Napendekeza,mdahalo ya wagombea iwe ni sehemu ya Katiba

Napendekeza,mdahalo ya wagombea iwe ni sehemu ya Katiba

emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
2,775
Reaction score
3,106
Ndugu wanabodi nimetafakari jinsi tulivyouziwa mbuzi kwenye gunia tukampata kiongozi wa sasa ambaye mambo mengi anayofanya si tu yanakiuka manifesto ya chama chake lakini pia wananchi hatukupata nafasi ya kuelezewa kwa kina yale amabayo angefanya.

Kama tungefanya mdahalo tungeweza kumpima huyu jamaa katika mambo yafuatayo:

1. Temper - tungempambanisha na wenzake jukwaani tungeweza kusoma body language tungeweza kujua jinsi asivyoweza kuhimili vishindo vya kubishana na kukubaliana au kutokubaliana na mawazo ya wengine.

2. Kufanya mdahalo na wagombea wengine kutatupa nafasi ya kuhoji kwamba mabo fulani hayakutekelezwa ingawa wakati wa mdhalo aliyaahidi.

Kama kuna sababu na wewe unaziona ni muhimu kufanyika naomba uongezee. Najua CCM huwa wanaogopa sana midahalo matokeo yake wanatuuzia kanyabwoya. Ikiingizwa kwenye katiba watakuwa hawana pa kutokea.
 
Back
Top Bottom