maganjwa
JF-Expert Member
- Sep 11, 2012
- 2,800
- 2,339
Mfumo wa elimu napendekeza ubadilishwe kuanzia shule ya msingi kwa walimu wenye sifa za degree na kuendelea kwa kuwa kufundisha ni kujenga taifa lenye nguvu na linaloweza kujitegemea. mtoto mdogo ni sawa na daftari mpya ambayo haijatumika kwa hiyo walimu hao wenye uwezo ambao sio walioshindwa kidato cha nne wakifundisha watoto taifa itapata wataalamu wazuri siku za usoni kuliko hali iliyopo hamasa ya sayansi imekufa kabisa. Hakuna Taifa lililofanikiwa bila sayansi lakini kwetu Tanzania masomo ya art ndio inakimbiliwa ambapo kwa hali hiyo taifa itaendelea kuagiza wataalamu kutoka nje hasa fani ya mbalimbali ya sayansi. Naomba tujadiliana je pendekekezo langu linaweza kuwa jawabu?