Napendekeza walimu wenye sifa kuanzia degree kufundisha kuanzia shule ya msingi.

maganjwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2012
Posts
2,800
Reaction score
2,339
Mfumo wa elimu napendekeza ubadilishwe kuanzia shule ya msingi kwa walimu wenye sifa za degree na kuendelea kwa kuwa kufundisha ni kujenga taifa lenye nguvu na linaloweza kujitegemea. mtoto mdogo ni sawa na daftari mpya ambayo haijatumika kwa hiyo walimu hao wenye uwezo ambao sio walioshindwa kidato cha nne wakifundisha watoto taifa itapata wataalamu wazuri siku za usoni kuliko hali iliyopo hamasa ya sayansi imekufa kabisa. Hakuna Taifa lililofanikiwa bila sayansi lakini kwetu Tanzania masomo ya art ndio inakimbiliwa ambapo kwa hali hiyo taifa itaendelea kuagiza wataalamu kutoka nje hasa fani ya mbalimbali ya sayansi. Naomba tujadiliana je pendekekezo langu linaweza kuwa jawabu?
 
mbona wapo wengi na bado wanakuwa vilaza ww ulifundishwa na walimu wa upe na umefanikiwa.kunatofauti ya kuelimika na kuelimisha.kuna walimu wenye upper class na bado wanashindwa kufundi vizuri.tafakar
 
Unapendekeza walimu wenye degree wawe wanafundisha shule za msingi mmejiandaa vipi kuwalipa ikiwa kuna wabunge darasa la saba wanalipwa kuliko malecture wa chuo kikuu unafikiri nani atataka kupoteza muda wake kwenye kazi isiyo na malipo mazuri
 
Mbona wapo hata wengi sana! Sekondari (tena O- Level)wapo hata wenye masters weni sana! Ikiwa kama mazingira ya kufanyia kazi yameoza, serikali imesahau kama kuna uhitaji wa elimu bora.
 
Nani mwenye digrii yake atakubal kwenda kijijin akalale nyumba za nyasi na wkt mjin ajira kbao? Halaf kua na digrii haimaanishi ndio kua na ujuz wakutosha, wapo wenye digrii za kununua, kumbuka waalim hao hao wa certificate ndo ambao mpaka leo wametufikisha hapa tulipo na hal hii ya ss ya kudorora elimu wakulaumiwa n serikal kwan mazngra ya walimu kuanzia maslah na miundombinu yao @ mmoja anaiona.
 
Mmeongelea kila mahara mi naomba niongelee kuhusu hayo masomo ya sayansi, Kwa ushahidi ulio wazi kuna shule moja ya sekondari ya serikali inaitwa VIWEGE SEKONDARY SCHOOL, hii shule haina mwalimu hata mmoja wa sayansi zaidi ya kujaza walimu wa art.
Nilifundisha mwezi wa kumi na kumi na moja Chemistry yaani madogo ni sharo mbaya sio hawasomi bali form two na4 walisoma kisela ili2 ionekane wamesoma yaani ni kwamba serikali hawataki watoto wa maskini wafaulu.
Pia la mwisho ni kwamba wanataka waibe vizuri hawa wana CCm cuz unakuta wanamleta mtaalamu wa Software wakati 2nao kibao na wanaweza kazi mfano kuna website na application software kibao watanzania wamedevelop huwez amini mpaka wizara ya elimu inatumia software kutoka nje wakati yenyewe sometimes inapeleka wa2 ulaya kusomea It 2seme nao hao wako wap au wanafundishwa na form six?. CHUKUA HATUA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…