Mkuu CCM haikutaka vyama vingi, na mpaka sasa inaonesha hivyo. Vyama vingi lilikuwa ni wimbi ambalo liliikumba karibu kila nchi ya Afrika. CCM ilikataa kwa kuwa kura za maoni zilionesha asilimia 80 ya watanzania hawataki vyama vingi, lakini heababu za kisiasa za Nyerere zikawahimiza wakubali. Hata vyama vya upinzani kama NCCR mageuzi vilianzishwa na usalama wa taifa kucontain opposition, mpaka sasa kazi hiyo inaendelea kwa viwango tofauti. George Liundi alijaribu kusema lakini akanayamazishwa.
Mentality ya CCM ni kuendela kutawala tu na kuhakikisha hakuna genuine opposition, na sio kuendeleza nchi. Having said that, ni lazima tukubali kuwa wananchi bado tuko kwenye mind set ya chama kimoja japo kuwa kisheria tuko kwenye vyama vingi, viongozi wa oppositin hawajakuwa serious kuhimiza mabadiliko ya katiba ili iwe ya kweli inayoendana na plural politics.
Umemaliza kaka tatizo ni upinzani, hata mimi ningekuwa CCM nisingetaka kuondoka! CCM haitaondoka kwa maombi! kwa kujitoa na kugharamia
Nchi hii siyo ya CCM! wala sio ya chadema, NCCR n.k ni ya wote watanzania!
hakuna upigaji wakura wowote nchi hii utakaomake sense kama
1. Hakuna mabadiliko ya katiba, katiba itakayo accomodate vyama vyote( serikali ya mseto) , serikali ya mseto inaamsha vyama na vyote vinakuwa active, sijui nani anakataa hili na sijui Zanzibar wameweza vipi
2. Rais lazima apunguziwe madaraka, haiwezekani, jaji mkuu uteue wewe, mkuu wa polisi, jeshi, PCCB, n.k!!
3. Tume ya uchaguzi iwe tume huru
Tukifanya hayo tutakuwa tunajenga msingi mpya wa taifa jipya.
Nashukuru umesema vyama vya siasa vimelala! sasa vyama vya siasa kama vinaingia kwenye chaguzi ili hali wakijua hayo hapo juu yanatakiwa,
tuwaeleweje??
Opportunity:
Mwaka huu vyama vyote vya upinzani visusie uchaguzi kwa kulazimisha hayo mabadiliko. Tena tunawapa ushauri wakati mzuri kabisa, maana inaonekana mwaka huu mnajua kabisa mtashindwa, hata sisi mmetuaminisha hivyo. Hivyo basi, ili mwaka 2010 usipotee bure, na muwe na uzito sawa na CCM katika chaguzi zote zijazo, katiba lazima ipiganiwe.
CCM kwa sababu wanawaza kuombaomba nje, nyie nanyi utangazieni ulimwengu kuwa hamtafanya uchaguzi mpaka katiba ibadilike! kimoyo moyo mnajua kabisa mkiingia kwenye uchaguzi mtashindwa! so why dont you think of taking this peace of advice?? kumbukeni dunia itawasupport kwa hili.
we will be behind you!