Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Huyu ndiye kinara wa kuharibu matokeo ya uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015 , hakuna aliyesahau , alipandikiza watu wake kwenye Tume ya Uchaguzi ili kuwabeba wagombea wa chama chake, aliamuru kukamatwa na kuporwa kwa vifaa vya waangalizi huru wa uchaguzi ili kuficha matokeo halisi ili chama chake kibebwe na tume kwa njia za gizani , huyu ndiye aliyekataa Maalim Seif asiapishwe kuwa Rais Halali wa Zanzibar baada ya kushinda uchaguzi uliokuwa huru na haki tena mbele ya waangalizi wa kimataifa , akiwemo Rais Mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan , dunia nzima ilifahamu kuhusiana na uporaji wa matokeo ya Zanzibar ambapo ccm ilianguka vibaya sana kuanzia , wabunge , wawakilishi hadi Urais wa Tanzania na Zanzibar kwa Unguja na Pemba
Mtu kama huyu awezaje kuteuliwa kuwa kiongozi wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola ? wamepanga asaidie tena wizi wa kura Nigeria ? Mtu aliyeshindwa kutenda haki nyumbani kwake atafanya maajabu gani ugenini ? Aliyemteua alitumia vigezo gani , mbona iko wazi kwamba hana vigezo ?
Naomba kuwasilisha