Mkuu Erythrocyte, pamoja na yote unayojitahidi kueleza hapa, elewa kuwa viongozi wa Afrika wanafanana na wanajuana sana. Usifikiri Kikwete anapewa majukumu kwa bahati mbaya. Kwamba “hawamjui”! Hizo spana huko nje hakuna anayezijali.
Mkapa alishawahi kukiri kwa jeuri katika mahojiano na media moja ya kimataifa kwamba haamini sana katika tija ya kuwa na “opposition” hapa Afrika. Lakini alipewa kazi za kusuluhisha migogoro ya kisiasa ya Burundi na Kenya.
Wapinzani Burundi walilalamikia kuwa anapendelea chama tawala lakini hakuna aliyejali.