Napendekeza Salamu ya Kudumu ya Kitaifa

Napendekeza Salamu ya Kudumu ya Kitaifa

Kichwamoto

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
3,403
Reaction score
4,692
Habari za leo wanajamvi.

Ni imani yangu ya kwamba sote tu wazima wa Afya.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Kwa miaka pengine toka uhuru taifa letu halina salamu ya kudumu ya kitaifa isiofungamana na imani wa itikadi. Binafsi nimetafakari sana juu ya kauli mbiu ama salamu ya awamu ya 6 ya Comrade Mhe. Rais Samia S. Hassan. "Nawasalimu kwa jina la JMT" Kazi iendelee..

Pendekezo: Salamu ya kitaifa iwe " Uhuru na Umoja" kiitikio " Nguvu yetu" kisha tunarudia kinyume chake "Nguvu yetu" kiitikio "Uhuru na Umoja".

Naomba kuwasilisha.

Wasalaaam
Galileo_Gaucho
 
Hiyo ya mama umeiona Shida gani ndani yake?
Swali zuri sana nimeonelea ya kwamba nilete chachu hii kwa tafakari tu na sio katika muktadha kinzani. Lazima iwe sasa labda hata nyakati zijazo katika kuimarisha hisia za umoja, uzalendo, mshikamano, A greeting that embraces Sustainable National coehessiveness. Nawasilisha
 
Hivi ile ya Bwana Yesu asifiwe Salamualeku ile ya Mwendazake ndio imetoswa mazima?
 
Hivi ile ya Bwana Yesu asifiwe Salamualeku ile ya Mwendazake ndio imetoswa mazima?
Ni zote na ni Rais huyu tu ndio hatumii utaratibu wa zamani, wengine huku chini wanatumia na zile za zamani
 
Back
Top Bottom