Napendwa na wanawake wengi na wazuri darasani

RichZ

Member
Joined
Mar 30, 2017
Posts
20
Reaction score
8
Hello,


Mimi ni mwanafunzi wa chuo fulani Morogoro, tatizo langu ni kwamba nilisha tendwa miaka miwili iliyo pita kwa hiyo sipendi kukaa na wanawake huwa na jitenga peke yangu discussion huwa sipendelei kwa kuwa katika kundi letu kuna wanawake 5 japo hupenda sana uwepo wangu kwa kuwa nipo serious na sipendi ujinga muda wa disc.

Tatizo ni kwamba robo tatu ya wana wake wa darasani wote wananikubali sana kimapenzi hupenda kuja nakuniomba niwaelekeze vitu fulani vya kimasomo, na mimi huwa sikatai lakini nikiwa katika kuwafundsha kutegwa kwingi alafu wengi wao wanakuwa wakifikiria mbali hapo ndipo wanaponiudhi.

Wengine wamenitongoza kabisa, nimetokea kuwachukia sana wanawake kwahiyo muda mwingi nakaa na wanaume wenzangu tukiwa katika stori ila tukiwa katika kusoma huwa nakaa alone tuu, nimekuwa gumzo sana kwa upande wa wanawake hadi mwaka wa kwanza tu wananifahamu kwa kuwa nipo tofauti na wenzangu, sijisifii ila ninaongea kilichopo.

Licha ya hayo mimi ninasali dhehebu fulani hivi na huwa napenda sana kufunga na kuomba kulingana na shida zangu kwa MUNGU wangu, nimefuta contacts picha na kila kitu cha alie kuwa mpenzi wangu tangu tuachane na mwezi huu ameanza kunitafuta kwa kunipigia na kunitumia text lakini sijawahi kupokea wala kujibu, sitaki kujua lengo lake nini kwani hata SMS zake huwa anasalimia tu " mambo". Basi nikiona text yake tuu hasira na kuwachukia wanawake zinakuwa mara mbili.

Naombeni ushauri kimawazo nifanyaje ili nifikie malengo yangu bila kuwaudhi na kutoonyesha hasira kwa wanawake.

Pia nimepanga kutokuwa na mtu hadi nitapohitimu masters yangu ingali sasa ni mwaka wa 2 wa degree yangu, kwa mtazamo wako nitaweza.?
 
Ushakuwa wewe Tafuta Msichana , si ushauri mbaya ila ukipata mwanamke wa level yako hapo ulipo utajifunza mengi na akili ktk mahusiano itakomaa
NB . BUT BE SMART AND SAFE HAPO UNAPOSOMA MAANA UKIMYA WAKO SI NGAO YAKO
 
Nimepata shida kusoma kha! Hebu rudia kuandika vizuri,mwanaume hana mwandiko mbovu kama huu halafu eti wewe ni mwanafunzi....
Mara hii umefika huku? Rudi kule muache mtoto asome ili afaulu vizuri.

Naona kijana bado anasoma chuo kwa muongozo wa wazazi ezi ifu yupo sekondari
 
Nnavo wajua watoto Wa chuo wanavyopenda kitonga waje kukuganda kisa sura. Mmmhhhh labda watoto Wa cheti maana diploma tu hawafanyagi huo ujinga
 
We jamaa funga zipu aisee watoto wa mama salma hawajawahi kutuacha salama,,,[emoji29] [emoji29] [emoji29] [emoji29]
 
Damn[emoji16] ...nimei-miss sana JamiiForums ya 2009/13 yaani ingekuwa kipindi kile ndo hivi wala nisingejiunga hapa ila shida sasa nimeshazoea na kutoka hapa siwezi.ona kama hapa:sielewi huyu anataka nini,kwanini na anatufikiriaje sisi tunaopita humu.nawashauri Mods kama kuzuia mada za kitoto toto hawezi basi wawaanzishie kajukwaa kao like TotoForums ili watoto wote wakutane huko pia kutupunguzia sisi wengine mzigo maana inachosha sasa.
 
Unajipromotion haya changanya na za kwako
 
Wanakupenda sababu hawajajua hela hivyo wanakupenda sababu unajiweza kimasomo wewe ni desa. achana nao usilewe mapenzi utafeli alafu mwanamke sio mwenzio baada ya masomo miezi mitatu unakutana naye anadrive range wewe ndio kwanza hata suluari umeazima ukafanyie interview. kuwa mwangalifu wengine wao walianza michezo hiyo darasa la tatu watakupa ukimwi bule.
 
Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…