Napendekeza kuundwa kwa taskforce ya kuleta pamoja wahindi wa daraja la chini wenye ujuzi rahisi toka India na kuwafungia kwenye karakana hapa nchini

Napendekeza kuundwa kwa taskforce ya kuleta pamoja wahindi wa daraja la chini wenye ujuzi rahisi toka India na kuwafungia kwenye karakana hapa nchini

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kuhusu maendeleo ya kiteknolojia, Africa hatujalogwa na wala hatuna udhaifu wowote ule wa kimwili au kiakili unaotufanya tuwe nyuma kiasi hiki, bali ni mazingira ya makusudi tuliyowekewa na waliotutangulia kuhakikisha tunabaki nyuma zaidi ili tusipate uwezo wa kuzitumia rasilimali zetu na hivyo waweze kujichotea kwa urahisi, huku sisi tukibaki soko kwa ajili ya bidhaa zao.

Swali la kujiuliza, kama Japan wana akili sana kuliko wa Africa, ni kwanini hawakugundua uundaji wa magari mwaka 1200, au 1300, au 1500? Kwanini? Kwamba waingereza, WaItaliano, Wajerumani na Wajapan akili zao zililipuka tu ghafla kwa pamoja miaka ya 1900 mwanzoni na wote ubongo wao ukawa umepevuka na kupata werevu wa kuunda magari kwa pamoja?!

Jibu ni hapana! Teknolojia ilianza kwa mmoja wao, na pakafanyika ‘Technology Transfer’ kwenda kwa wengine! Hali kadhali kwa vifaa vingine vyote vya kiteknolojia, kama Tarakilishi , simu na simu janja; sasa ni kwanini hii ‘Technology Transfer’ inakwepeshwa kwa Makusudi huku Africa?!

Mbina kadha zilitumika na China kuhamisha Teknolojia toka Marekani kwenda kwao. Waliwapa makampuni ya Kimarekani ukumbi wa kuanzisha viwanda bila kutozwa kodi nchini China, huku wakiweka kima kidogo sana cha mshahara, ni kama mtu ulipe mfanyakazi laki 1 kwa mwezi, hata wewe kama unakampuni ya magari lazima ukimbilie China ili upate faida kubwa! Hapa ndipo China alipotumia mwanya huu kuiba technology karibu zote za Marekani!

Marekani pia walitumia mabavu kuiba technology nyingi za wanasayansi wa kiyahudi wa Adolph Hitler mwishoni mwa vita pili ya kuu ya dunia. Mfano ni Rocket science among others, wayahudi wengi wanasayansi waliokimbilia Marekani walikusanya na kuamrishwa watoe siri zote za kitaknolojia za Adolph hitler, hata Atomic Bomb ilitokea kwake.

Wahindi , Japan na Wengine wote wametumia mbinu zao kivyao ili kupata ‘Technology Transfer’.

Sasa kwakuwa sisi hapa tunao akina Faustine Mafweli, napendekeza kiundwe kikosi chini yake cha kwenda kuwateka wahindi wa daraja la chini (Lower caste) wanaofanya kazi viwandani ambao kule hawathaminiki kabisa, kisha wawekwe kwenye zile Karakana kama aliyopekwa Sativa, wabinywe kisawasawa hadi watufundishe A to Z kwa mfano motor zinaundwa vipi, Transformer zinaundwa vipi, from scratch, na hapa simaanishi theory zile tunazofundishea darasani, bali practically, motor iundwe na ikajaribiwe kusaga na kukoboa mahindi. Hadi tufike.

Mfano huyo muhindi hapo chini, tukiwateka kama hawa 100, hatufuki kweli?!

Na wakitekwa , tunapora na ‘Mold zote’ ikiwezekana


View: https://youtu.be/9OpwrbdyMvU?si=8bMkOHf9OpkO-_1A
 
Watungaji na watekelezaji sera waende study tour nchi za Asia mfano India, Bangadesh wakajifunzw kutekeleza sera ya viwanda vidogo vidogo kwa vitendo. Kuna bidhaa hatutakiwi kuagiza China ambazo zinaweza kutengenezwa hapa nyumbani.

Je, tunafeli wapi mpaka tunashindwa kuwa na viwanda vidogo vidogo vingi na vya kati maeneo mbalimbali ya nchi ikiwa tuna malighafi mbali mfano Chuma ili kuepuka kuagiza bidhaa za kawaida kutoka China mfano bidhaa za majumbani, spea za pikipiki, baiskeli nk. Inawezekana vipo huko mkoa uliopo, tuhabarishane.

Kwa mfano, huwa natazama mtandaoni video fupi fupi kuhusu viwanda vidogo vidogo katika nchi za Asia mfano Bangladesh, India na nchi nyingine zinazoendelea.

Viwanda hivyo vidogo vidogo kwa asilimia kubwa mikono ya binadamu inatumika kuiongoza mitambo na wala si maroboti lakini wanazalisha bidhaa ambazo wangeagiza nje ya nchi.

Pia, wakati mwingine viwanda hivyo vipo uchochoroni tu kwa zana duni lakini bidhaa zinazalishwa.

Huku kwetu TZ, tatizo ni nini? Hatuamini katika viwanda hata vidogo vidogo?

Je, sheria za kuanzisha viwanda ni ngumu sana?

Je, mashine na mitambo ya viwanda ni gharama hata za bidhaa ndogo ndogo? Au tatizo ni nini?

Utasikia tu mtu anasemwa mtaani, yule jamaa ana pesa ndefu. Watu kama hawa tuwashauri wawekeze katika viwanda vidogo vidogo ili kuzalisha ajira kwa Watanzania wenzao na siyo kujenga majumba tu na frame za kupangisha kwa kutegemea kuchuuza bidhaa za China.

Kwa kweli huko Asia wanapambana na kuamini katika viwanda. Inawezekana sisi Watanzania hatuamini katika viwanda mana tunashindwa kabisa.

Watunga sera walitizame suala la viwanda kwa jicho la tatu kwakweli. Ikiwezekana, serikali hata imuondolee kodi zote kwa miaka kadhaa mtu anayetaka kuanzisha kiwanda ili tuachane na uchumi wa fremu za kupangisha pamoja na uchuuzi wa bidhaa za China ambazo tunaweza kuzalisha humu humu.

Naambatanisha video baadhi (zipo nyingi) fupi fupi za viwanda vidogo vidogo kutoka huko Asia ambapo sisi huku TZ tunaagiza China mfano spea za pikipiki nk. Naomba usionee huruma bando lako, bali zitazame hizo video halafu tujilinganishe na sisi. Waonesheni matajiri wakanunue mitambo na watunga sera warahisishe mazingira.

 
Back
Top Bottom