Napendekeza vijiji vyote kila wilaya wahamie kwenye kijiji kimoja teule, vijiji vingine vibaki mashamba tu

Operesheni vijiji miaka ya 1970.
Simaanishi ujamaa, kila mtu analima shamba lake kwa uwezo wake, atakaefanya kazi kwa bidii ndio atasonga mbele zaidi, ila tukipeleka transformer moja la umeme tunahudumia vijiji 10 kwa mpigo. Juzi kati nikiwa safarini kuingia Chemba ndani ndani nimecheka sana, Tanesco wameunguza matrillion kusambaza umeme kwa minguzo ya kibao , halafu unakuta mwishoni kabisa kumbe umeme ulikuwa umepelekwa kwenye nyumba hata tatu hazifiki. Ilibidi nisimame nishuke kuangalia vizuri, nilitafakari sana, nisijue nicheke au nilie
 
^Makaburi ya wazee nayo yatahamishwa?^~ Sauti kutoka mkoa fulani.
 
Simaanishi ujamaa, kila mtu analima shamba lake kwa uwezo wake, atakaefanya kazi kwa bidii ndio atasonga mbele zaidi, ila tukipeleka transformer moja la umeme tunahudumia vijiji 10 kwa mpigo. Juzi kati nikiwa safarini kuingia Chemba ndani ndani nimecheka sana, Tanesco wameunguza matrillion kusambaza umeme kwa minguzo ya kibao , halafu unakuta mwishoni kabisa kumbe umeme ulikuwa umepelekwa kwenye nyumba hata tatu hazifiki. Ilibidi nisimame nishuke kuangalia vizuri, nilitafakari sana, nisijue nicheke au nilie
Chemba Jimbo la Mhe Juks
 
Makanisa yakae mtaa mmoja, misikiti mtaa mmoja, bar mtaa wake, ijulikane vijiji vya makahaba, bila kuwasahau wazee wa ganda la ndizi mashoga wakae mtaa wao, walokole mtaa wao, bikira mtaa wao, wenye ajira mtaa wao, wafanyakazi mtaa wao!
Wakulima kivyao, wafugaji kule, wavuvi wasirudi inchi kavu wabaki baharrin,
Uwanja wa taifa iwe mesi ya wanafunzi wote dar!

ITASAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA
 
Simaanishi ujamaa, kila mtu analima shamba lake kwa uwezo wake, atakaefanya kazi kwa bidii ndio atasonga mbele zaidi, ila tukipeleka transformer moja la umeme tunahudumia vijiji 10 kwa mpigo. Juzi kati nikiwa safarini kuingia Chemba ndani ndani nimecheka sana, Tanesco wameunguza matrillion kusambaza umeme kwa minguzo ya kibao , halafu unakuta mwishoni kabisa kumbe umeme ulikuwa umepelekwa kwenye nyumba hata tatu hazifiki. Ilibidi nisimame nishuke kuangalia vizuri, nilitafakari sana, nisijue nicheke au nilie

Ingekuwa kila neno linalipiwa, aisee! Wewe ungekula hasara kubwa sawa na Tozo na Kodi na Mikopo ya Bi Mkubwa katika nchi hii!!!
 
Ukipeleka mnara mmoja wa simu unahudumia vijiji 20 kwa mpigo. Ni hayo tu, labda kama kuna mengine ya kuongezea
Nyerere aliwaza kwa mtindo huo, lakini binadamu hata umpe nini huwa haridhiki, anapenda uhuru wa kujiamria zaidi kuliko kuamriwa ama kupangiwa!

Ye'aliwaza kuwa akiwarundika katika vijiji vyenye sura na mipangilio ya kimtaa,basi itakuwa ni rahisi serikali kuwahudumia.

Raia hawakuridhika na maisha hayo, wakaishi kwa amri ya serikali kishingo upande.

Ilipofika '84, Mh. Mwinyi akatengua utaratibu huo uliokuwa umedumu kwa miaka 10 na kuruhusu watu waishi wapendavyo.

Kulianzisha upya wazo lililokuwa limeanzishwa na likafeli, si rahisi sana kupokelewa na kuungwa mkono, maana watu wana kumbu kumbu nalo.

Embu kwanza fikiria, jiografia isivyo rafiki kwa baadhi ya maeneo, watu uwarundike let say km.40 toka yalipo mashamba yao, hizo gharama za kuwapeleka na kuwarudisha mashambani kufanya kazi kila siku zipo, nk nk?
 
Back
Top Bottom