidhani ka wajumbe watakuacha salama??
Katiba ya Warioba?? Yule aliyepigwa vichwa na ngwara na Mkolomije?

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Habari Tanzania!

Poleni kwa mihangaiko ya hapa na pale kwa marika yote.

Napenda kutoa wazo kwa Utawala wa sasa na ule ujao kama itawapendeza na kuona inafaa kwao; na wanapenda kuona kesho yao ikiwa nzuri wanapaswa kwanza kulifufua upya Azimio la Arusha na baadae ndio pafanyike kusimikisha rasmi iliyokuwa Rasimu ya Katiba ya Warioba kuwa Katiba Mpya.

Hii itachochea kila kona ya nchi kwa pande zote Umma kuheshimika, rasilimali kuwa salama, mgawanyo mzuri wa madaraka na kisekta; siasa na biashara kutokukaa kwenye chungu au sufuria moja kama ilivyo sasa; na Taifa Tanzania litapona haswa haswa pasipo shaka lolote.

Mfano; Tazama changamoto za Kiutawala zinavyotokea katika Siasa, Biashara, Serikali na Michezo hii yote ni upungufu na ukosefu wa Azimio la Arusha na Katiba Mpya iliyochakatwa na Jaji Sinde Warioba.

Tanzania ni nchi nzuri sana.
Mambo yako kwenye PIPELINE tumpe Mother muda.Rome haikujengwa kwa siku moja.Tena tuendelee kupiga debe aongezewe muda kama vile tulivyofanya kwa Hayati Magufuli...ie muhula huu uwe SABA miaka na ujso uwe SABA pia.
 
Back
Top Bottom